Hivi ni kitu gani kinatusumbua sisi mpaka biashara au utajiri wa kifamilia unakuwa mgumu sana au una shindikana kabisa ?

Mto Songwe

JF-Expert Member
Jul 17, 2023
6,029
12,353
Hili ni swali huwa najiulizi mara nyingi.

Hivi ni kitu gani kinasumbua jamii yetu mpaka utajiri au biashara za kifamilia kufa na kushindwa baada ya mwenye mali kufa ?

Maana ukitazama wenzetu waarabu wanaweza kufanya biashara au kuendeleza utajiri wa familia kwa miaka mingi sana vizazi na vizazi, wahindi nao hii kitu wanaweza, wachina wanaweza, wazungu nao wanaweza ila sisi ni nadra sana hii kitu kuwezekana.

Unakuta mali ya familia ni mtu mmoja tu anaijua peke yake hata watoto au mke hafahamu akifa yeye shughuli kwisha hapo na ugomvi wa mali unaanza mara watakuja na watoto wa michepuko ambao hata kuwa tambulisha mwenye mali hakuwahi hapo vurugu za mahakamani na waganga wa kienyeji zitaanza.

Kwenye jamii yetu mali au biashara za familia mwenye mali ni ngumu kuachia akiwa hai wengine wapate uzoefu bali ata ng'ang'ania mpaka kufa na mwisho naye zinakufa naye.

Ila kwa wenzetu cases za hivi ni ngumu kuona zinatokea ni rahisi kabisa mwenye mali kumuachia mwanae uongozi hata akiwa hai huku akimpatia uzoefu hata akifa mali zitaongezeka na kukua zaidi na zaidi ila kwetu mhhhhh!.

Jamii zetu ugomvi wa mali mpaka ukoo unahusika unakuta wajomba nao wanataka gawio wao kwenda mahakamani hawawezi kwa sababu kisheria hawawezi pewa ila wataenda mahakama za jadi hapo ni mwendo wa ushirikina tu.

Mfano tazama bwana Mengi baada ya kufa na migogoro ya mirathi ikaanza mahakamani full kupelekana mahakamani kisa mali wenzetu wanajitahidi kuweka mambo sawa mapema kabisa.

Je, ni nini hasa kinacho tusibu sisi katika hili ?
 
Nikwamba sisi tuna amini kwenye kuanza katika zero siku zote maana hii ni kama principle ya familia nyingi ni kwamba hatuamini katika muendelezo ?
 
Tutazame list ya matajiri wa hapa kwetu na historia ya utajiri wao na connection baina yao na familia zao ?
 
Mali nyingi za ulozi kuendeleza ni shida
Tatizo wazee hawataki kuwarithisha tunguli watoto,wanawaaminisha kwamba wametafta kwa jasho lao kumbe ni za kwa waganga...
 
Waswahili hawahitaji MAFANIKIO Makubwa most of them wapo materialistic driven with zero plan toward the success

Hatuna misingi Imara kata kukisimamia kitu ambacho sio chetu.
 
Back
Top Bottom