Hivi watawala wetu wapo "serious" kweli Katika kujibana na kujinyima Ili kukabiliana na kupanda Sana kwa bei ya mafuta Duniani?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,484
30,156
Nimeisikiliza hotuba ya Rais Samia, aliyoitoa jana, kuhusiana na kilio cha wananchi kuhusu kupanda Sana kwa bei ya mafuta Duniani.

Katika hotuba hiyo nime-highlight, jambo muhimu Sana aliloliongelea, anasema kuwa ni LAZIMA watendaji wa Serikali, TUJIBANE na KUJINYIMA, Katika kipindi hiki kigumu, ambapo wananchi wetu wanakabiliana na Hali ngumu Sana ya uchumi, kutokana na kupanda huko kwa gharama za mafuta, ambako kumesababisha bei mbalimbali za vitu kupanda, ikiwemo kupanda nauli kwenye vyombo vya usafiri

Nimekuwa najiuliza mbona Rais Samia, wala Waziri Makamba, sijawasikia Katika hotuba zao, hatua wanazochukua Katika KUJIBANA na KUJINYIMA Katika kipindi hiki kigumu?

Je inamaana hiyo Hali ngumu ya kupambana na Hali ngumu ya kiuchumi, tumeachiwa sisi wananchi wa kawaida pekee, itutese na kutuangamiza?

Siyo siri tena wananchi tunaojua kuwa Katika kila lita moja ya mafuta ya Petroli , ambayo inauzwa zaidi ya shilingi 3,100, zaidi ya shilingi 700 ni tozo mbalimbali za Serikali, ambazo tozo hizo ndiyo ambazo CAG Katika ripoti yake ya kila mwaka, ameelezea kuwa mabilioni ya shilingi, yanatafunwa na wajanja wachache, tuliowakabidhi dhamana hizo za ofisi za Serikali!

Mbona Rais Samia, hajafuata mfano wa Rais wa awamu ya kwanza, Mwalimu Nyerere, ambaye yeye kila alipokuwa anahutubia Taifa kuhusu Hali ngumu ya uchumi, yeye alikuwa wa kwanza kujipunguzia mshahara wake!

Tunaendelea kuwaona waheshimiwa wetu wabunge wakiendelea kuishi Maisha ya kifahari mno wakiendeshwa kwenye magari ya kifahari mno, Land cruisers "V-eite" zinazogharimu pesa ya walipa kodi wa nchi hii zaidi ya shilingi milioni 400 kwa kila gari moja!

Vile vile waheshimiwa wabunge wetu wanapokea mshahara wa zaidi ya shilingi milioni 12, bila kukatwa kodi yoyote, kwa Kila mwezi, licha ya posho zao kubwa za shilingi 300,00 kila "anapoketi" kwenye kikao cha Bunge kila siku!

Hivi tunaojibana ni sisi tu wananchi wa kawaida, wakati wenzetu watawala wetu wakiendelea kula STAREHE, pamoja na kipindi hiki kigumu Sana cha uchumi kinachotukabili?
 
TUPUNGUZE MAGUMU YA MAISHA

Screenshot_20220510_112835.jpg
 
Siasa tu hizo, hakuna kujibana hapo.

We fikiria tu alhamisi wiki iliyopita jumatatu alikua Dodoma, jumanne akawa dar, jumanne hiyohiyo akaenda Arusha, jumatano akarudi Dodoma. Iijumaa akaenda Zanzibar, jumapili akaenda dar, Leo jumanne kaenda Uganda.
Aisee........
Inasikitisha Sana🥺
 
Nimekuwa najiuliza mbona Rais Samia, wala Waziri Makamba, sijawasikia Katika hotuba zao, hatua wanazochukua Katika KUJIBANA na KUJINYIMA Katika kipindi hiki kigumu?
Huwa wanaongea maneno ya jumla jumla tu. Ni maneno matupu
 
Siasa tu hizo, hakuna kujibana hapo.

We fikiria tu alhamisi wiki iliyopita jumatatu alikua Dodoma, jumanne akawa dar, jumanne hiyohiyo akaenda Arusha, jumatano akarudi Dodoma. Iijumaa akaenda Zanzibar, jumapili akaenda dar, Leo jumanne kaenda Uganda.
Duuh Toomuch
 
Back
Top Bottom