Mwanamke hakuumbiwa majukumu, ni Shida tu.....

Mwizukulu mgikuru

JF-Expert Member
Oct 21, 2021
4,830
11,310
Mwanamke ameumbwa kuhudumiwa tu,

Mwanamke ili atafutiwe na apewe atumie na ikitokea Mwanamke akatafuta na watu wakatumia basi watu hao hivyo vitu vitawatokea puani kwa masimango au kashfa yoyote watakayopewa.

Mfano huu hapa baba yangu wakati anamuoa mama yangu wa pili (mama wa kambo) alikuwa vizuri Sana kiuchumi, familia yetu sisi ilikuwa katika uchumi wa kipato cha kati.. Uchumi wa mzee uliporomoka hasa kipindi cha Magufuri na kufirisika kabisa na akawa ni Mtu wa kujifungia ndani.

Kipindi hicho Huyu Mama yangu wa pili alikuwa akijishughulisha na biashara ndogo ndogo kama kuuza ice cream na nyinginezo ambazo kwa kiasi chake alikuwa na akiba ambayo ilitumika kutatua matatizo matatizo madogo madogo mfano kulipia bili ya maji, umeme na kujazia Karo ya shule kwa wadogo zangu.

Lakini baada ya mzee kuyumba mama wa pili ilimbidi usukani kwa kusaidia kulisha familia na hapa ndipo tatizo likazaliwa.. Anachagua Nani ale chakula na Nani asile kwa sababu yeye ndie anaenunua chakula.

Hii imepelekea hata Mimi mwenyewe nikitaka kwenda kumtembelea mzee inatakiwa niende na kiasi kikubwa cha pesa kitakachoniwezesha kununua chakula na mahitaji mengine kwa siku zote nitakazokuwa kwa mzee Vinginevyo nitaambulia masimango mpaka kieleweke (mama yangu Huyu wa pili kabila lake ni mrangi wa kinda😁).

Hawa watu ni Shida tu za dunia lakini kiukweli ni kuwa hawakuumbwa kutoa wameumbiwa kupokea tu..
 
Kwa case ya huyo baba ako, huoni kwamba huyo mama ako wa kambo kama angekuwa mama wa nyumbani ungekuta familia wamekufa kwa njaa.?
 
Unapitwa hadi na wanyama...Simba jike ndio linawinda vizuri..kuwatafutia wanae chakula simple ni hivi linapokuja suala la nyumba na familia mwanamke ana jukumu.

Mwanaumme anabaki na jukumu security na provisions ambayo kwa sasa ni pesa.
 
Nikisoma sifa ze mke mwema kwenye METHALI 31

Sijaona mahali Mungu anasema mke akae nyumbani kama kubwa jinga anamsubiri tu mumewe.

METHALI 31:16
16. Huangalia shamba, akalinunua; Kwa mapato ya mikono yake hupanda mizabibu.

METHALI 31:24
24. Hufanya nguo za kitani na kuziuza; Huwapa wafanya biashara mishipi.

METHALI 31:27
27. Huangalia sana njia za watu wa nyumbani mwake; Wala hali chakula cha uvivu.
 
Mwanamke ni msaidizi, unajua kazi ya msaidizi?

Unajua CEO huwa anafanya kazi chache sana kulingana na wasaidizi wake?

Siku zote msaidizi ana majukumu mengi kuliko kiongozi wake.

Hata dada(house helper) anafanya kazi nyingi kuliko bosi wake na huyo ni msaidizi tu.

Bottom line, let women work, let them earn income...tuliwasomesha binti zetu sio wakae nyumbani kusubiri kimeletwa au hakijaletwa. Let them work.
 
MWANAMKE HATAKIWI KUWA MPAMBANAJI, BASI TU MAISHA YA SASA INABIDI IWE HIVYO

Nasikia kwa waislamu ukioa mwanamke umuhudumie kila kitu, yeye akae ndani, kukuhudumia wewe na watoto.
 
Back
Top Bottom