Walioiba fedha zilizotajwa na CAG wabanwe warudishe zijenge daraja la Fire - Magomeni Mapipa

Mzee wa Twitter

JF-Expert Member
Nov 5, 2023
1,272
2,028
Wadau nawasabahi.

Nichukue fursa hii kuwapa Pole mamilioni ya watanzania wanaoteseka na tatizo sugu lisiloisha la MAFURIKO eneo la Jangwani Jijini Dar.

Tatizo hili limekuwa ni agenda ya kisiasa ya kuwadanganya wananchi badala ya kuwa Agenda ya Serikali ya KUTEKELEZA UJENZI wa DARAJA. Viongozi wamekuwa wanatoa matamko kila Mafuriko yakitokea kuwa tutajenga DARAJA la urefu kadhaa na upana kadhaa kisha hunyamaza mpaka yatokee mafuriko mengine lugha ni hiyo hiyo.

Serikali ina Fedha nyingi sana FEDHA ambazo Masikini wananchi wamekuwa wanakamuliwa kupitia Matozo na Kodi lukuki lakini SERIKALI badala ya KUBANA MATUMIZI imekuwa na Matumizi makubwa sana na mengi hayana Tija kwa Taifa zaidi ya Viongozi tu. Serikali ina tumia MABILIONI ya Fedha kununua Magari ya Kifahari kila Mwaka
Serikali inashindwa kudhibiti Ufisadi unaofanywa na Watendaji wake Kama REPORT ya CAG inavyoonyesha WIZI MKUBWA.

HALMASHAURI kwa kushirikiana na WIZARA za HAZINA na TAMISEMI zimekuwa VINARA wa Upigaji wa Fedha zisizo na Maelezo Kama Sakata la Kigoma lilivyoibuliwa na WAZIRI MKUU.
USHAURI kwa SERIKALI.

Tunaishauri SERIKALI iwabane Wahusika wote waliopiga Fedha za UMMA Kama Walivyotajwa kwenye REPORT ya CAG kwani ni MATRIONI ya Fedha Fedha ambazo zitumike KUJENGA DARAJA la FIRE-MAGOMENI MAPIPA badala ya kuwaacha MAFISADI watambe na Fedha hizo huku MAMILIONI ya Wananchi wakiteseka na MAFURIKO ya kila Mwaka.

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom