Hivi vitu vina maana gani?

Hivi vitu vina maana gani?

Wenye imani zenu samahani sana.

Wakati fulani huko nyuma yule mzee kakobe alikuwa akienda nje ya Tanzania kufanya mikutano hadi, wakati mmoja alienda Kongo ya DRC na kuwaombea watu magonjwa yao hadi kupona.

Ila kwa baadhi ya watu wanaofuatilia hizi mambo iko hivi, kuna magonjwa ya kupandikiza, haya magonjwa unaweza kuangaika sehemu zote duniani unapopajua wewe, ila sasa tiba yaje inakuwa lazima akatibiwe kwa aliyepandikiza huo ugonjwa.

Iliwahi fanyika na huyo kakobe huko kongo ya DRC ili watu wapate kumuamini na ilifanyika hivyo sehemu kadhaa na watu wameshuhudia, hadi sasa kwa kufupisha, huyo binti kapelekwa sehemu mbalimbali hata kwenye maombi ni bila bila ila mlipompeleka sijui kwa nabii gani akapona kwa kutoa hizo takataka.

Tayari imani kwa huyo jamaa inaongezeka na watu huwezi waambia lolote kumuhusu.

Na hii ndiyo dunia tuliyomo.
 
We Kuna mtu umemuona uchi kwenye kongamano la Mwamposa?au neno UCHI limepoteza maana?

Nataka tujadiliane kielimu. Niambie uchi kwa mujibu wa Biblia unasemaje au unaelezewa vipi ?

Kwanza tu Ile mtu kujiita nabii au Mtume, Hilo ni kosa la kwanza la kiufundi. Hakuna nabii wala Mtume katika mgongo huu wa ardhi kwa Sasa.

Kwa mujibu wa dini yangu wale wako uchi.
 
Swali mujarabu, nami nitajaribu kukujibu.

Ili maombi yako yapokelewe, ni lazima uwe na imani kuwa hakika uliyoyaomba yamepokelewa. Ukisoma Marko 11:24 inasema 'Kwa hiyo nawaambieni, mnaposali na kuomba kitu, aminini kwamba mmekipokea, nanyi mtapewa'.

Kwa hiyo lazima uwe na uhakika wa kuwa maombi yako yatajibiwa. Usiweke shaka yeyote.

Kama una imani na umejiunganisha katika jina la Yesu Kristo, katika yote uombaye naye atakujibu.

Kwa nini Kuna watu wakikuombea unapona au kufanikiwa katika jambo lako?
Ukweli ni kuwa unaweza kujiombea mwenyewe na usifanikiwe katika hitaji lako. Ila Kuna watu wa Mungu wakikuombea hapo hapo tatizo lako linatatuliwa. Je, kwa nini? Ni kwa sababu watu wamepewa vipawa na Mungu. Na kukemea pepo wachafu nao wakawatii. Lakini pia, watu hao wamejiunganisha karibu zaidi na nguvu za Mungu. Na ndivyo, maombi Yao husikika kwa uharaka zaidi. Wana elimu ya ufahamu wa neno na imani yao i thabiti. Wanafahamu ni namna Gani waenende katika Kila tatizo.

Mungu hapokei maombi ya wenye dhambi. Ila mwenye dhambi akikubali na kumkiri Yesu kuwa Mwokozi wake, naye humsamehe dhambi zake zote na kumfanya mwana wake. Na ukishakuwa mwana wa Mungu, yote uombaye kwa imani utapata.
asante sana mkuu, ubarikiwe
 
Wenye imani zenu samahani sana.

Wakati fulani huko nyuma yule mzee kakobe alikuwa akienda nje ya Tanzania kufanya mikutano hadi, wakati mmoja alienda Kongo ya DRC na kuwambea watu magonjwa yao hadi kupona.

Ila kwa baadhi ya watu walilifuatilia hizi mambo iko hivi, kuna magonjwa ya kupandikiza, haya magonjwa unaweza kuangaika sehemu zote duniani unapopajua wewe, ila sasa tiba yaje inakuwa lazima akatibiwe kwa aliyempandikiza huo ugonjwa.

Iliwahi fanyika na huyo kakobe huko kongo ya DRC ili watu wapate kumuamini na hadi sasa kwa kufupisha, huyo binti kapelekwa sehemu mbalimbali hata kwenye maombi ni bila bila ila mlipompeleka sijui kwa nabii gani akapona kwa kutoa hizo takataka.

Tayari imani kwa huyo inaongezeka na watu huwezi waambia lolote kuhusu huyo jamaa.

Na hii ndiyo dunia tuliyomo.
Lkn si anabaki kwa dini yake haina shida,
 
Nataka tujadiliane kielimu. Niambie uchi kwa mujibu wa Biblia unasemaje au unaelezewa vipi ?

Kwanza tu Ile mtu kujikita nabii au Mtume, Hilo ni kosa la kwanza la kiufundi. Hakuna nabii wala Mtume katika mgongo huu wa ardhi kwa Sasa.

Kwa mujibu wa dini yangu wale wako uchi.
Haya bwana hiyo ni kwa mujibu wa dini yako,mi kwa mujibu wa dini yangu yupo sahihi kabisa kila mtu aamini anachoamin
 
mpaka muda huu sijuu kama mwamposa anatumia nguvu gan kuna mtu kasema nguvu za giza kuna mtu kanielezea vzr sana so hebu chagua upande then nenda kwa imani
Madame S hii nguvu ya mwamposa inanitia shaka kidogo, maana yasije kuwa maajabu kama ya kina tb Joshua 🤔🤔
Zile pigo za kule Nigeria sio kabisa, ila hope tukipona. Hatuto sumbuliwa na majanga mengine

Ila mzima wewe rafiki, maana Ni muda Sasa toka tuongee🤔🤔
 
Swali zuri.

Huo unakuwa umepewa mtihani, kutokana na mapito unayo pitia.

Shetani yupo kwa ajili ya kuwapoteza watu, na alipewa uwezo wa kufanya maajabu, ndiyo maana Kuna marafiki wa shetani na Marafiki wa Allah. Ukisoma vitabu utakutana na habari zao.

Mchawi anatibu na anaponya, ila ukimuamini unakuwa umepotea na kukufuru, hapa ndipo Kuna mtihani na kunahitaji Elimu.

Kwenye kutoa ushuhuda, hapa hakuna hoja na Watu wame yaongelea sana, waja wema au watu wakweli hawana mambo ya ushuhuda na huwa hawataki kujulikana wakitenda maajabi waa hawajitangazi, bali wapo na wafanya haya mambo.
nimesoma cuba, nimekuelewa sanaa
 
Haya bwana hiyo ni kwa mujibu wa dini yako,mi kwa mujibu wa dini yangu yupo sahihi kabisa kila mtu aamini anachoamin
Ndiyo nataka uniambie Yesu hakuwaambia uchi ukoje sababu hili ni jambo muhimu sana.

Wewe tuachane na dini yangu, tuongelee kuhusu Biblia na Yesu anasemaje kuhusu haya yanayofanywa na manabii na kuhusu huo uchi.
 
Back
Top Bottom