Hizi ni hoja zilizoibuka mara tu baada ya Kikwete kumaliza hotuba yake! Wewe una hoja gani?

Moto unawaka leo Star TV kuhusu hii mada na Saed Kubenea anampa Kikwete za uso kwa hotuba aliyoitoa pale bungeni jana lakini Tanesco wamezima umeme pande za Arusha naona wameshtukia hii ni noma!
 
Alishasema hayo mengine yatafanyika akiondoka madarakani. Anaogopa mzimu wa Nyerere kumrudia.
 
Binafsi ningependa kuona ushindani wa kimaendeleo kama ilivyotokea kwa korea kusini na hongkong, urusi na ukraine na mifano mingine mingi.
 
Hukuna alichoongea cha maana zaidi ya kuwaeleza wajumbe kuwa wasiweke ukomo wa ubunge kwasababu riz1 bado ni mdogo ataweza ongoza vipindi zaidi ya 6.
 
Tatizo lenu chadema siasa zimewashinda mnachofanya sasa ni riot.mlipanga kuzomea mmeshindwa,najua sio kwamba wengi wenu hampendi serikali 2 bali tu kwa kuwa ndio msimamo wa ccm.kwenu mnapingana na ccm hata kama wana wazo zuri.kama ccm wangesema serikali 3 nyie mngeshabikia 2.nyie ni watu waajabu sana.tukiwasikiliza nyie hatwendi popote.
 
Rais kikwete wananchi tulishamaliza kutoa maoni kwa tume.usiturudishe nyuma.rasimu iliyopo ina maoni ya wananchi.nashangaa leo unatudharau wananchi.na dharau za wana ccm zinakera sana.kama jimbo la chalinze lililotoa rais leo huko hamna amburance tulisikia mwanao anaahidi unategemea ccm mna nia ya dhati na sie?.pitisheni serikali 2 muone mziki wake.leo hautaki ukomo wa ubunge kwa kuwa unataka mwamao riz awe mbunge wa maisha chalinze.hatukubali.
mimi ni mmoja wa watanzania walio pendekeza serekali tatu kwenye tume ninacho tofautiana nao ni mfumo mimi nilipendekeza kuwe na rais mmoja wa jamuhuri ya muungano na apewe meno ya kusimamia serekali kuu alafu zanzibar na tanzania bara ziongozwe na mawaziri wakuu ambao ndio watakuwa wasaidizi wa kuu wa rais na watashughulikia tamisemi hayo ndiyo maoni yangu kwa serekali tatu
 
Nilitegemea sAna mkuu wa nchi kuzinduabunge na si kuchambua Rasmu na kuelezea msimamo wa chama chake. Lakini akionesha kujikanganya mh. Dr. Kasema kila mtu ajadili kama yeye na si kujadili kwa kuambiwa. Lakini wakati kadhaa yeye na Nape na wengine wameeleza msimamo wa CCM ambao tiyari wamewambia wajumbe ambao ni wana CCM kuufuata je hapo hawajachaguliwa la kusema? Bado wangali huru?.

Suala la pili ni kuhusu mawaziri kutokuwa wabunge hapa naona Rais kapotosha. Anasema mawaziri kama si wabunge hawawezi kwenda bungeni kujibu maswali na hoja hii si kweli. Mfano mzuri ni AG (Mwanasheria Mkuu wa Serikali) . Huyu jaji Werema ni mbunge wa wapi?. Mbona anakuwa bungeni na anajibu hoja na maswala kadhaa ya kisheria bungeni. Naamini utaratibu unaomwingiza AG bungeni na kumpa nguvu ya jushiriki kikamilifu unaweza pia kuwaingiza mawaziri ambao si wabunge na wakashiriki kikamilifu kabisa. Lakini pia kuwapa wabunge nafasi nzuri ya kuisimamia serikali. Sasa mbunge huyo huku mwakilishi wa watu wake huku serikali hapa ufabisi utakuwa mbovu. Ni sawa na padre amewekwa wakfu kuwa Padre lakini anataka wakati mwingine awe ni muumini na aoe. Kwa hiyo watanzania waelewe kwamba hapa ukweli ni kwamba mawaziri wanaweza kabisa wasitokane na wabunge na bado wakashiriki kikamilifu bungeni. Swala la msingi ni kuweka mfumo wa katiba vizuri utakaowaruhusu kama ilivyo kwa AG saaa.

Swala la tatu ni kuhusu serikali ya shirikisho kutokuwa na raslimali na kukopesheka. Rasimu inataja ardhi iwe ya muungano. Sasa hii si rasilimali kubwa ambayo ndani ya ardhi kuna madini' maziwa, bahari, milima, mito, mabonde, misitu na kadhalika. Kuna rasilimali kubwa zaidi ya hii. Sikuweze kumwelewa DR kama analiona ili au basi yawezekana katika kusama aliliruka au alilisoma kwa bahati mbaya maana alisema serikali ya muungano itakuwa na eneo lote la tanganyika na bahari yake na sehemu yazanzibar na bahari yake. Sasa tena akashauri na mambo kama maziwa na mito na milima nayo yatajwe. Sasa hapa serikali ya shirikisho itaweza kupata mapato na kukopa.

Swala la tatu ni ukomo wa ubunge Hilo Mimi naona liwe na ukomo kama tume ilivosema ila ukomo huo uwe wa vipindi viwili vya miaka kumi kumi yaani mbunge awezi kugombea jimbo lake na mzunguko wa maraisi wawili iwe 5 *4=20.

Nne kuhusu Zanzibar kujiunga na mashirika na jumuhiya za kimataifa. Hivi zanzir ikijiunga na baadaye Tanzania ijiunge haoni mkanganyiko. Maana Tanzania ikienda huko itakuwa inawakilisha Tanganyika na Zanzibar wakati huo Zanzibar ilishajiunga. Hapa cha msingi na Tanganyika iwe na nguvu za kujiunga yenyewe kama Zanzibar itakavyokuwa na haki hiyo.

Kuhusu mafuta na gas amelisema vizuri bila kujielewa. Leo Zanzibar ikiruhusiwa kuchimba mafuta na Gas basi itatumia mapato yatokanayo kwa ajili ya Zanzibar vivyo hivyo Tanganyika iwe na uwezo wa kutumia yatokanayo na madini na rasilimali zingine kwa ajili ya Tanganyika na si kwa ajili ya Tanzania ambapo tayari itakuwa ni kwanba cha Zanzibar wanatumia kwa ajili ya Zanzibar halafu Cha Tanganyika kinatumika kwa ajili ya Tanganyika na Zanzibar kama mfumo ni wa serikali mbili.

Suruhisho hapa ni serikali 3 au moja ila miundo mingine itazidi tu kulalamikiwa.
 
Mi nilitegemea angalau Rais aje na ujasili wa kutuambia kwake anaona kuondoa huu mkanganyiko suluhisho ni kuwa na Muungano wa serikali moja.Kumbe naye mwoga tu kama tulivyo sote waoga wa kuliogopa hili kwa kuwaona Wazanzibar watatuchapa.
 
Wakati jaji warioba anakusanya maoni ya wananchi kuhusu katiba mpya kikwete alikuwa kasafiri kwenda nchi gani vile!!!!!!
au ni Jamaica kwenda kubembea.
 
Zito, kama unataka huruma utapata tuu, lakini serikali 3 sahau kbs , Historia , umri na utamaduni wetu utavurugika kwa kuwa na serikali tatu.
Ni kweli mkuu, utamaduni wetu wa kubebana, kutosema ukweli, kutetea maslahi yetu, kuunda tume ambazo zinakuja na jibu lile lile na watawala na siyo viongozi wetu kuukataa ukweli.

Kinachofanyika sasa ni kuficha funzo miguuni kwa kuvaa viatu.
 
samahani ndugu, unatumia nini kufikiria?nadhani kama hoja ni wachache waliohojiwa, basi katiba yote haifai maana haiwezekeni vipengele vingine mnasema waliotoa maoni wamewakilisha wananchi na hiki cha muungano hawawakilishi, yaani kuona tu dhaifu kaongea umekopi na kupaste, basi tupige kura nchi nzima
jk mwenyewe alichaguliwa na watanzania 5,000,000 kati ya 40,000,000 walio kuwepo wakati hivyo urais wake ni batili kwani alichaguliwa na watu wachache kwelikweli
 
Ukweli nikwamba watanzania walio wengi wanataka muundo wa serikali tatu ukiachilia wachache wanaopendekeza serikali moja na wengi ambao wengi wao ni wanachama watiifu wa ccm,wanapendekeza serikali mbili. kiukweli kila mmoja ana hoja yake tena inamantiki kuliko ya mwenzake.
kiukweli binafsi nimeona kunakitu hakiko vizuri katika serikali ya tatu ambayo itaitwa ndiyo ya muungano(tz). Binafsi nimeliangalia aswa katika namna ya kumpata ama kuwapa kiongozi atakaye ongoza serikali ya muungano,je,njia gani itatumika kumpata huyo kiongozi
1)kwanjia ya kupigiwa kura kutoka katika nchi za muungano ama
2)kwa njia ya kupokezana vijiti kutoka tanganyika na kumpa zanziba?

Angalizo kama kwa njia ya kupiga kura je hakutokea kwa tannganyika kutoa kiongozi mara kwa mara kutokana na wingi wa watu wake?
 
Nilisha sema JK nikinyonga kwani utumbo huo si ulitegemewa! ila hayo ni mawazo yake wa2subirie kula ya Maoni lazma kitaeleweka tu! tutaka mawazo yetu na sio ya MACCM
 
hivi Mch. Mtikila hajajiuzulu tu toka ktk hili bunge baada ya hii hotuba ya JK jana? msimamo wake tangu awali ilikuwa ni uwepo wa serikali ya tanganyika vinginevyo angejiuzulu na kurudi dsm aendelee na shughuli zake

Mtikila humjui ndugu. Yule ni mchumia tumbo tu hua hamaanishi kile anachokipigia kelele.
 
Nashauri wajumbe warudi tu maeneo yao maana hakuna katiba Mpya hapo dodoma
 
Kweli watanzania ni kichwa cha mwenda wazimu, wapo kama bendela fuata upepo, na ninaimani kuwa wanaotaka selikari tatu hawajalichunguza na kulifikiria kwa undani jambo hilo, ni bora useme selikari moja kuliko selikari tatu, ukisema selikari tatu ni sawa na kuvunja muungano na kila upande kujitenga na mambo yake, Ushauri wangu wangu kwa selikari iliyopo iitishe uchaguzi nchi nzima ipigwe kura kuchagua
SELIKARI 3
SELIKARI 2
SELIKARI 1

Na hapo ndipo watakuwa na jibu la pamoja kuwa watanzania wanataka selikari ipi,
mimi binafsi nataka selikari 1

suala la serikal moja linakuwa gumu hata kulitaja tu kwa sababu wazanzibar hawalitaki, wanataka zanzibar iwe nchi kamil inayotambulika sasa ikiwa serikal moja, zanzibari itamezwa na tangnyka hapo ndipo wanapokataa, ila upande wa tanganyka suala la serikal moja linakubalika, lakini hatuwezi kulipigia debe wakati upande wa pili hawautaki mfumo huo kwa kuhofia nchi yao kufutika na kuwa mkoa.
 
Back
Top Bottom