Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,486
- 30,166
Baada ya kuona haya mateso makubwa wanayopata wanabchi kwa kufunga barabara inayounganisha jijini Dar na Magomeni ikijirudia Mara kwa Mara kutokana na mvua kunyesha, nimekuwa nikijiuliza hivi hawa watawala wetu walitumia busara kweli kuamua kujenga daraja la kuunganisha Coco beach na Salenda, badala ya kutoa kipaumbele cha kuliinua daraja la Jangwani?
Imekuwa ni kawaida sana kwa siku za karibuni kila mvua inaponyesha, hata kama ni ndogo, tunaambiwa kuwa barabara ya Morogoro, inayounganisha Magomeni na jijini Dar imefungwa
Hebu tujaribu ku-imagine ni madhara kiasi gani yanayopatikana kiuchumi kila barabara hiyo inapofungwa?
Hebu pia tujaribu ku-imagine ni wakazi wangapi wanapata usumbufu wa kutokwenda kutibiwa kwenye hospitali ya Muhimbili au kwenda waona wapendwa wao waliolazwa katika hospitali hiyo kubwa hapa nchini kutokana na kadhia hiyo?
Lakini kwa kuwa nchi hii hivi sasa tunajua kuwa inaendeshwa kwa "misifa" ya ONE MAN SHOW, kila alitakalo bwana yule ni lazima litekelezwe, bila kwanza kuangalia ni kitu gani cha kutoa kipaumbele kwa muda tulionao
Nina hakika watu maelfu kwa maelfu wanaathirika sana na hii barabara ya Morogoro ya kipande cha daraja la Jangwani kinachounganisha Magomeni na jijini Dar
Pia soma:
1). Magufuli: Tutajenga flyover Salender Bridge
2). Yaliyojiri Uwekaji wa jiwe la msingi Daraja la Selander
3). Wabunge pingeni na kataeni kujengwa kwa Daraja la Juu ya Bahari kutoka Coco Beach to Agakhan

Serikali haikukosea na sipingi ujenzi wa daraja jipya la salenda lenye urefu wa km 1.5 ambalo ni kubwa kuliko lile la nyerere kule kigamboni.
Lakini ujenzi huu umekuja katika wakati ambao kwa maoni yangu sio sahihi ukilinganisha na kero nyingi za wananchi zilizopo kwa Sasa.
Ujenzi huu unagharimu Tsh bil 556.1 huku serikali ikitoa bil 49.5 ikiwa zaidi ya bil 506 zikiwa ni ufadhili kutoka Korea kusini.
Pamoja na kuwa mradi huu umekuja kwa lengo la kupunguza adha ya foleni katika eneo hili lakini kuna maeneo muhimu zaidi katika mkoa wa Dar es salaam ambayo yalitakiwa kupewa nafasi ya kwanza kwenye ujenzi.
1; Daraja la Jangwani.
Daraja hili ni kiuongo muhimu Sana hapa jijini, ikumbukwe kuwa shughuli nyingi za wana dar hutegemea sehemu hii kuunganisha wilaya kinondoni na Ilala kupitia fire na magomeni.
Mara nyingi daraja hili limekuwa likikumbwa na adha ya mafuriko na kufunikwa na maji hivyo kukwamisha shughuli nyingi kwa masaa mengi Sana. Hii ni kero kubwa na niaibu kwa jiji letu hili bora kabisa Afrika mashariki.
Badala ya daraja la salenda serikali ingeanza na hili kwanza.
2; daraja la mto msimbazi katika eneo la kigogo njia panda.
Hapa napo ni sehemu korofi sana lakini ina umuhimu mkubwa kwa wakazi wa jiji la Dar Kama ilivyo kwa eneo la Jangwani hapa napo tatizo ni lile lile, serikali isifumbue macho eneo hili, kila siku Makonda anakuja hapa kujifanya kuangalia athari za mafuriko bila kuchukua hatua yoyote ile, hapana tumechoka Sasa.
Badala kujenga daraja la salenda mngeanza hapa kwanza.
Na sio kujenga daraja tu bali mje na
mpango mkakati wajinsi ya kutanua mto msimbazi kupunguza athari za mafuriko kwa wakazi hawa.
Nasisitiza kusema ujenzi wa daraja la salenda serikali yangu imekurupuka mlitakiwa kuangalia ni eneo gani linagusa watu zaidi Kama kweli hii ni serikali ya wanyonge.
Achaneni na miradi inayolenga tu kupendezesha jiji huku wananchi wanalia.
Mh Rais wangu mpendwa naomba liangalie hili utakuja kuwaambia nini Wana Dar es salaam wakati wa kampeni??
Umejenga mfugale na ubungo ujenzi unaendelea hatupingi kabisa lakini hao watu wanao tokea kimara kupita ubungo kwenye flyover kuja kariakoo watapita wapi wakati Jangwani daraja linajaa maji MH RAIS?
Mh Makonda unayaona haya?
Wananchi wamechoka kukuona unakuja na macamera kupiga picha za daraja kufunikwa na maji watu wanashindwa kuendelea na shughuli za kila siku we kazi unakuja kupiga picha au mnaona kuwa hili ni kivutio cha utalii.???
Tumechoka!!.