Baba " mwanangu upo tayari taratibu za ndoa ziendelee'' @Etugrul bey" ndio baba''

Etugrul Bey

JF-Expert Member
Aug 6, 2020
3,496
6,451
Hii ni story ya kweli ya ndoa yangu iliyodumu kwa miaka Saba (7)....lengo la kuandika bandiko hili ni Kwa wadau ambao wanataka kufunga ndoa au kuingia katik Maisha ya ndoa..wajifunze kitu Fulani hapa

Kabla ya kukutana na mke wangu nilikuwa katika mahusiano na binti mmoja hivi....lkn mahusiano yetu haya kuwa mazuri Kwa maana mwenzangu alikuwa na option nyingi na hivyo kushindwa kujua yupi anafaa kuanza nae Maisha ya ndoa...hivyo baada ya kuona mwenzangu haeleweki nikaona isiwe tabu nikaachana nae na kuendelea na Maisha mengine.

Mara paap .....nikakutana na mwanamke mwengine,kwakweli alinijali Sana na kunitreat vizur kiasi nikaona mapenzi si ndo haya sasa...lkn kiukweli ni kosa kubwa Sana kuingia ktk uhusiano mwengine mara baada Tu ya kuachana na awali...kwani unaweza dhani unampenda mtu kumbe sio kweli,ni kwasababu Tu Kwa Wakati huo unapata faraja kwake.

KOSA NAMBA MOJA.....inashauriwa mara baada ya kuachana na uhusiano WA Kwanza usijiingize katika mahusiano haraka haraka take time na upate uhakika kama hisia zako ni za kweli....kwahiyo mm fasta nikaingia na ndani ya miezi minne tukakata shauri tufunge ndoa..lkn binti akasema tusi sex mpaka tufunge ndoa any way kwangu haikuwa na shida kabisa...tulichofanya tukapima afya zetu na kujua status yetu....lkn wakati matayarisho ya ndoa yanaendelea nikawa na mashaka na hisia zangu...lkn nikapuuzia Tu!
Wakati matayarisho yanafikia ukingoni napata uhakika sasa kuwa hapa hakuna hisia za kweli.......

Tafuta pop corn au karanga hapo Kwa mangi ushushie taratibu huku unakula madini....usiwe serious Sana kana kwamba unasoma tangazo la kifo au unaangalia dodoso la Sensa...just relax okaaay!

KOSA NAMBA MBILI....Kipindi cha mwisho mwisho cha maandalizi ndio hisia zangu zinakataa au zinanisaliti hivi hivi...swala linakuja nitaanzaje kuahirisha ndoa,nitamwambiaje mwenzangu na ndugu zangu pia....hlf kumbuka Mzee wangu aliniuliza my son tuendelee na taratibu za ndoa nikamjibu ndio! Halafu baadae nije na habari nyingine? Nikajisemea Baharia haogopi kuchafuka Kwa bahari lazima meli ikate Mawimbi Tu iwe mvua iwe jua!

Mungu mkubwa ndoa ikapita salama salimini,na Maisha ya ndoa yalikuwa na furaha Sana na Amani ,kifupi mke nilipata Sana Tu,anajali,msikivu na anajua nini maana ya kuwa mke. Tatizo baharia Mimi ndio hisia Kwa mke wangu sina....show zilikuwepo lkn sio zile zinazo takiwa haswaa....yaani mpaka nijilazimishe wkt Yale mambo yanatakiwa yaje automatic Tu kama kuvuta pumzi vile!

Mwenzangu akawa analalamika kuwa mbona tunaishi kama tumekaa kwenye ndoa miaka 20 vile au kama wazee vile Kwa maana hakuna maneno matamu ya mapenzi,simwambii kama nampenda daah ikawa changamoto...mtu mzima najitahidi kumwambia lkn baadae nasahau na hata nikimwambia naona unafiki Tu coz najua simaanishi....ukisikia mke na mume wanaishi kama house mate ndo hiyo sasa,yaan mnakula vizur,hakuna ugomvi na mnaishi vizur lkn chemistry hakuna.

Ndo baharia nikatafuta faraja nje ya meli ya yangu mwenyewe...nikachepuka lkn sijisifii Kwa hili hata kidogo kwani huu ni udhaifu mkubwa Sana...lkn ndo hivyo tena nimeingia Choo cha kike inabidi nichutame!

Chukua hii....watu mara nyingi huwa hawachepuki na watu wapya Ila ni watu wao WA zamani kwahiyo kuwa makini Sana na wapenzi WA zamani WA mtu wako...sio unaambiwa '' unajua huyu ex wangu ndio ananisumbua nilimwambia asinifuatefuate Ila mbishi tu'' nah aisee utapigwa na kitu kizito sasa hivi shtuka fasta.....hapa sikuchekupa na Yule mwenye option nyingi laa! ila kabla sijakutana na huyo aliye zingua,kulikuwa na mwingine pisi Kali ila level zake kubwa na alikuwa anafanya kazi hospital Fulani ushuani halafu yupo mapokezi just imagine anakutana na washua wangapi?

So nilimpotezea Tu kimya kimya lkn nilimtafuta Tu nipate faraja na bahati nzuri alikuwa hajaolewa bado....naogopa Sana wake za watu! Na ukisikia kila mtu na mtu wake ni kweli kabisa...Yani hii pisi kwangu haichomoi hata akiolewa na Putin Mzee wa KGB atajua anafanyaje ilimradi baharia Mimi nisihuzinike,ndio maana unakuta unaoa mwanamke unampa kila kitu lakini ana mtu wake daah Maisha haya!

Kiukweli nilikuwa namuonea huruma Sana mke wangu,,napenda kukiri wazi kama ningempenda kama ninavyotaka wallah ningekuwa mwanaume mwenye furaha Sana duniani,nakumbuka kuna wakati nilikwama mpaka kulipa Kodi ya nyumba ilikuwa tabu maana tulipanga nyumba nzima,lkn aliongea na familia Yao...kwanza walikuwa tayar kutupa Mda tukae ktk hiyo nyumba mpaka nitakapo kuwa vizur lkn kwenda kukaa Kule nikaona sio Sawa nikaona Bora apangishwe mtu then akilipa kodi tunachukua na kulipa huku walau inakuwa poa hivi..walikuwa na nyumba kadhaa za kupangisha hivyo akakubali wazo langu daah she is an angel kwakweli mpaka nilipo kaa Sawa alinistiri Sana.

Na ndani ya miaka Saba ya ndoa yetu sikuwahi kupata mashaka yoyote juu ya uaminifu wake na wala sikuwaza hata siku moja kupekua Simu yake,na alikuwa ananiambia ujue mume wangu wanawake wengi wanapenda Sana kuliwa lkn shukuru Mimi sipo hivyo...na nikweli hata ukiangalia tafiti mbali mbali wanawake wanapenda kuliwa na ndio maana wanawake walio ndani ya ndoa wengi wanachepuka Sana nje na sababu ni Sisi....tunajifanya tuko busy Sana,mara tumechoka plus hatuonyeshi mahaba kwao kwanini wahuni wasiruke nao!

Kibaya zaidi ikafikia kipindi wakati WA maandilizi dushe linasimama vizur lkn likizama baharini linanywea daah hapo ndo ikawa shida nyingine,kwahiyo nikawa namuwacha mwenzangu katika hali mbaya Sana,au nikipiga Gia namba moja basi ya pili ujue shughuli,sasa alivyokuwa analalamika namna vile ndo ugonjwa kwangu unazidi,Kwa maana nikawa nimeathirika kisaikolojia sasa,kwahiyo tukianza kufanya tendo kuna kitu kinakuja akilini kwangu...najiuliza je ikinywea tena itakuwaje nakweli Bana lile nililo waza linakuja vile vile tena....kwahiyo mwisho wa siku kujiamni kukaondoka kabisa,mwenzangu akanishauri nitafute dawa lkn binafsi najua tatizo liko wapi Kwa maana najua kabisa nipo fiti lkn hisia Kwa mwenzangu sina,na ndio maana nawashauri Sana wanaotarajia kuingia katika ndoa hakikisha unampenda haswaa unayetaraji kuwa nae,migongano mingine ktk ndoa ni ya kawaida Tu lkn ukikosekana upendo wa dhati basi ndio chanzo cha kukosa furaha ya kweli na kuchepuka kunaanzia hapo.

Ikafikia kipindi nikaona hapana ingawa sipendi talaka lkn siwezi ishi maisha ya uongo,sikupenda watoto wetu watatu ambao mmoja nilimkuta nae na wawili tuliozaa pamoja waishi Bila wazazi wao wawili lkn nikaona siwezi ishi ktk Maisha haya kwa kutafuta furaha Kwa mchepuko....na je nitaishi ktk Maisha yasiyo mpendeza mungu Hadi lini....nakumbuka hata mwenyewe alianza kuniambia ''au mume wangu huenda haujanipenda ndio maana huna hamu Sana na mimi'' natamani nimwambie ndio daah lkn nitaanzia wapi baharia Mimi!

Mwisho wa siku nikampa talaka,ingawa aliniambia siku ukipona urudi tuishi tena mume wangu...ishu ikaja je sababu ya kuwaambia wazazi wetu nimemuachia nini coz within seven good years hatujawahi peleka au kutokea ugomvi wowote mpaka ufikie Kwa wazazi...haikuwa na jinsi ingawa ni aibu ukweni ila ikajulikana Tu sina nguvu za kiume..kwangu aibu hiyo ilikuwa afadhali kuliko kuishi ktk ndoa ya kuiigiza,ingawa kwetu wazazi Tu ndo wanajua hiyo sababu ingawa nahisi Dada zangu wanaweza jua Hilo pia si jua bimkubwa na wanawe wa kike tena.

Ni miaka miwili imepita sasa tangu nimuache,tuna lea watoto vizuri Tu sometime mpaka kulipia Ada ananisaidia Kwa mapenz yake....na juzi Kati namwambia bimkubwa natarajia kuoa hivi karibuni kuna binti nimezaa nae mtoto wa kiume,akaumia Sana na kusema mzazi mwenzako vipi maana hata Leo hii yupo tayar umuoe tena...Kwa waislamu kama mwanamke umemuacha Kwa talaka moja au mbili unaweza kumuoa tena upya...ikabidi nimwambia mama ukweli kuwa Mimi sio mgonjwa nipo vizur Tu tatizo sijampenda Sana mwenzangu,ndo amenielewa Ila kumchana mshua ndo bado ila nitamueleza pia,Ila ndugu zangu waliumia Sana kumwacha mke wangu yaani anakubalika Sana.

Ila kwakuwa Mimi ni muislamu naweza kuwa na wake wawili nafikiria kama atakuwa bado hajaolewa na akiridhia uke wenza naweza muoa tena ingawa hapo awali alishaniambia kuwa ukioa mke mwingine mi natoka...huwezi jua with time huenda akakubali lkn akikataa Maisha lazima yaendelee!

Wakati naanza mahusiano na huyu mke wangu mtarajiwa sio Siri nilisha hasirika Sana kisaikojia lkn bahati nzuri nilimweleza kila kitu nikamtaka awe mvumilivu na anisaidie show zirudi kama kawaida...kweli mwanzoni ilinipa taabu lkn baadae nikawa Sawa na show show zimerudi kama kawaida tena Kwa ubora wake,kwahiyo wanawake wakati mwingine sio Kila mwanaume ambaye ana tatizo la nguvu za kiume ni mgonjwa laa! Saa nyingine kauli zako zaweza mfanya akashindwa kupafomu na kumsababishia matatizo ya kisaikolojia....jaribu Sana kumsoma mumeo na kumsaidia linapokuja swala hilo na mwisho wa siku ni show show!

Ni hayo Tu.
 
Kwahiyo huyo mkeo alishindwa kukusoma saiklojia yako au ulishindwa kuwa muazi kwake ili ajue jinsi gani yakukusaidia? Ila pole yake mkeo wa zamani, ila nionavyo mie shida wewe kumpenda sana usipopendwa.
Kwa mke wangu....kwakuwa lilikuwa ni tatizo la Mda mrefu kidogo ilikuwa vigumu kwake kunielewa ingawa nilijaribu kumuelewesha lkn hata hivyo bado kumbuka sina hisia nae kwahiyo bado ingeendelea kuwa tatizo Tu....Lau kwamba ningekuwa nampenda hata Mimi ningekomaa nae mpaka kieleweke lkn ndo hivyo tena Ulweso
 
Sawa bwana Hemedy PHD, naona unamuendekeza Abadallah kichwa wazi kuliko maisha, piga yope babaa

Sent using Jamii Forums mobile app
vanus Maisha ni pamoja na ndoa yenye upendo...tunaoa ili tupate Amani na furaha katika nyoyo zetu....kama mtu hupati lililo kusudiwa ndani ya ndoa basi hata maana halisi ya ndoa haipo.... asikudanganye mtu ndoa ni tendo la ndoa kama hiyo ndoa haina Jambo Hilo na wote ni wazima WA afya basi ni mtihani...matokeo yake unaenda unachepuka.

Najua kuna mtu aweza sema ungekaa nae Tu hivyo hivyo....ina maana nitaendelea kuchepuka na mwisho wa siku Nakutana na Mola wangu peke yangu...je nitakuwa ktk mazingira gani?
 
Kilichokukuta hata mm kilinikuta

Niliajiriwa sehem wakat tumefika tukakutana ajira mpya nikapiga dem then tukapotezana akarud na mimba miez mitatu ikabid nioe tu ila sikuwa nampenda wala kuwa na hsia nae
Aisee niliteseka alinitafutia tiba weee bila kujua me nje napiga show ya uhakiia

Badae ilibid nifunguke tukaachana yaan mkasa wako kama wangu 100% maana hata wangu alikuwa na mtoto tayali na pia alikuwa mke bana yaan mke kabksa kwa sifa zote za tabia
 
Nimejisikia vibaya sana. Yani wanawake wema hawanaga bahati. Itafika mahali binti yangu nitamwambia mwanangu bora uwe sister tu.

Makurumbembe ndo yanapata wanaume wema. Wanawake wema wanaishia kuachika tena unakuta hana baya. Mkuu jua tu nimejisikia vibaya.
 
Nimejisikia vibaya sana. Yani wanawake wema hawanaga bahati. Itafika mahali binti yangu nitamwambia mwanangu bora uwe sister tu.

Makurumbembe ndo yanapata wanaume wema. Wanawake wema wanaishia kuachika tena unakuta hana baya. Mkuu jua tu nimejisikia vibaya.
Utawa (sista) mtu hapangiwi, ni wito wake yeye mwenyewe kutoka moyoni mwake vinginevyo tutamkula tu kama tunavyowakula hawa masista jina tu huku parokiani

Ni Siri
 
Mwanamke wa awali alikuwa ni akili kubwa kukuzidi na mchepuko wake uliokuwa unamridhisha ulikuwa ni akili kubwa ndio maana pamoja na kutomridhisha kwako kitandani hukuwahi kuona sikitiko lake na ukitaka kuliamini hilo mfuatilie anayemrusha maji kwa sasa utajua muda tokea wameanza ni muda aliokuwa kwako anakuonesha upendo wa hali ya juu ingawa humridhishi...

The World Is Full Of Alternatives na katika miaka yako 7 ya ndoa jua kuna mwamba ambaye yupo Good Upstair alikuwa ana mi 5-6 yake humo humo sema wewe unajihisi alikupenda sana ila sio, ni alikuwa na akili nyingi sana. NdoaMakaratasi, Kila binadamu anahitaji kupewa raha na usipompa wewe ataipata kwingine sababu watu ni wengi sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom