kiukweli wakati mwingine huwa nawahurumia sana ninyi mnaosomea taaluma tofauti chini ya kivuli cha NACTE/TCU,,,yaani mnatoka kapa sana hadi nashindwa kuelewa hiyo miaka yote mnakaaga chuoni kufanya nini hasa, hapa si UDOM tu peke yao ni vyuo vyote vinavyotumia mfumo wa NACTE wahitimu wake kusema kweli hawatimizi vigezo/hawana tija kwenye ajira, asilimia kubwa wanakuwa ni mzigo tu maofisini,,,,mfano ukichukua watu wa geology kutoka pale mlimani inataka moyo kufanya nao kazi maana hawana wanachokijua, ukija upande wa computer ndo kabisaaa eti mtu wa IT,C.Science, C.Engineering hajui hata RAM ikoje, hajui HDD ya sata na IDE zinafananaje, halafu unaniambia mtu huyo ka-spend 3 years kusomea fani hiyo kweli?,,,,,kiukweli VETA wanatoa taaluma safi sana kwa hapa Nchini cha ajabu wanadharaulika.