Hivi Rais analindwa na vikosi vingapi vya askari?

blackhawk

Member
Feb 9, 2020
36
125
Bonjour wana JF,

Sijui kuna mtu ameshawahi kua na swali kama langu ila akakosa majibu ya kitaalamu.

Kila nikiangalia ziara za Rais JPM huwa naona walinzi mwenye sare tofauti tofauti nikapata wazo la kufuatilia layers za walinzi wale ila sijui kazi za kila mmoja naomba nipate kujuzwa za mimi nielewe leo.

1. Kwanza kuna yule amevaa sare ya JWTZ huwa yupo na Rais bega kwa bega na hata gari huwa wanakaa moja huwa ni nani na kazi zake exactly ni zipi?

2. Kuna hawa wanavaaga SUTI huwa wanana silaha zinazoonekana sijui kama wana silaha ila huwa wamevaa vifaa vya mawasiliano katika sikio moja na wapo hadi wanawake hawa ni kina nani na wajibu wao ni upi?

3. Kuna hawa wengine wana silaha kubwa sana sijawahi ona silaha ya vile uniforms zao zina mabaka madogo madogo rangi yake kama uniform za US Army tunazoonaga kwenye movies huwa wamejaa sana weusi tii na wanaogopesha.

4. Kuna hawa wengine wamevaa uniforms za kama polisi FFU ila kofia zao ni ngumu nyeusi sio nyekundu kama zilivyo za FFU na zina mifumo ya mawasiliano direct, huwa wana machine Guns za kisasa hatari kama tunazoonaga kwenye movie nyingi za Hollywood kufuani huwa wamevalia Bullet proof vest nyeusi ikiwa na gears nyingi sana kama kamba, mabomu ya mkono, visu, Vidude vya risasi vile na vitu vingine hata sielewi ni vitu gani, vest zao kwa nyuma zimeandikwa SWAT sijui maana yake ila huwa naonaga kwenye movie pia hilo neno kwa askari wa vikosi maalum. Hawa kazi yao ni nini?

5. Wa mwisho ni hawa askari wa kawaida tunakimbizana nao kila siku mtaani wanavaa kofia nyekundu kichwani FFU na hawa wengine wanaovaa kofia za kawaida pamoja na Traffic hawa najua wajibu wao ni nini.

Kwa yeyote mwenye uelewa mzuri wa layers za kijeshi naomba kupata elimu.

Nawasiliaha

UH-60 Black Hawk

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
8,493
2,000
1. Kwanza Kuna yule amevaa Sare ya JWTZ = Mpambe wa Raisi, kawaida kutoka JWTZ

2. Kuna hawa wanavaaga SUTI huwa hawana silaha zinazoonekana = TISS kikosi cha ulinzi wa Raisi (bodyguards)

3. Kuna hawa wengine wana silaha kubwa sana sijawahi ona silaha ya vile uniforms zao zina mabaka madogo madogo = with love from Rwanda

4. Kuna hawa wengine wamevaa uniforms za kama polisi FFU = Polisi kikosi cha ulinzi wa Raisi na kudhibiti umati

5 Wa mwisho ni hawa askari wa kawaida tunakimbizana nao kila siku mtaani wanavaa kofia nyekundu kichwani = FFU Kikosi cha ulinzi wa Raisi na kudhibiti umati
 
Mdaiwa-Sugu

Senior Member
Mar 8, 2020
149
250
Nakujibu kama ifuatavyo.

Anayevalia sare ya JWTZ ni mpambe wake kazi yake ni kumsaidia Rais kazi ndogo ndogo kama kumbebea begi, simu n.k mara nyingi utamwona akiwa nyuma ya Rais.

Wanaovalia suti ni watu wa usalama, kazi yao kubwa ni kuhakikisha Rais anakuwa salama muda wote.

Wenye silaha kubwa wanaovalia combat kama za US Army ni walinzi, kazi yao kubwa ni kuhakikisha ulinzi kwenye eneo la tukio

Askari wa FFU kazi yao kubwa ni kutuliza ghasia na Askari wanaovalia kawaida kazi yao ni kukamata waleta fujo na ghasia

Nadhani mpaka hapo nimekujibu.
 
MTAZAMO

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
15,619
2,000
TISS wana vitengo vingi kama Polisi, wale wenye sare za mabaka madogo ni moja ya vitengo maalum ndani ya TISS na pia wale wenye sare za FFU ni moja ya vitengo maalum ndani ya FFU.

Wote wamepitia mafunzo maalum ya kikomandoo na mambo ya ulinzi kwa viongozi maalum V.I.P. Ukikutana na FFU kitengo maalum hata bila kuambiwa utajua si askari wa kawaida na hawa hawatumiki kwenye operations za kutuliza ghasia n.k labda matukio yaliyoshindikana.

Baadhi ya maelezo yalitolewa kwenye sherehe za uhuru kama sikosei zilizofanyika dodoma. Issue ya askari kutoka Rwanda ni uzushi a.k.a matango pori.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukwaju

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
11,337
2,000
1. Kwanza Kuna yule amevaa Sare ya JWTZ = Mpambe wa Raisi, kawaida kutoka JWTZ
2. Kuna hawa wanavaaga SUTI huwa hawana silaha zinazoonekana = TISS kikosi cha ulinzi wa Raisi (bodyguards)
3. Kuna hawa wengine wana silaha kubwa sana sijawahi ona silaha ya vile uniforms zao zina mabaka madogo madogo = with love from Rwanda
4. Kuna hawa wengine wamevaa uniforms za kama polisi FFU = Polisi kikosi cha ulinzi wa Raisi na kudhibiti umati
5 Wa mwisho ni hawa askari wa kawaida tunakimbizana nao kila siku mtaani wanavaa kofia nyekundu kichwani = FFU Kikosi cha ulinzi wa Raisi na kudhibiti umati
kuna mahali tumebishana kidogo kutoana meno, waking'ang'ania ni TISS
nikawaambia kuna wenye mabaka sio wa kwetu wala Mambo ya ndani

Kutoka kuwa Mkurugenzi wa TISS na kuwa IGP hii imekaaje?
 
Ukwaju

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
11,337
2,000
TISS wana vitengo vingi kama Polisi, wale wenye sare za mabaka madogo ni moja ya vitengo maalum ndani ya TISS na pia wale wenye sare za FFU ni moja ya vitengo maalum ndani ya FFU.
Wote wamepitia mafunzo maalum ya kikomandoo na mambo ya ulinzi kwa viongozi maalum V.I.P. Ukikutana na FFU kitengo maalum hata bila kuambiwa utajua si askari wa kawaida na hawa hawatumiki kwenye operations za kutuliza ghasia n.k labda matukio yaliyoshindikana.
Baadhi ya maelezo yalitolewa kwenye sherehe za uhuru kama sikosei zilizofanyika dodoma. Issue ya askari kutoka Rwanda ni uzushi a.k.a matango pori.
Sent using Jamii Forums mobile app
sio Matango pori ni ukweli mtupu, imeshajadiliwa na hata MTAZAMO ulishaiweka hapa Ulinzi wa Rais Magufuli ni wa hali ya juu
Bungeni kuna askari wa Bunge na FFU wa Bunge lakini wanaripoti kwa DCO na hawakubali kutoka hapo Bungeni mpaka waraka, Wapo Traffic wanaoongozana na misafara huwezi kwenda mpangia lindo ashike silaha, kuna FFU wa msafara huwezi wapangia Benki au Mpirani
kwa hiyo ni sawa na Askari akipelekwa kitengo cha ulinzi Magogoni huwezi mpeleka akafanye kazi za ambush za mitaani mikoani au kumfuatilia mhalifu ndio maana unakuta ni walewale wanaoonekana kwa Waziri Mkuu aliyepo au wale wastaafu au Rais mstaafu au Rais aliyepo. namaanisha km umetoka JW utakuwa JW umeazimwa TISS kitengo cha ulinzi, Fuatilia kideo ya leo Ubungo hao walinzi wenyewe kwa wenyewe wanapishana wakiwa kazini
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom