Hivi ni kweli kazi za TRA ni bora sanaa kimaslahi?

Liverpool VPN

JF-Expert Member
Aug 29, 2020
5,851
13,118
Wajumbe salamaaa.

Ni yuleyule Mr. Liverpool nikireport kutoka Anfield chini ya Mzee Klop..!!

Ngoja niingie kwenye mada.

Tarehe 22/10 TRA kupitia Sekretarieti ya ajira ili tangaza nafasi za ajira kibao.

Lile Tangazo bana likafika Ofisini..!!

Mimi ni mfanyakazi wa halmashauri fulani humu nchini..

Sasa wakati tupo lunch ofisini, katika maongezi ya kuzungumzia zile post ofisini kwetu watu 3 wamesema wao wataapply. Wakimaanisha wata jaribu transfer.

Maana wanaamini TRA Kuna maslahi sanaa kuliko ofisi nyingi za serikali na hasa huku halmashauri.

Ila nilivyokuja kuchunguza nikagundua, wote ambao tulikua kwenye yale maongezi ni kwamba aidha tulitoka private tukaingia halmashauri au tulitoka kitaa tukaingia halmashauri.
Ila hakuna alihama hamaa sanaa mwenye uzoefu na maslahi ya ofisi mbalimbali za serikali.

Sasa wajuzi ambao mlipata hii changamoto ya kuona "kwenye nafasi zenu za awali hakukua na green pasture nzuri kama kule mliko kuwaza" mkakomaa na sasa mko kwenye taasisi/ofisi nyengine na hasa TRA.

Hivi ni kweli TRA kuko Bora zaidi kuliko ofisi nyingi za serikali?

#YNWA
 
Back
Top Bottom