Hivi serikali inawezaje kuona ni sawa mtu kukaa mahabusu tangu Juni 2017 hadi Desemba 2019 na kuachiwa huru na Mahakama kuwa hana hatia?

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,023
18,563
Watu wanasema suala la haki ya dhamana ni suala la katiba, hapana, mie napinga kwa nguvu zote kwamba hili ni suala serikali inapaswa kulishughulikia mara moja kwa sababu lina ukosefu mkubwa wa haki za binadamu na uonevu kwa wananchi.

Suala la kuwa na makosa ambayo eti hayana dhamana ni uonevu na unyanyasaji, hasa kwa namna kesi hizi zinavyoshughulikiwa hapa nchini. Kama mtuhumiwa amewekwa mahabusu kwa kosa ambalo serikali inaona halipaswi kuwa na dhamana, basi uwepo utaratibu kwamba kesi za namna hiyo zimalizwe ndani ya miezi miwili, yaani siku 60.

Huwezi kumkamata mtu kwa kosa ambalo halina dhamana, halafu polisi wadai kwamba upelelezi bado unaendelea, na huyo mtuhumiwa akae ndani hadi wengine miaka mitano, halafu mahakama ije iseme hana hatia, halafu tuone ni sawa mtuhumiwa aachiwe akaendelee na maisha yake. Huo ni ukosefu mkubwa wa haki.

Kama polisi hawajakamilisha upelelezi basi hawapaswi kuwakamata watu au kuwashikilia mahabusu.

Angalia kwa mfano huyu Nsiande Mwanga aliyekuwa akikabilia na kesi ya ufisadi TFF. Amekaa mahabusu tangu Julai 2017, na leo December 2019 Mahakama inaamua kwamba hana hatia aachiwe. Je, kweli kweli hii ni sawa katika haki za binadamu? Mtu anawekwa ndani muda wote huu wakati hana hatia na tunaona ni sawa? Je, polisi watamlipa fidia kwa kumweka ndani muda wote huu bila kuwa na kosa?

Ndiyo maana nchi kama Afrika Kusini hata kosa la mauaji lina dhamana, kwa kuwa waliona kumweka mtu ndani muda mrefu wakati upepelezi haujakamilika si sawa.
 
😄hii nchi inaendeshwa kipekee Sanaa😂😂😂
TANZANIA NAKUPENDA KWA MOYO WOTEEE...🎶🚶🏿🚶🏿🚶🏿
Lakini labda wenye tatizo ni sisi raia. Tunapaswa kuja juu. Pia wapo wanasheria ambao wanaweza kufungua kesi kupinga hili kuwa linapingana na baadhi ya viengere vya katiba yetu
 
Watu wanasema suala la haki ya dhamana ni suala la katiba, hapana, mie napinga kwa nguvu zote kwamba hili ni suala serikali inapaswa kulishughulikia mara moja kwa sababu lina ukosefu mkubwa wa haki za binadamu na uonevu kwa wananchi.

Suala la kuwa na makosa ambayo eti hayana dhamana ni uonevu na unyanyasaji, hasa kwa namna kesi hizi zinavyoshughulikiwa hapa nchini. Kama mtuhumiwa amewekwa mahabusu kwa kosa ambalo serikali inaona halipaswi kuwa na dhamana, basi uwepo utaratibu kwamba kesi za namna hiyo zimalizwe ndani ya miezi miwili, yaani siku 60.

Huwezi kumkamata mtu kwa kosa ambalo halina dhamana, halafu polisi wadai kwamba upelelezi bado unaendelea, na huyo mtuhumiwa akae ndani hadi wengine miaka mitano, halafu mahakama ije iseme hana hatia, halafu tuone ni sawa mtuhumiwa aachiwe akaendelee na maisha yake. Huo ni ukosefu mkubwa wa haki.

Kama polisi hawajakamilisha upelelezi basi hawapaswi kuwakamata watu au kuwashikilia mahabusu.

Angalia kwa mfano huyu Nsiande Mwanga aliyekuwa akikabilia na kesi ya ufisadi TFF. Amekaa mahabusu tangu Julai 2017, na leo December 2019 Mahakama inaamua kwamba hana hatia aachiwe. Je, kweli kweli hii ni sawa katika haki za binadamu? Mtu anawekwa ndani muda wote huu wakati hana hatia na tunaona ni sawa? Je, polisi watamlipa fidia kwa kumweka ndani muda wote huu bila kuwa na kosa?

Ndiyo maana nchi kama Afrika Kusini hata kosa la mauaji lina dhamana, kwa kuwa waliona kumweka mtu ndani muda mrefu wakati upepelezi haujakamilika si sawa.
Nakubaliana na ww asilimia 100 South Africa umeenda mbali Kenya makosa yote yana dhamana likiwemo la mauaji......
ni vile tu watu wanapotezea hawaishitaki serekali kwa kuwaweka ndani watu muda mrefu mwishoni mwa siku inaonekana hawana hatia......
kuna haja ya sheria kubadilishwa kwa kweli....
 
Kuna mzee alikuwa anasimulia Clouds FM kipindi cha njia panda. Yeye alisingiziwa kuwa amehusika na mahuaji walikuwa kama watatu na yeye na kipindi hicho jamaa alikuwa Dar akifanya biashara ya Bar. Akawekwa jela miaka 2 hiv huku upelelezi unaendelea, kesi ikaunguruma ikawa inapigwa tarehe uchunguzi bado. Wakakamatwa wahusika waliohusika na mauaji wakajumuisha lakini hawa wahusika wakasema hawa hawahusiki sisi ndiyo tunahusika mahakama haikuwalewa sijui walitaka rushwa. Wakahukumiwa kunyongwa mpaka kufa lakini hawa watatu waka appeal. Kesi ikasikilizwa na hawakukutwa na hatia. Wakaachwa huru hapo mzee ametumikia miaka kama 20 hivi. Nilisikitika sana.
Unamfunga mtu miaka 20 hivi halafu unakuja kusema hana hatia, huko ni kuharibiana maisha maana maisha ni umri. Haya mambo naona yawe na faini yaani fidia. Wakikufunga halafu ukakutwa hauna hatia basi inabidi serikali pamoja na mshitaki wakulipe kuanzia milioni 10 yaani mwaka 1 ni milioni 10. Huko ni kupotezeana muda.
 
Kungekua na demokrasia wabunge wa upinzani wangelisema bungeni na sheria ikatungwa. Kwa usawa huu. Tuombe Mungu yasitukute
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom