Hizi ni hoja zilizoibuka mara tu baada ya Kikwete kumaliza hotuba yake! Wewe una hoja gani?


- Kitendo cha Warioba kuwasilisha Rasimu mbele ya Bunge kinahitimisha rasmi kazi ya Tume. Kazi inayofuatia ni ya Bunge!

- Niliwaagiza Tume kuiweka Rasimu ya Katiba Mpya kwenye Tovuti ili wananchi waweze kusoma na kutoa maoni yao!

- Nawapongeza wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwa kazi nzuri waliyoifanya. Haikuwa kazi rahisi

- Tume ya Mabadiliko ya Katiba imepokea maoni 772,211 toka kwa wananchi na kuyafanyia uchambuzi wa kina!

- Tume imefanya kazi nzuri, yenye manufaa kwa watanzania. Rasimu imeandikwa vizuri na mapendekezo yanayofaa! - Kikwete.

Jk alikuwa anang'ata na kupuliza, kama panya!
 
- Masikini wa Mungu binadam asiyekuwa na msimamo, kwanza alikuwa Adui wa Lowassa kila siku kumchafua kwenye magaeti yake, ghafla akabadilika na kuwa Rafiki wa Lowassa na kuanza kuitukana sana Serikali ya sasa aliyokuwa akiisifia sana alipokuwa adui wa Lowassa, sasa amekuwa adui wa Serikali ya sasa aliyekuwa akiisifia kwa nguvu zake zote,

- Gazeti lake limefungiwa kwa kuandika uzushi kila kukicha uzushi, hivi kweli ulitegemea aende kwenye TV ya Taifa amsifie Rais au akubali hoja zake? Jamani naomba mwneye CV yake aiweke hapa ili tujue elimu ya tunayemjadili!!

Le Mutuz

Ujue wazi kuwa kiUMRI ww ni sawa na baba yangu.. ila tatizo lako kuu ni UJUHA. Na pia huwezi kuwa against na mfumo qa kidhalim uliokufanya uwe hvyo
 
Pamoja na kuandaliwa spich alipaswa aongezena akiki yake. Huwezi kumteua mtu kufanya kazi halafu ukapingana na matokeo ya kazi yake. Ameonyesha udhaifu mkubwa sana na badala yake alipaswa kumpongeza Sinde kwa kazi aliyofanya.
 
Punguza unafiki, kama huwezi kuacha kabisa.

Naona umekushuka, hoja zimekushinda, hayo ni baadhi ya mambo yalioongelewa na kikwete jana. Umeshindwa hoja sasa unanivaa mimi?

Chunga adabu yako kama huna hoja kaa kimya.
 
- Masikini wa Mungu binadam asiyekuwa na msimamo, kwanza alikuwa Adui wa Lowassa kila siku kumchafua kwenye magaeti yake, ghafla akabadilika na kuwa Rafiki wa Lowassa na kuanza kuitukana sana Serikali ya sasa aliyokuwa akiisifia sana alipokuwa adui wa Lowassa, sasa amekuwa adui wa Serikali ya sasa aliyekuwa akiisifia kwa nguvu zake zote,

- Gazeti lake limefungiwa kwa kuandika uzushi kila kukicha uzushi, hivi kweli ulitegemea aende kwenye TV ya Taifa amsifie Rais au akubali hoja zake? Jamani naomba mwneye CV yake aiweke hapa ili tujue elimu ya tunayemjadili!!

Le Mutuz

Kweli wewe ni mpuuzi na mzandiki kweli, yani umevimba mishipa ya shingo hapa unajadili mtu badala ya kujadili hoja zake???
 
Ilikuwa ni kati ya hotuba za hovyo kabisa kutolewa na mkuu wa nchi kwenye ufunguzi wa mjadala mkubwa wa kitaifa. Hakustahili kutoa maoni yake kuhusiana na mapendekezo ya tume. wala hakustahili kufanya kazi ya kujibu hotuba ya Warioba. Kitu alichostahili zaidi kukizungumza ni msimamo wa serikali, na jinsi ilivyojiandaa na itakavyoweza kusimamia mchakato mzima wa upatikanaji wa katiba mpya. Pia alistahili zaidi kukazania uhuru wa maoni na kuheshimiana wakati wa zoezi zima. Aliyasema haya mwanzoni vizuri (nahisi alifundishwa), baadaye akarudi kwenye asili yake - ambapo mara nyingi Rais wetu hupenda aonekana si mnyama wala si ndege wakati ni dhahiri kuwa yeye ni mnyama.

Hivi kuna mtu aliwaza raisi huwa hana msimamo wake ktk masuala km haya? Amesema maamuzi ni ya wajumbe. Yeye katoa angalizo kwa mtizamo wake. Tusijipe hofu tufanyie kampeni tunayoamini na tuwe tayari kwa matokeo yoyote. Aliyosema JK wengi walitarajia.
 
mimi huyu jamaa yenu sio rais wangu kuanzia alipotoa ile mipasho yake na ngonjera..

sitaki kuwa na kiongozi wa hivi hta leo nikiulizwa na mgeni yeyote rais wako ni nani jibu ni " nchi yetu ina kiongozi wa chama ambae ana act kama rais but for real hana interest na nchi wala wananchi wake.
 
Kubenea naye kama mwandishi akitambua majukumu ya chombo cha habari ameegemea msimamo wazi wazi sasa kwa nn ana mlaumu Jk? sasa kama watu wenginE kama cc wananchi wa kawaida tumeelewa Hotuba ya Rais kwa nn yeye kama mwandishi anataka kupotosha kwa makusudi?
Labda huyu kabenea amesahau kazi yake au ameichoka na anatamani kuvamia kazi nyingine kinyemela.yeye ni mwandishi wa habari.anachotakiwa ni kutuarifu aliyosema Mh Rais wetu na si kutupatia hadidhi zake.hatujamchagua, hajaomba kuchaguliwa na hatujamkabidhi dhamana yeyote.Rais tumemuelewa.
 
Hotuba haikunisisimua hata kidogo kwani aliyokuwa akikazia kwangu mimi ilikuwa kinyume. Waziri kutokuwa mbubge kunaongeza uwajibikaji. Vipndi 3 vya ubunge inatoa fursa kwa vijana nao kupata nafasi ya kuongoza nchi. Kuruhusu Zenj kuwa na katiba yake inamaanisha imekua nchi kamili je bara itatambulikanaje kama haina katiba yake? Muungano unahusika na maeneo machache je hayo mengine kwa bara itakuwaje?
 
Hivi kweli mkulu alihitaji masaa 2: 30 kuzindua bunge maalum la katiba? La hasha! Alikwenda pale kutoa maoni ya kama mwenyekiti wa CCM. Akikwenda pale kuonyesha jinsi ambavyo tume ya Warioba imetumia vibaya pesa za wananchi kwa kuleta rasimu mbaya na isiyo na maslahi kwa wananchi. Alikwenda pale kueleza msimamo wa CCM wakati ambapo alipaswa kutoa hotuba fupi tu ya kuzindua bunge; alikwenda "kubrainwash" wajumbe wa bunge maalum kwa kuikandia tume aliyounda mwenyewe!

JK ni janga kweli kweli lakini ndo mtaji wa CCM; ndiyo maana kanuni ilivunjwa ila Warioba aanze na baadaye JK asawazishe.

Dah, kweli huyu mkulu wananchi tumeingia mkenge.
 
Sababu unazo au unafuata mkumbo? Kama unazo hebu tuambie "Serikali 3/Nchi 3" zitaondoaje umaskini? Au mwenzetu ukisoma Neno Tanganyika kwenye vitabu ndio kichwa kinatulia?
Hata serikali mbili zimetokota mkuu kuondoa huo umasikini.Mtanzania sasa anaelekea kwenye maisha ya kuishi kwa chini ya nusu dola kwa siku-Mkuu unataka tufikie 0 ndo tufikirie mabadiliko?
 
Ilikuwa nzuri sana. JK ni mtaalamu wa kujenga hoja na kuitetea. Ni rahisi sana kuielewa hotuba ya rais kwani kila atoapo hotuba hujaribu kufanya watu wote wa rika zote, wasomi kwa wasio wasomi kuelewa anachoongelea. Mi nasema Bravo JK!
 
Lazima tutambue kuwa kila mmoja alipewa nafasi kupeleka maoni yake kwa jaji warioba sasa sioni mwanga huko tuendapo kama watawala wenyewe ni akina kikwete
 
Sitakosea tena kupigia kura mgombea urais anaetokea sehemu za Mwambao wa Pwani, au maeneo ya beach!!! Duuh nimejuta!! Uswahili swahili, majungu majungu, ujanja ujanja, umbea umbea,nk. Sasa hapa najua J3 tutaanza moja/upya kukusanya maoni tena.
 
Sitta aliogopa,maana pale alikua na wasiwasi ajui Kikwete angezomewa WAPI,angeweka mda wa ziada na JK kuzomewa, kesi itakua kwa Sitta,maana siku Ile Warioba yeye alikua anaongea tu,hivyo Sita akacheki time,akaona aongeze,ila JK kalalamika muda haotoshi na ana mengi ya kusema,Sitta kauchuna Tu
haha...Warioba aliongezewa muda kwa mbwembwe..as if walikuwa akipenda sana..Ila JK aka[iga fix kuwa ana mengi ila muda hautoshi..halafu akaendelea na pumba..sitta hata kubeep kuwa muda uongezwe wapi.Niliwaambia watu uwepo wa sitta hauna faida sana kwa CCM kwani wenye kujua wapi pa kumkandamiza ..hakuona shida..
 
Mimi napenda Serekali 3 lakini namuunga mkono Rais kwamba hofu zilizoonyeshwa na tume zipatiwe majibu ya kina. Tume haina majibu na muda wake umeisha.kama tume ingekuwa objective baada ya kupendelea serekali 3 wangeshauri mchakato usimame Tanganyika itunge katiba yake.ilivyo sasa katiba ya Tanzania inatungwa ili iwiane na katiba ya Zanzibar.baadae Tanganyika italazimishwa kutunga katiba inayokubaliana na ya Muungano na ya Zanzibar.hii ni kuinyima Tanganyika haki.tume imependelea au imejipendekeza kwa Zanzibar.bunge liwe makini.kwa nini tuwe na nchi mbili alafu uraia mmoja.Mfano Zanzibar ikijiunga na oic itahusu raia gani.sio Watanganyika!
 
Back
Top Bottom