Hivi vitu vina maana gani?

Hivi vitu vina maana gani?

Mawardat

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2021
Posts
28,958
Reaction score
147,860
Wassalaam,

Nina mdogo wangu yupo na miaka 13, kidato cha kwanza.

Huyu mtoto kiukweli ameteseka sana na baadhi ya mambo aliyoyapitia huyu mtoto yanatisha.

Alivyokuwa darasa la tano alipatwa na matatizo ya kuzimia,tatizo la kuzimia alianzia nyumbani na hiyo siku alikuwa katoka shule,alivyoingia ndani tulisikia akipiga kelele na kuanguka, tokea hapo alikuwa anazimia bila mpangilio hasa akienda shule hasomi.

Ikapelekea tukamuhamishiaa shule ya jirani na nyumbani,lkn kila akienda shule anazimia, Tumepambana sana na tiba na visomo lkn kama inapoa tu baada ya muda kinaumana tena

Alivyomaliza shule tukampeleka znz nyumbani kwaajili ya tiba, maana alikuwa akizimia anapandisha mashetani akizinduka anapotolea kusiko julikana. Kafanyiwa tiba znz na tukaambiwa kapona na hayawezi mtokea tena.

Karudi home, tumempeleka shule kaingia darasani wiki moja tu kimeumana tena kila akienda shule anazimia, Kiukweli tu, wenyewe tumeshachoka na hii hali ya dogo maana tumezunguka sana kutafuta tiba na visomo lkn hakuna wapi.

Wiki iliyopita kaanza kutumia maji na mafuta ya...

J,nne karudishwa shule kasema anakuhoa sana na mbavu zinambana na kuna kitu kimemkaba kohoni kama anataka akitapike.

Leo usiku baada ya kufuatilia maombi katapika vitu hivi.

Hivi kama kavitoa hivi inamaana hatosumbua tena?
 

Attachments

  • IMG-20230305-WA0000.jpg
    IMG-20230305-WA0000.jpg
    35.6 KB · Views: 94
  • IMG-20230305-WA0001.jpg
    IMG-20230305-WA0001.jpg
    96.9 KB · Views: 86
Uwepo wa mungu ni mkubwa...

Familia nzima inawapaswa kufanya maombi sana na kuendelea kutumia hayo mafuta kwa kunyunyiza(kumwaga) pande zote za nyumba hata hayo maji pia na kuongeza imani kwanye maombi huenda anaefanya hayo maovu hatokei mbali na familia yenu..

Poleni sana.
 
Back
Top Bottom