MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 20,897
- 63,784
Leo nimewaza sana,
Nakumbuka miaka ya zamani tunakua, kulikuwa na ukaribu mkubwa sana baina ya watu. Ilikuwa inafika kipindi watu wa mtaa mzima tulikuwa tunafahamiana vizuri kabisa hata kutembeleana. Hili lilikuwepo kuanzia mitaa ya uswahilini, hadi uzunguni.
Kuanzia shuleni, tulikuwa tunasoma na watoto wa wakubwa, na hata siku za sherehe kama Brithday, Eid, Christmas, Easter, New-Year n.k tulikuwa tunakutana bila kuangalia mtoto wa nani ni nani. Lakini mbali na watoto, hata wazee walikuwa na ukaribu sana. Unaweza kumuona mtu kwenye taarifa ya habari, lakini siku za mwisho wa wiki unakuta kaja kwenu kusalimiana na wazazi wako na wanaongea hata masaa.
Nakumbuka utoto wangu tulikuwa tukienda kwenye nyumba za wakubwa fulani hivi, weusi, wahindi, waarabu hata wazungu na kucheza na watoto wao bila kuzuizi chochote kile. Huu uhusiano haukuwa kamili (There were prejudices, here and there) lakini watu tuliweza kuvumiliana na kuchukuliana sana. Tumecheza mpira wote, tumeangalia televisheni wote, tumecheza michezo wote, tumejisomea wote n.k
Hili lilitusaidia kutengeneza ukaribu, urafiki na kufahamiana ambako kwa namna moja au nyingine kumekuwa na manufaa sana hadi leo hii. Tumesaidiana na kubebana kama ndugu kwenye shida na raha. Nadhani hili ndilo lengo kubwa la ujirani mwema.
Kinachonishangaza kidogo ni kwamba, leo hii ambako watu wengi wameelimika na kuwa na vipato vya kati ilitegemewa kwamba ndiyo tutakuwa na ukaribu na mahusiano mazuri. Lakini imefikia kipindi jirani wa nyumba moja hamfahamu hata mwingine, watu tunaogopana na kukwepana. Kila mtu anataka kuwa kivyake na watoto wake. Hata ndugu wa damu kila mtu anakufa kivyake. NO FAMILY REUNIONS, NO FIDELITY, NO FRATERNITY.
Mtoto anatoka International School tokea asubuhi mpaka jioni, akifika nyumbani anapewa Ipad, Video Game, Laptop au TV imeunganishwa na Netflix tayari anakaa peke yake hadi kesho tena. Huu ndiyo unakuwa mfumo wake wa maisha 24/7/365. Kibaya zaidi watoto wetu siku hizi hata KISWAHILI hawajui vizuri kabisa lakini wazazi hatustuki kabisa.
Wazazi tunafurahia (We are very proud) maisha ambayo watoto wetu wanaishi, tunaona haya ndiyo mafanikio yenyewe kwasababu wengi hatukuishi haya maisha. Wengi wetu tuliishi maisha ya kidumu, jembe, ufagio, viboko na kufanya kazi za nyumbani, hivyo tunahisi yale maisha hayakuwa mazuri. Kanuni nzima ya adhabu na nidhamu kwa mtoto limekuwa jambo la kishamba kabisa(Antiquated Medieval Madness). Mtu anayewaza kutoa adhabu ni mshezi tu.
HAPA NAWAZA TU, NAWEZA NISIWE NIKO SAHIHI.
Mwisho kabisa, watoto wetu wanasoma mitaala ya GCSE, moja ya mitaala mizuri kabisa ambayo inawawezesha kuwa na vyeti vizuri mbavyo huwapa nafasi nzuri kwenye soko la ajira. Lakini nimeangalia kwa macho yangu kama mzazi na kufahamu kwamba mbali na watoto kufahamu mambo mengi sana (General Knowledge), Ufahamu na Uelewa sahihi(Proper Understanding & Comprehension) kuhusu mazingira yao wanakuwa hawana. THEY'RE SIMPLY DETACHED FROM REALITY.....
Nawaza sana hiki kizazi tunachokitengeneza kitakuwaje huko mbele na sipati majibu. Aidha ni woga wangu tu, AU uelewa wangu mdogo, AU bado naishi siku za kale bila kukubali kwamba dunia imebaridika (Nostalgic and Trapped in the past). Lakini yote tisa, kizazi hichi cha kisasa ni cha kisasa haswaaaaa.