Wadau wataka uwajibikaji kwenye uamuzi ambao umekuwa ukitolewa na Mahakama kwenye masuala mbalimbali

Nyakijooga

Senior Member
Dec 9, 2018
123
202
Asasi za Kiraia zaidi ya 15 zimetoa wito kwa Serikali kupitia Mwanasheria Mkuu wa Serikali kutaka uwajibikaji katika masuala ambayo tayari yameamuriwa kisheria au ambayo yapo kwenye Mahakama mbalimbali ambayo Serikali inatakiwa kuwajibika kuyatekeleza kulingana na maelekezo.

"Tunatoa wito wa jumla kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kutekeleza maamuzi
mbalimbali ya Mahakama kisheria. Mfano maamuzi ya Mahakama za ndani, za Kikanda na Kimataifa. Maamuzi hayo ni kama ya kesi ya Rebecca Gyumi, Maria Mushi, Mjomba Mjomba, Kesi ya THRDC, LHRC na MCT iliyoamuliwa na Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki Mwaka 2019, THRDC na LHRC iliyoamuliwa na Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, kesi za Mch. Mtikila, kesi ya Jebra Kambole na kesi ya Bob Wangwe ya Wakurugenzi wa Uchaguzi "limeeleza tamko hilo."

Hayo yameelezwa Mkuu wa Dawati la Utetezi la Mtandao wa Watetezi wa Haki za binadamu Tanzania (THRDC), Wakili Paul Kisabo alipokuwa akisoma tamko la pamoja la wadau kulaani baadhi ya matukio yanayodaiwa kughubikwa na ukiukwaji wa sheria hususani yanayodaiwa kuwakumba wafugaji walioko kando na hifadhi kwenye maeneo tofauti nchini.

Tamko hilo kupitia Wakili Kisabo anaeleza kuwa kuna baadhi ya mambo ambayo tayari Mahakama imeyatolea uamuzi wa kisheria lakini mpaka sasa uamuzi huo haunekani kuzingatiwa, ambapo ametaja baadhi ya kesi mbalimbali ambazo mamlaka zinatakiwa kuwajibika.

"Tunatoa wito wa jumla kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kutekeleza maamuzi
mbalimbali ya Mahakama kisheria. Mfano maamuzi ya Mahakama za ndani, za Kikanda na Kimataifa. Maamuzi hayo ni kama ya kesi ya Rebecca Gyumi, Maria Mushi, Mjomba Mjomba, Kesi ya THRDC, LHRC na MCT iliyoamuliwa na Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki Mwaka 2019, THRDC na LHRC iliyoamuliwa na Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, kesi za Mch. Mtikila, kesi ya Jebra Kambole na kesi ya Bob Wangwe ya Wakurugenzi wa Uchaguzi "limeeleza tamko hilo.

Ikumbukwe katika uamuzi wa baadhi ya kesi za hivi karibuni, hususani kesi ya Bob Wangwe ambaye ni Mkurugenzi wa Jukwaa la Katiba (JUKATA), kesi hiyo ilikuwa ikipinga vifungu vya sheria vinavyoruhusu Wakurugenzi kwenye Halmashauri kusimamia uchaguzi, ambapo

Katika uamuzi shauri hilo June 2023 Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu iliagiza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufanya marekebisho ya sheria ya Taifa ya uchaguzi inayotoa uhalali kwa Wakurugenzi (DED) kusimamia uchaguzi.

Mlalamikaji alidai kuwa wakurugenzi hao ni 'makada wa Chama Cha Mapinduzi' ambacho ni chama tawala hivyo alidai kuwa ni vigumu uchaguzi kuwa wa huru na wa haki, lakini pia inadaiwa kuwa vifungu hivyo vinakiuka haki ya usawa mbele ya sheria ikiwa ni pamoja na haki ya wananchi kuchagua viongozi wao wanaowataka kwa uhuru.

Katika shauri la Wakili Jebra Kambole Mahakama ilitoa uamuzi kutaka makosa yote kuwa na dhamana, ambapo mleta maombi alidai kuwa sheria zinayagawa makosa kwamba kuna makosa yenye dhamana na yasiyo na dhamana.

Aidha katika tamko hilo wamesema kuwa yapo baadhi ya maeneo ambayo yanawazunguka wafugaji ambayo tayari Mahakama imeweka zuio na sehemu nyingine kesi zinaendelea, lakini amedai licha ya hivyo uzingatiaji wa maagizo ya Mahakama bado haujaonekana.

Amesema "Mnamo tarehe 19.09.2022, Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Arusha ilitoa uamuzi juu ya Tangazo la Waziri wa Mali Asili na Utalii Na. 421 la Mwaka 2022 ambapo pamoja na mambo mengine Mahakama ilitamka kuwa Tangazo la Waziri halikufuata utaratibu wa Kisheria hasa kuwashirikisha wananchi wakazi wa vijiji hivyo, Kata, Halmashauri ya Wilaya pamoja na wahanga wa Tangazo hilo.

Ameongeza kuwa "Katika uamuzi huo, Mahakama ilisisitiza kwamba:(a) Pori Tengefu la Pololeti lenye kilometa za mraba 1,502 halikutangazwa kwa kufuata Sheria na lilikufa mara baada ya Rais kutangaza kuwa eneo hilo ni Pori la Akiba kupitia Tangazo la Serikali Na. 604 la mwaka 2022 na hivyo kwa sasa hakuna kitu chochote kiitwacho Pori Tengefu la Pololeti(b) Utekelezaji wa Tangazo lililotolewa na Rais Na. 604 la Mwaka 2022 usimame kuanzia tarehe 22.08.2023 hadi kesi ya msingi itakapoisha kwa kutolewa uamuzi na Mahakama."tamko hilo limeeleza

Kufuatilia suala tamko hilo limeeleza “Tunatoa wito kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwaelekeza watumishi wa Serikali hasa katika maeneo lalamikiwa kuheshimu maamuzi na amri za mahakama kwani zinapaswa kuheshimiwa na kila mtu,”

Baadhi ya Asasi hizo ni pamoja na kituo cha Sheria na Haki za binadamu (LHRC), JUKATA na Pan African Lawyers Union (PALU).
 
Back
Top Bottom