Hivi ni majukumu au ubinafsi unaofanya watu wasiwe karibu kama zamani?

Wengi hawajui zamani O'bay nyumba nyingi hazikuwa na fence,unakatiza nyumba kwa nyumba mitaa mitatu....watoto,wazee wote wanafahamiana. Sasa hivi kuna maukuta kama gereza na watu wanaona sifa kutokufahamiana.
Daah, juzi niko Dar nikasema nifanye zoezi na kushangaa kidogo, nimefika Coco-Beach kuelekea Laibon Road nimekutana na masinagogi yana kuta za hatari. Kibaya zaidi ni kwamba hata Easement (Njia za kupita) hakuna, inabidi uvuke huu mtaa kuelekea wa pili ndiyo upate njia. Mtaa uko kimya vibaya mno, nikasema hata wenzetu wazungu hawafanyi hivi aiseee. Lakini hichi ndicho wanasema A NEW NORMAL,....
 
Zamani maisha yalikua mazuri watu walisocialize vzuri na mkijenga urafiki unakua ni urafiki hasa na wenye faida tofauti na sasa.

Pia siku za sherehe mtajumuika familia + marafiki wamama watapika tutakula na kuenjoy + stories kibao but nowdays sijui ndio utandawazi kukiwa na sherehe mtu atabebana na familia yake anaenda kuenjoy restaurant/hotelin basi imetoka.

I miss the good old days kwakweli.
Watu wengi hawajui tu, lakini hizi jumuiya zina manufaa sana sanaa. Hasa linapokuja suala zima la ajira, elimu na biashara. Kama umeshirikiana na kuishi vizuri na watu unakuwa kwenye nafasi nzuri zaidi kwenye maisha. YOUR NETWORK IS YOUR NET-WORTH, sema watu wengi hawajang'amua kabisa.

Siku hizi hata vijana au wamama wakija kuniambia kuna shughuli za mtaani, hata kuchangia timu ya mpira au mradi fulani. Mimi huwa najiweka tu bila hiyana, na mimi nifanye kitu. Nafahamu dhahiri siku za mbeleni hili litanisaidia tu,....
 
Nadhani dhana ya ujamaa ilikuwa namna nzuri sana ya kuishi,kila mtu aliishi kwa ajili ya mwingine bila kujali tofauti zetu katika kipato,elimu,imani,n.k. Kila kitu katika jamii ilikuwa mali ya wote pamoja na umasikini wetu.
Leo hii tumekuwa na vipato ahueni lakini tunajenga jamii iliyoparanganyika kwa kila namna.

Kwa mawazo yangu,zamani heshima ya mtu katika jamii ilikuwa ni kwa namna gani una wajibika kwenye jamii lakini siku hizi heshima inaletwa na unamiliki nini kwa mtizamo wa jamii husika,hivyo kila mtu ameegamia kujilimbikizia mali ili aipate ile hadhi ya kueshimika katika jamii.
 
Watu wengi hawajui tu, lakini hizi jumuiya zina manufaa sana sanaa. Hasa linapokuja suala zima la ajira, elimu na biashara. Kama umeshirikiana na kuishi vizuri na watu unakuwa kwenye nafasi nzuri zaidi kwenye maisha. YOUR NETWORK IS YOUR NET-WORTH, sema watu wengi hawajang'amua kabisa.

Siku hizi hata vijana au wamama wakija kuniambia kuna shughuli za mtaani, hata kuchangia timu ya mpira au mradi fulani. Mimi huwa najiweka tu bila hiyana, na mimi nifanye kitu. Nafahamu dhahiri siku za mbeleni hili litanisaidia tu,....
Mifumo ya maisha ya upweke ina madhara makubwa sana hasa kwa maisha ya mbeleni. Kuna mahala nilisoma haya maradhi ya msongo wa mawazo yanasababishwa kwa kiasi kikubwa na maisha ya kujitenga sana na jamii.

Siku hizi ukipata tatizo hakuna rafiki wa karibu kufarijiana ndio maana tunakimbilia kwenye pombe ili kujisahaulisha. Tofauti na rafiki,kwanza anakusikiliza unapata faraja halafu anakupatia ushauri.
Bahati mbaya haya maisha hayakwepeki tena,tushaingia ndani yake.
 
Kweli zinasaidia sana na ukishirikiana vzuri na watu unajijengea reputation nzuri ambayo itaweza saidia hata kizazi chako.
 
Mifumo ya maisha ya upweke ina madhara makubwa sana hasa kwa maisha ya mbeleni. Kuna mahala nilisoma haya maradhi ya msongo wa mawazo yanasababishwa kwa kiasi kikubwa na maisha ya kujitenga sana na jamii.

Siku hizi ukipata tatizo hakuna rafiki wa karibu kufarijiana ndio maana tunakimbilia kwenye pombe ili kujisahaulisha. Tofauti na rafiki,kwanza anakusikiliza unapata faraja halafu anakupatia ushauri.
Bahati mbaya haya maisha hayakwepeki tena,tushaingia ndani yake.
Daah hapo kwenye upweke ndio tatizo kubwa, kama baadhi ya taarifa za vifo unaskia mtu amekutwa kafariki nyumbani kwake mwili umekuja kugundulika baada ya week that means alizidiwa akakosa hata msaada wa watu wa karibu hadi anafariki
 
Kuna ndugu unaweza kumpigia simu kwa sababu ana ahueni ya kimaisha anawaza unataka kumuomba ela, hovyo kabisa hii dunia ya sasa.

Mimi sasa hivi nina ndugu ambao ni marafiki zangu nje ya undugu, pili vyama vyetu vya kihiyari vya misiba na sherehe ndio ndugu zangu, nje ya hapo sina habari na mtu.

Ukitokea msiba kwenye ukoo nitachanga mchango wangu, lakini binadamu wa sasa wana roho mbaya zaidi ya wanyama ndio sababu unaona watu wengi wameamuwa kujitenga wapo kivyao.

Mungu akikujalia kuna watu wawili watatu mnaelewana hao ndio ndugu zako.

Kingine watu wa leo wamemuhasi Mungu, hawana hofu na Mungu na wala hawamchi Mungu ndio sababu ya yote haya.

Nina jirani yangu hapa mwislamu kila sikukuu ya kuchinja lazima aniletee mguu wa mbuzi na ana imani sana na dini yake ndio alinifanya nielewe waislamu wa kweli wana upendo na wana hofu na Mungu.
 
Utandawazi... Ubinadamu kazi...

Watu wamejenga zaidi urafiki simu zao, television, computer , vitanda, nyumba zao...
 
Umbeya na usumbufu vinachangia sana na hii inatokana na ugumu wa maisha.

Mitaa wanayoishi watu walioelimika na wenye vipato vya kati ni tofauti sana na uswahilini.
 
Back
Top Bottom