Ulinzi wa rais upo so complicated na unahitaji utulivu kuutambua, Kwanza ili uwe kwenye 'convoy' ya ulinzi wa rais lazima uwe TISS na upite kwenye vile vyuo vyao ukaive. TISS kama majeshi mengine yana department na sections nyingi kuna
1) kurugenzi ya Mambo ya nje
2)mambo ya ndani, kuna 'deep covers' kuna 'undercover' kuna wengine wanakua recruited kama 'informers' na pia kuna VIP protection unit ambao ndani kuna PSU (presidential security unity) hawa wapo wengi kulingana na majukumu. Wapo wale wavaa suti, wavaa suti wabeba mabegi, wenye sare za mabaka mabaka, sare kama FFU, sare kama polis wa kawaida nk. Wote hawa wanapatikana kwa njia mbali mbali inaweza kua direct recruited from mtaani baadaye unaenda mafunzoni, inaweza kua jeshini,polisi,magereza,nk
Ulinzi mkubwa wa rais hauonekani kwa macho, maana hujichanganya kama raia wa kawaida hivyo kumtambua ni ngumu kwa sie watu wa kawaida.
Kwa kumalizia tu niwakumbushe vijana wanaopenda kazi hizo kua ni NGUMU na zina kiapo kikali sana pengine kuliko viapo vyote. Wanajua mengi na Wana jukumu la kulinda ustawahi wa nchi. Hakuna sehemu utaona vyombo vya habari vinawamulika, hakuna siku utaona wanapandishwa cheo hadharani kama ilivyo jeshini magereza na polisi. Ni ukimya ni siri.
Sent using
Jamii Forums mobile app