Prof. Mkenda: Kwenye elimu Rais Samia anaangalia kizazi kijacho na sio uchaguzi ujao

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,042
49,727
Uwekezaji wa Rais Samia kwenye Elimu unalenga matokeo ya mda mrefu na kwa faida ya kizazi Kijacho.Hayo yameelezwa na Prof.Mkenda wakati Akitoa muhtasari wa mafanikio ya Miaka 3 ya Rais Samia kwenye sekta ya Elimu.
---
DODOMA: Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda amesema kuwa faida na matunda ya uwekezaji unaofanywa katika Sekta ya Elimu na Rais, Dk. Samia Suluhu Hassan utaanza kuonekana 2030.

Waziri Mkenda ameyasema hayo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari Jijini Dodoma akielezea mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya Elimu katika kipindi cha Miaka 3 ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan.

Amesema kuwa moja ya jambo aliloelekeza Rais, Dk. Samia alivyoingia madarakani aliagiza kufanyike mapitio ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014 na kufanya mabadiliko ya Mitaala kuhakikisha elimu inaboreshwa nchini na kutoa ujuzi unaendana na wakati.

Waziri Mkenda amesema kuwa Rais Samia ni kiongozi anayeangalia kizazi kijacho na sio uchaguzi ujao. Amesema kuwa watu wangependa kiongozi afanye maendeleo yanayoonekana kama ujenzi wa madaraja, barabara na miundombinu mingine lakini Rais, Dk. Samia ameamua kuwekeza katika kujenga rasilimali watu na faida yake haiwezi kuonekana kwa sasa.

My Take
Nimewahi kusema Rais ambae ameleta Mageuzi ya ukweli kwenye jamii na Uchumi ni Samia.

1. Sera Mpya ya Elimu na Mitaala.

2. Maboresho makubwa kwenye sekta ya biashara ikiwemo kufuta na kulinganisha Mashirika ya Umma yanayoleta hasara

3. Maboresho ya kisera na uwekezaji kwenye Kilimo.

4. Bima ya Afya Kwa Wote.

5.Kuomarisha sekta binafsi kushika hatamu ya Uchumi eg DP World nk

6. Kuokoa Mbuga zetu Kwa kuwahamisha Wamasai wasiharibu Hifadhi,hapa wanapata vile ambavyo hawakuwa navyo mfano wanajengewa nyumba zaidi ya 7,000 na kupewa Ardhi.

7. Demoktasia na Uhuru wa Maoni.Alisema watu waandamane wakosoe ajue panapovuja.

8. Ameleta Mageuzi Kwenye Sera ya Ardhi ambapo Sasa Wabia(Wawekezaji Wanaweza Nunua Ardhi au Kuwekeza kwenye Ardhi).
9.Kutungwa Kwa Sera ya Matumizi ya Nishati Safi ikiwemo mfuko wake.Lengo ni ifikapo 2030 88% ya kina Mama wawe wanatumia nishati safi na kuondokana na Kuni ambazo husababisha vifo Kwa watu zaidi ya 35,000 Kwa mwaka.

Hayo ni Baadhi tuu ambayo Samia amefanikisha kati ya mengi ndani ya miaka 3.

Siri ya yote hayo ni kwamba Samia anajua kutafuta pesa, hongera sana kwake 4Rs zimelipa.

Screenshot_20240318-073332.jpg
 
DAR ES SALAAM: WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) amesema wanataraji kuajiri walimu wasiopungua 10300 ili kuendana na mabadiliko ya sera ya elimu na mafunzo ya mwaka 2014 toleo la mwaka 2023 na mitaala ya elimu kwa kidato cha tano.

Waziri Mchengerwa amesema hayo leo katika ofisi ndogo za TAMISEMI, Kivukoni, Dar es Salaam
 
Mama amelivunja hilo fupa la Mtaala,Sera ya Elimu ya mwaka 2014 ilikuwa kizungumkuti Kwa Marais waliopita kabla yake,ilihitaji kichwa hasa na Waziri na Makatibu wakuu wanaojielewa Kuja kuanza kufumua hii Elimu ya kijinga iliyopitwa na wakati.Tusisubiri aondoke madarakani au afariki tuseme Bora Samia.Mahali anapostahili pongezi Wakati ni huu wa kuzitoa tusisubiri Kuwa wanafiki.Wenzetu tunaowasifia wamefikia walipo Kwa sababu ya rasilimali watu.
 
Mama amelivunja hilo fupa la Mtaala,Sera ya Elimu ya mwaka 2014 ilikuwa kizungumkuti Kwa Marais waliopita kabla yake,ilihitaji kichwa hasa na Waziri na Makatibu wakuu wanaojielewa Kuja kuanza kufumua hii Elimu ya kijinga iliyopitwa na wakati.Tusisubiri aondoke madarakani au afariki tuseme Bora Samia.Mahali anapostahili pongezi Wakati ni huu wa kuzitoa tusisubiri Kuwa wanafiki.Wenzetu tunaowasifia wamefikia walipo Kwa sababu ya rasilimali watu.
Wenye akili tuu ndio wanamwelewa Samia
Screenshot_20240318-073332.jpg
 
Back
Top Bottom