Hivi Transcript ni haki ya Mwanafunzi kupatiwa na Chuo?

stow away

JF-Expert Member
Dec 5, 2022
8,887
17,546
Naomba kuuliza wadau kuhusu hilo suala la transcript zinazotolewa vyuoni, hizi transcript ni haki ya Mwanafunzi kupatiwa na Chuo au ni mpaka mwanafunzi afukuzane na uongozi wa Chuo ndio wampe transcript?

Nasema hivi sababu kuna Chuo X kilichopo maeneo ya Mkoa wa Dar es Salaam kinamzungusha mwanafunzi kumpa transcript yake huu unaenda mwaka wa Pili kila mwanafunzi akienda anaambiwa transcript haijaprintiwa bado Mara anaambiwa anaeprint hayupo amesafiri visingizio haviishi, sasa nauliza hizi transcript kutoka kwenye vyuo vyetu ni haki ya Mwanafunzi kupatiwa pale anapomaliza Chuo au ni mpaka aombe sana ndio apatiwe transcript yake ?!
 
Taja jina la chuo usadike sio dhambi usiogope

Sent from my V2026 using JamiiForums mobile app
Kuna mengi nitayaeleza baadae nikipata wasaa kuhusu huu mkasa Ila kwa sasa nilihitaji kujua km transcript ni haki au ni ombi, sasa km ni haki ikiwa km Chuo kimegoma kutoa transcript na kimeizuia, Mwanafunzi achukue hatua zipi ili apatiwe transcript yake ?
 
Kitaje,,,unazungumzia taasisi ya elimu. Itaje Kisha hiyo transcript atapewa.
 
Mkuu km unajua hatua za kufuata ili ipatikane elezea maana hapo ndio panaleta utata wapi pa kuanzia?
Kuogopa kutaja Jina la chuo inaonesha wewe ndio mwenye tatizo au pengine ni vile vyuo vya uchochoroni chumba kimoja floor ya pili.

Ili cheti kikamilike lazima upewe na hiyo Transcript hata gvnts huwezi kuapply kazi bila hiyo Transcript .

Sent from my SM-A025U using JamiiForums mobile app
Mwanafunzi hana tatizo maana alipoenda wamecheck mbele ya msajiri km mwanafunzi ana tatizo wakasema mwanafunzi hana tatizo lolote Ila sasa transcript kutoa na kumpa ndio inakua ngumu maana ipo ndani ya laptop inaonekana na mara zote amekua akienda anaonyeshwa transcript yako ipo hii hapa Ila kuiprint ili apewe ndio anazungushwa achukue hatua zipi ili aweze kupatiwa? Sio Chuo Cha kata ni Chuo cha Serikali
 
Kuna mengi nitayaeleza baadae nikipata wasaa kuhusu huu mkasa Ila kwa sasa nilihitaji kujua km transcript ni haki au ni ombi, sasa km ni haki ikiwa km Chuo kimegoma kutoa transcript na kimeizuia, Mwanafunzi achukue hatua zipi ili apatiwe transcript yake ?
Transcript ni matokeo yote ya chuo kwa mihula na miaka yako. Na ni haki yako sio ombi, kama inazuiliwa basi clearance haijakaa sawa yaweza kuwa unadaiwa bado lakini mdaiwa anatoa ubishi kuwa hadaiwi, hapo huwezi kupewa. Fanya clearance!

Back
Top Bottom