Kwa Hiyo Serikali /DCI na Mahakama, mmeamua kuwaambia Watanzania kuwa Dada wa Msuya alijichinja mwenyewe?

Carlos The Jackal

JF-Expert Member
Feb 6, 2017
24,052
71,325
Mnajua Mfike Mahali Mumuogope Mungu, hii ni Roho ya mtu asokuwa na hatia, ilopotewa, Kwa Kuchinjwa , Tena Kuchinjwa na kutenganishwa Kichwa na Kiwiliwili.

Maumivu aloyapata marehem, wakati Chombo chenye ncha Kali kikipita Shingoni mwake , pengine akirusha miguu na mikono, Chombo che ncha kali kikipenyeza kwenye Kooo, mishipa ya Damu, Damu ikirukaaa, Kikapenya kwenye Mishipa ya faham, nahatimaye Kikapenya katikati ya maungio ya shingo, Ni wazi Dada wa Msuya alikufa Kifo chenye maumivu makubwa sana.

Kifo kilichokusudiwa, Kifo ambacho Ndani yake ,Muuaji alijawa hasira, Chuki na Roho ya kisasi ilokusudia "Nitakuonyesha", ..Na Kwa sababu hiyo, Muuaji alichagua Kuua Kwa KUCHINJA , tuseme kwamba aliuwawa akiwa tayari kasinzilishwa Kwa dawa za usingizi, yote Kwa yote, aliuwawa Kwa KUCHINJA.

Maajabu ,Leo katika Nchi ya Hasira, Nchi ambayo MaJAJI ni Matajiri wa kupindukia, Nchi ambayo hata askari anayelinda nyumba ya Jaji na wasaidizi wa Jaji ni matajiriii...

Nchi ambayo Polisi imejaa Darasa la Saba, Na Walofeli Kidato Cha Nne ndio wanaofanya Forensic investigation, Nchi ambayo alofeli Kidato Cha Nne, ndio anapewa kazi ya upepelezi.

Nchi ambayo, Wakili mwenye Uwezo mzuri, alofaulu kujua Ombwe la Sheria zetu, naaam kwakua kwake ni Kutetea mteja na Pesa, anaamua kutumia Elimu yake na uelewa wake, kumtetea mteja wake, na kweli Mteja kaachiwa huru.

Ni nani alimuua dada wa msuya? Tuambiane basi kama alijichinja tujueee.

Mdada wa kazi? Mdada wa kazi ndio muuaji? Kwamba alimshinda nguvu dada wa msuya??.

Katika uumbaji wa mwanamke, hana gut ya kuua kwa kuchinja, hawezi na haitokaa itokee.

Kama alotekeleza mauaji hayo ni mwanaume, aliyafanya kwa lengo gani ,afaidike na nini?.

Haya bana, niwashukuru kwa kuendelea kutenda haki. Hivi kama jeshi halikua na uwezo wa kipelelezi, simngeomba msaada nje?

Kwanini maisha ya watu ni mnachezea kamari namna hii?
 
Ukiskia MMACHAME kimbiaaaaa.
Wanawake wa Aina hii ndio wanafanya vijana wanakataa Ndoa!
Ndoa ni Kifo.
Ndoa ni Jela.
Ndoa ni gereza.
Ndoa ni Utapeli.
Lkn zingatia ili uwe mwanaume timilifu lazima Uoe, kikubwa ishi nao kwa akili.
aione Uffwoo Swarro na wafuasi wake.
 
Hivi sababu hasa ya Mke wa Msuya kuhusishwa na kifo cha Wifi yake ni ipi ? na kwamba kama angemuua wifi angepata nini zaidi ya mali ambazo alikuwa nazo za bilionea Msuya?

Na kwamba uwepo hai wa huyu wifi ungezuia kitu gani kwa mke wa Msuya kupoteza mali za mumewe na huku ni mke halali?

Hapa nahitaji kueleweshwa .
 
Hivi sababu hasa ya Mke wa Msuya kuhusishwa na kifo cha Wifi yake ni ipi ? na kwamba kama angemuua wifi angepata nini zaidi ya mali ambazo alikuwa nazo za bilionea Msuya ? na kwamba uwepo hai wa huyu wifi ungezuia kitu gani kwa mke wa Msuya kupoteza mali za mumewe na huku ni mke halali ?

Hapa nahitaji kueleweshwa .
Kuna siri kubwa sana tangu kifo cha Bilionea msuya hadi dada yake.

Kuna hati ya Kiwanja kilicho Arusha kilikuwa cha Bilionea msuya, ila hati ya Kiwanja hicho marehemu Bilionea msuya alikuwa ameiweka Kwa dada yake Aneth Msuya.

Baada ya kifo cha Bilionea msuya, mke akataka kukiuza hicho Kiwanja , akashindwa Kwa sababu hati Iko Kwa Aneth Msuya, Dar, issue ikawa Aneth Msuya afanyiwe aliyofanyiwa ili hati ipatikane na Kiwanja kiondoke .

Wiki ijayo nitakusimulia zaidi ila Kwa Sasa simamia hapa
 
Wauaji wa Kaka wote wako nje
Wauaji wa Dada wote wako nje

Mahakamani kuna kazi kweli kweli
Wenyewe wanataka "proof beyond reasonable doubt"..

Kwa mfumo wa mahakama haujali hisia wala utashi wa kawaida. Unahitaji logic, uelewa wa sheria na jinsi ya kucheza nao

Hapa ndo maskini na watu wasio na uwezo hupoteza haki zao maana mwenye kuijua sheria, nguvu ya kupata mwanasheria mzuri na pesa ya kufanya lobbying, lazma apenye hata akifanya kosa
 
Ni kweli marehemu alichinjwa. Swali linabaki je ni nani alimchinja?
Vyombo vyenye dhamana vituambie.

Itakuwa ajabu kubwa iwapo hawatefanya uchunguzi kubaini muuaji na kumfikisha mahakamani.

Kifo cha kuchinjwa ni cha kuuliwa sio cha kujiua mtu mwenyewe.

Jamii inahitaji kujua Jamhuri itafute wauaji.

Kwa polisi hilo ni jambo la kawaida kuchunguza na kubaini watuhumiwa na kuwafikisha mahakani
 
Aisee.Haya mambo yanauma sana.Kama ni kweli huyu mama alitenda basi Mahakamani ni ujanja ujanja tu hakuna haki. Pesa ilimuua Yuda na alimsariti Yesu- immagine usikute wakina Kibatala wanajua ukweli kabisa lkn wanatafuta loop holes za kumuokoa mtu.

Hivi uchawi na uganga au majini huwa yapo kweli??
 
Back
Top Bottom