mrangi
JF-Expert Member
- Feb 19, 2014
- 80,852
- 106,056
Dawa si kuinua barabara, dawa ni kuvunja nyumba zilizo bondeni3ili maji yapite
Tuache ubinafsi, barabara ya nyakanazi to kigoma ndio muhimu zaidi,,jangwani ni makosa ya kujenga namna ile wakati mto mkubwa unapita pale
Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo kila mtu leo hii ni mtaalamu wa ujenzi na mazingira. Kweli unaamini mto huo ukichimbwa mafuriko yatakoma? Unauita mto sawa, mi nasema ni bonde linaloanzia Gongo la mboto. Utachimba tangu gongo la mboto hadi Selander? Hiyo idadi ya watu waliovamia bonde hilo uwaweke wapi? Unachimba nini na kimetoka wapi? Vowanda vya tabata unaviweka wapi?Mapendekezo yenyewe haya hapa chini. Niliyaweka hapa 17July,2018 kwenye uzi wa Mbu wa Muhimbili
Mbu wa Muhimbili
Hawa wa hapa Muhimbili ni kama wamekuwa biologically modified kama sio specie tofauti na nyingine. Mbu anatoboa hadi turubai..!!www.jamiiforums.com
Hii si sawa kabisa, kuparamia utaalamu wa ujenzi na mazingira, kumradhi kwa hilo. Hata hivyo nimeshangazwa na namna ulivyoshindwa kutumia 'professionalism' kuuliza ni namna gani utekelezaji wa mpango ninaopendekeza utakavyokuwa; kwa kuanza na swali la '.....unaamini mto ukichimbwa mafuriko yatakoma..!?'Tatizo kila mtu leo hii ni mtaalamu wa ujenzi na mazingira.
Lakini si busara pia wataalamu kukaa kimya, mkisubiri sijui amri ya nani, huku mambo yakiharibika. Ndiyo maana sisi ambao siyo wataalamu tunalazimika kuumiza vichwa kuona namna gani tatizo linaweza kuondolewa kwa haraka na kwa faida ya wengi.Tusijipe ufahamu wa haraka na kuona ufumbuzi. Ni tatizo gumu kuliko tuonavyo hapo kwenye mafuriko.
Tuna miundo mbinu ya hovyo sana Dar tena miaka yote , yaani hapo Jangwani kumeshindikana mara utasikia feasibility study zinatumia bil 50, mara tunasubiri world bank, tatizo kubwa hatuna mipango ya maana ya maendeleo, tukangefanya tafiti ya maeneo korofi yote mfano jangwani ,sewage system modernization ya mji wote Dar, Barabara za mwendo kasi phase 2 & 3, tukazichukulia mkopo mara moja kwa pamoja zikajengwa, baada ya hapo kinachobaki inakuwa ni kulipa tu loan, shida iko pale mnakaa miaka mitano mkisubiri pesa mpate huku watu wanatabika, au mnakwenda kuchukua mkopo wa jangwani peke yake ,baada hapo mnakaa kusubiri tena tatizo litokee sehemu Fulani hao mnakimbia huku mara kule, very bad.
Chukueni mara moja mikopo jengeni mmalize yote then kaaeni kukusanya pesa mlipe, ndio maana Africa iko hivi, watu wanahamia sehemu Fulani wanazaliana ,population inaongezeka ,hawana maji au barabara ndio serikali inatoka usingizini kuanza kuplan wakati huo kumekuwa hakuna jinsi wanaishia kubomolea watu majumba yao, wakati nchi za nje wanapeleka kwanza maji, barabara zinajengwa, umeme unakuwa huko, shule zinajengwa, hospital halafu wana encourage watu wahamie kule, sisi ni opposite kila kitu ni holela sijui tuna nini kichwani. Mnakumbuka Jangwani tumeimba miaka yote, mwendo kasi kelele nyingi tumeishia phase leo 2020, mitaro ndio hivyo tena mvua ikinyesha, 58 yrs ya uhuru hatujui tufanye nini, wapisheni na wengine wajaribu.
Mlalahoi unawahi kwenda wapi? Wacha matajiri wawahi kwenda tra kulipa Kodi ili mlalahoi apate matibabu watoto wasome bureHata wewe inaonekana kabisa tatizo hujalielewa! Haijalishi yalianza lini na nani aliaababisha! Mimi na wengine tumeshuhudia haya matatizo ya jangwani miaka na miaka!
Ni kwa nn hii serekali iliopo wakati huu na ikifanya miradi mingi na mikubwa ya ujenzi kimfano daraja la baharini, ukilinganisha na kero inayotokea jangwani kila mvua zikinyesha, pesa tunazo ndo mana tunajenga! Tatizo ni nn??
Kuna mdau hapo juu yeye alisema daraja la jangwani wanapita walala hoi na daraja la baharini wanapita wenye hela zao!
Na mi naunga mkono hoja hii.
Sent using Redmi Y2
Unacho kinena sahihi kabisa, Kati ya watu na bonde Nani kamfuata mwenzie? Hamieni dodoma yaacheni maji yapite zake kwenda baharini, mnakuwa Kama mumevaa mawigi mnataka kuoga shower bila kulowana kichwaUshauri wangu wa haraka ni kwamba siyo kila mafuriko yanarekebishwa kwa ujenzi wa madaraja na kuchimba mitaro. Kuna wakati tunayapisha na kuna sehemu duniani zimeachwa na binadamu, kutafuta sehemu zenye amani. Miji huanza na kufa! Using'ang'anie Dar hata kama nature hairuhusu tena!
Dar ni mji ulioanza kama bandari, maji mengi ni sehemu ya sifa za bandari. Kwa nini unalazimisha ufie Dar na kulaumu serikali, ifanyeje?
Tutakuwa tunapita huko huko , aandae tuu traffic wa kutosha. Huko baharini.
Hizo porojo za kajima tunazifahamu. Ila kabla ya ujenzi huu wa BRT maji yalikuwa hayapandi juu ya daraja. Maji yameanza kupanda juu ya daraja baada ya huu ujenzi kwa kuwa wameyang'anya maji sehemu ya kutulia bahari inapokuwa imejaa.Tatizo lako wewe mtoto wa juzi! Wakati kajima anakamilisha hilo daraja lilikuwa juu sana. Uchafuzi wa mazingira umesababisha Mchanga na takataka kujaa. Hata wakiinua vipi bila mkakati wa kupambana na uharibifu wa mazingira ni kazi bure. Aidha kama umeishi ulaya, utakuwa umeona jinsi vijito na mito inavyotunzwa! Lazima tuwe na culture ya kutunza mazingira si kila siku kujenga. Daraja hili linakupigisha kelele kila siku. Shame on you