Ngoja nami nichangie machache
1,huyo mwanajeshi ambae muda wote unamuona na raisi anaitwa ADC Aide de camp,kazi yake kubwa ni kuhakikisha anamsaidia raisi kwenye shughuli zote,kama kumbebea simu na baadhi ya vitu vyake na kingine kikubwa yeye ndo mtu wa kwanza kuwa responsible pale inapotokea ambush ya haraka na yeye ndo huhusika haraka kwenye kumtorosha raisi au kumkinga na lolote mfano pale bush alipo rushiwa kiatu basi angekuwa rais wetu basi yule ADC angekidaka na kumuondoa chap mkuu eneo la tukio.
2.namba mbili ni hao wavaa suti,hao ni kikosi cha raisi ambao kazi yao kubwa ni kuhakikisha usalama wa raisi katika nyinja mbali mbali hasa kuhakikisha kuna radius(duara)ambalo watalitengeneza kuhakikisha kuwa hakuna adui anaingia ndani ya meter hizo,hvyo chunguza raisi kila atembeapo huwa kuna duara linatengenezwa na hwa jamaa kuhakikisha kuwa adui hasogei karbu na raisi na kila wanapopiga hatua ndio hapo hapo raisi nae atakanyaga.
Hawa jamaa hubeba silaha aina ya pistol ndogo kiunoni but kama utakuwa makini kila raisi akiwa ameshuka kwenye gari anatembea huwa kuna magari yanatembea yakiwa karibu nae mno,likiwemo gari lake basi yale magari mengne huwa ni maalum yamebeba silaha nzito incase limetokea tatizo basi ni kitendo cha dakika tu wanaume walishazibeba na kukinukisha.
3.Hao wanaovaa nguo za mabaka mabaka na silaha nzito hao wanaitwa energence response team hao kazi yao ni ku act haraka na kupambana na adui as soon ameact au kuonyesha dalili za kutaka ku attact na ndio wakwanza kumzunguka rais na viongozi ndani ya tukio(kumcover) wakati huo wale wengine wasuti wanachukua silaha kwenye magari ili kuunganisha nguvu,then kumtoa mkuu eneo la tukia as soon as possible huku msala mkibaki nao na hawa wa mabaka mabaka
4,ni hao unao waona kama field force hicho ni presidential force ambayo inahusika na kuweka mazingira sawa,wakati raisi akiwa bado hajafika eneo la tukio na wangine wanakuja nae,kazi yao ni kutengeneza njia ya raisi kupita na kuzuia mtu yoyote au chochote kisiwe karibu na raisi kwa umbali wa meter 10.nao pia wana act ina case kumetokea tatizo na wako vizuri sana kwenye combat kwa maana ukitaka kumkarbia raisi alafu wakakuonya ukajifanya mbishi utachezea ngumi ndani ya sekunde na watu wasijue but watashangaa tu pua znatoka dam
Pia kuna hao trafiki ambao unawaona hapo kwenye msafara,hao k
Ote ni usalama wa taifa wanakuwa wanakink moja kwa moja na kitengo,na kabla mheshimiwa hajapita eneo la tukio ni lazima lipite gari au piki piki ya ikulu kwanza kuangalia njia na waongozaji kama ndo wenyewe au kuna tofauti then ndo anatoa permission kwa msafara kusogea ikiwa other wise msafara unaweza kugeuza hata hapo hapo.
Pia mwisho tambua kuwa raisi si mtu bali raisi ni taasisi inayojitegemea na ya kipekee kushinda zote, hivyo usishangae umaambiwa kuwa kuna magufuli watatu (doubles)
I hope nmejibu tunachotakiwa kujua mengine yaache yawe classified
Sent using
Jamii Forums mobile app