Hivi unafiki itakusaidia nini? Tajiri vs Masikini

Freiston

JF-Expert Member
Oct 25, 2020
302
339
Kiukweli dunia ya sasa inashangaza sana. Kuna wakati nikaa na kutafakari mambo yanayoendelea katika dunia hii hasa hapa kwetu Tanzania naumia kiukweli.

Hivi siasa unafki utakusaidia nini? Nauliza hivi kwa sababu ni rahisi sana kwa masikini kumtetea tajiri ili apate zaid kuliko tajiri kumtetea masikini.

Ona kwa mfano, sheria zetu zimekuwa zikitoa adhabu kali kwa watu ambao huiba kidogo mf. Kuku, vyombo vya ndani n,k yaani wadokozi kuliko wale wanaiba mabilioni ya fedha za walipa kodi wa nchi hii. Ila cha kushangaza ni kuwa masikini huyu kibaka au mdokozi hupewa adhabu kubwa (labda miaka 20 au 30 jela) kinyume na kosa alilofanya wakati huyu tajiri anawezaiba bilioni na akaambia alipe milioni 2 au 3 anaachiwa.

UNAFIKI SASA:

Masikini huyu yuko radhi kumtetea tajiri huyo aachiwe huru lakini sio kumtetea masikini mwenzie. Inabidi ifike mahali watu tuone umehimu wa kuwasidia hasa hawa ndugu, jamaa, marafiki na majirani zetu kuliko hao tunawatetea lakini kesho anaenda kuiba tena hela ambayo inaifanya nchi yetu izidi kuwa masikini.

TUACHE UNAFIKI NDUGU ZANGU. Jiulize, ni lini sisi masikini tulitetewa na hao matajiri wakati tukilia shida? Masikini wa nchi hii ataendelea kuteseka mpaka lini?

Inabidi ifike mahali tujue namna ya kuondoa boriti zilizo kwenye macho yetu, kabla ya kuondoa kibanzi kwenye macho ya tajiri.

Naomba kuwasilisha....
 
Kiukweli dunia ya sasa inashangaza sana. Kuna wakati nikaa na kutafakari mambo yanayoendelea katika dunia hii hasa hapa kwetu Tanzania naumia kiukweli....
Mkuu ujamaa ulidaganya eti binadamu wote ni sawa na Africa ni moja huo ni uongo......Masikini ni nusu binaadamu, na ni shida/tatizo kwa serikali zetu za kiafrica na tunanyoonywa zaidi kuliko matajiri.
 
Tofauti ipo...

Tajiri anakuibia ma million bila kukudhuru... Kwa kutumia kalamu tu...

Masikini anakuibia Kwa kuacha uharibifu wa kukudhuru... ( Roba za mbao, bisi bisi, kuchomwa visu, kuburuzana )
 
Back
Top Bottom