nikiomba mwenyewe nitaupata huonuponyaji?? au kuna watu maalum
Swali mujarabu, nami nitajaribu kukujibu.
Ili maombi yako yapokelewe, ni lazima uwe na imani kuwa hakika uliyoyaomba yamepokelewa. Ukisoma Marko 11:24 inasema 'Kwa hiyo nawaambieni, mnaposali na kuomba kitu, aminini kwamba mmekipokea, nanyi mtapewa'.
Kwa hiyo lazima uwe na uhakika wa kuwa maombi yako yatajibiwa. Usiweke shaka yeyote.
Kama una imani na umejiunganisha katika jina la Yesu Kristo, katika yote uombaye naye atakujibu.
Kwa nini Kuna watu wakikuombea unapona au kufanikiwa katika jambo lako?
Ukweli ni kuwa unaweza kujiombea mwenyewe na usifanikiwe katika hitaji lako. Ila Kuna watu wa Mungu wakikuombea hapo hapo tatizo lako linatatuliwa. Je, kwa nini? Ni kwa sababu watu wamepewa vipawa na Mungu. Na kukemea pepo wachafu nao wakawatii. Lakini pia, watu hao wamejiunganisha karibu zaidi na nguvu za Mungu. Na ndivyo, maombi Yao husikika kwa uharaka zaidi. Wana elimu ya ufahamu wa neno na imani yao i thabiti. Wanafahamu ni namna Gani waenende katika Kila tatizo.
Mungu hapokei maombi ya wenye dhambi. Ila mwenye dhambi akikubali na kumkiri Yesu kuwa Mwokozi wake, naye humsamehe dhambi zake zote na kumfanya mwana wake. Na ukishakuwa mwana wa Mungu, yote uombaye kwa imani utapata.