Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Watu wanasema suala la haki ya dhamana ni suala la katiba, hapana, mie napinga kwa nguvu zote kwamba hili ni suala serikali inapaswa kulishughulikia mara moja kwa sababu lina ukosefu mkubwa wa haki za binadamu na uonevu kwa wananchi.
Suala la kuwa na makosa ambayo eti hayana dhamana ni uonevu na unyanyasaji, hasa kwa namna kesi hizi zinavyoshughulikiwa hapa nchini. Kama mtuhumiwa amewekwa mahabusu kwa kosa ambalo serikali inaona halipaswi kuwa na dhamana, basi uwepo utaratibu kwamba kesi za namna hiyo zimalizwe ndani ya miezi miwili, yaani siku 60.
Huwezi kumkamata mtu kwa kosa ambalo halina dhamana, halafu polisi wadai kwamba upelelezi bado unaendelea, na huyo mtuhumiwa akae ndani hadi wengine miaka mitano, halafu mahakama ije iseme hana hatia, halafu tuone ni sawa mtuhumiwa aachiwe akaendelee na maisha yake. Huo ni ukosefu mkubwa wa haki.
Kama polisi hawajakamilisha upelelezi basi hawapaswi kuwakamata watu au kuwashikilia mahabusu.
Angalia kwa mfano huyu Nsiande Mwanga aliyekuwa akikabilia na kesi ya ufisadi TFF. Amekaa mahabusu tangu Julai 2017, na leo December 2019 Mahakama inaamua kwamba hana hatia aachiwe. Je, kweli kweli hii ni sawa katika haki za binadamu? Mtu anawekwa ndani muda wote huu wakati hana hatia na tunaona ni sawa? Je, polisi watamlipa fidia kwa kumweka ndani muda wote huu bila kuwa na kosa?
Ndiyo maana nchi kama Afrika Kusini hata kosa la mauaji lina dhamana, kwa kuwa waliona kumweka mtu ndani muda mrefu wakati upepelezi haujakamilika si sawa.