Hivi, wanaume wa humu mkoje?

Hivi, wanaume wa humu mkoje?

NRNE

Samahanini kama ntakuwa nawakwaza kwa kuliongea hili wakuu, binafsi nimesikitishwa sana na hii tabia ambayo baadhi ya wanaume wanayo humu.

Ukija kuomba ushauri kuhusu mahusiano humu kuna baadhi ya members wakiume watajifanya wanaguswa na unayoyapitia na watakuonea huruma na kukufata PM, na kuanza kukuaproach.

Hii tabia sijaipenda kwasababu mimi nakuwa nimekuja kuomba ushauri nisolve tatizo langu na siyo kuja kutaka mpenzi mpya, na kuna baadhi ya members siyo wastaarabu anakukutumia na meseji huko PM akiona hujibu anakutukana kabisa, guys badilikeni hakuna mwanamke atayempenda mwanaume asiye mstaarabu.

Najua wanaume wastaarabu wapo wengi tu humu,... ila hawa baadhi wanawaharibia sifa haswa haswa hawa wanaoenda kukutana na members wa kike na wanakuja kujigamba huku jukwaani, binafsi siwezi kuwa na mtu humu kwanza hamko serious it seems kila mwanamke mnamfata huko PM.


Muwe na mchana mwema😍
Kutongozwa ni kesi??! Wakatae tu. Waambie Hapana. Au ni lazima kujibu messages zao?
 
Nikajua ni mimi pekee tu ndio ninayeshangazwa na hili...

Yaan kabisa mtu anakomaa anatongoza ID bila hata kuwa na uhakika 100% kuwa anayewasiliana naye ni mwanamke? Inashangaza na inasikitisha jinsi vile wanaume wenzetu baadhi wa humu walivyo desperate.

Lakini pia inawezana hakuna kitu kama hicho, bali hii mada muhusika kaileta kwa kutafuta attention tu au kujipa self-validation kwamba na yeye ana soko.
Siwezi kufanya kitu kama hiko mkuu, ni kweli kabisa wanaume wa humu wana hayo mambo hadi nimeshangazwa, sina haja ya attention yoyote humu
 
Huu mwezi wa August naona umeongoza kwa mambo ya inbox kuja public.
Hii inashiria jinsi gen Z haina kifua cha kutunza siri.

We unahisi ukisema ndio hawatakuja?
Ungefunga PM bila kelele ungepungukiwa nini?
Nimefunga na kelele ili wasisogee kabisa
 
Back
Top Bottom