Hivi ni kipi kilipaswa kujengwa kwanza, ni kuinua daraja la Jangwani au kujenga Daraja jipya la Salenda hadi Coco beach?

Wamejihujumu wenyewe.........
Unajenga Barabara hapo Jangwani na Wanajua fika matatizo ya hapo..... Na wametumia mabilion ya fedha
Leo hii hapo panatakiwa kuvurugwa tena na kujenga daraja kutoka magomeni mpk fire
Ina maana pesa ikiyotumika mwanzoni ni Sawa na kutupwaa msalani
Sasa mpaka hapo sisi tun akili au matope

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbe Mkuu impongo hao tunawaita mabeberu pale tunapowaponda, lakini tunapowanyenyekea na wanapotupa misaada, jina lao linabadilika na kuwa wahisani?
Daraja la mfugale... Kwa ajili ya Mabeberu na viongozi from AIRPORT TO CITY CENTER... .

Nyie wanyonge pambaneni na foleni zenu...
 
Mystery,

Ukiwa na Akili timamu na zinakutosha vyema tu Kichwani mwako huwezi Kuanza na Daraja la Agha Khan hadi Coco Beach kupitia Baharini na ukapuuzia njia na Daraja muhimu katika Nyanja zote hasa kwa Mkoa wa Dar es Salaam kama la Jangwani.
 
Acheni ulevi. Si mngegombea na nyie ili mpate fursa ya kufanya mnachofikiri ni sahihi?

Wananchi wanapomchagua mtu awe rais wanajua wanachofanya.

Msitake kulaumu serikali ya Magufuli kwa vipaumbele vyake. Mjilaumu wenyewe kama mnaona hafai.

Na kama kweli hafai uchaguzi ni miezi michache sana ijayo, pigeni kura mumwondoe akapumzike.
 
Tumeshatoa ushauri na mawazo, ila watu wamekalia kuongelea mambo ya siku za kusali, kusajili ndoa, sijuwi nini na nini, coco beach tu shughuli, pako super mno ila wanashindwa kufanya lolote, vyoo 2 tu ukanda wote ule?!
Wahusika wana mawazo mgando kuliko, bure kabisa...
 
Tunajionea tu Mkuu Abul Aaliyah kila siku Jiwe akijigamba hadharani kuwa hii ni nchi tajiri sana, tunaweza kuwa "donor country"

Hivi kweli nchi tunayoambiwa ni tajiri sana, inaweza kusumbuka kila leo na hii adha ya kufungwa daraja la Jangwani kila mara?
Mvua zikiisha nyinyi nyote mnao lalama mtaungana na serikali kusahau daraja la jangwani! Mtaanza tena kipindi cha masika. Mtasahau tena baada ya masika kwisha. Hivyo hivyo mpaka mnazeeka. Au mnahamia chama tawala na kufumbuka macho.
 
Wakati kajima anakamilisha hilo daraja lilikuwa juu sana. Uchafuzi wa mazingira umesababisha Mchanga na takataka kujaa. Hata wakiinua vipi bila mkakati wa kupambana na uharibifu wa mazingira ni kazi bure.

Aidha kama umeishi ulaya, utakuwa umeona jinsi vijito na mito inavyotunzwa! Lazima tuwe na culture ya kutunza mazingira si kila siku kujenga. Daraja hili linakupigisha kelele kila siku. Shame on you
 
Hivi mabalozi wengi wa nchi za nje wanakaa wapi na ofisini zao zipo wapi? Mambo mengine ni matakwa ya wageni. Mfano wakati wa ukoloni mambo yote mazuri hayakufanywa kwa kumnufaisha mzawa.
 
Nashukuru , hili nilikua naliwaza sana. Nakuunga mkono. Kwann tatizo la miaka nenda rudi halitafutiwi ufumbuzi? Wanahangaika na wakazi wa mabondeni tuu kila siku lakini kutatua tatizo la msingi hawatatui. Fedha za daraja salenda zingeelekezwa hapo na chenchi ingebaki.
 
Tatizo lako wewe mtoto wa juzi! Wakati kajima anakamilisha hilo daraja lilikuwa juu sana. Uchafuzi wa mazingira umesababisha Mchanga na takataka kujaa. Hata wakiinua vipi bila mkakati wa kupambana na uharibifu wa mazingira ni kazi bure. Aidha kama umeishi ulaya, utakuwa umeona jinsi vijito na mito inavyotunzwa! Lazima tuwe na culture ya kutunza mazingira si kila siku kujenga. Daraja hili linakupigisha kelele kila siku. Shame on you

Ni kweli hili daraja ni la miaka mingi sana na halikuwahi kuleta kero kama hizi hapo kabla.

Vipi hizi kero zije baada ya kujenga mwendo kasi na ofisi zake pale?

Kilichofanyika, walipoongeza barabara ya mwendo kasi na kujenga ofisi kuna mkondo umefinywa pale, matokeo yake kutapika kule na si swala la mazingira Boss!
 
hakuna daraja linalounganisha Salender na Coco Beach... daraja linaanzia Sea View linakuja sambamba na Salender, linaishia Ubalozi wa UK ambao uko karibu na mataa ya Salender njia panda ya Kinondoni, ambapo ndio Oysterbay inapoanzia. Coco Beach ipo kwenye edge ya Masaki, Oysterbay inapoishia. Kwa hiyo hili daraja litakuwa linachukua traffic ya Kinondoni na Mwenge pia.

hakuna njia ya jangwani inayounganisha Magomeni na jijini D'Salaam kwa sababu Magomeni ipo jijini D'Salaam...

tuuelewe kwanza mji na mabarabara kabla ya kupendekeza na kukosoa madaraja na mafuriko.....
 
Back
Top Bottom