Hivi ndivyo nilivyotapeliwa mwaka 2005 na matapeli wanaokutemesha nywele mdomoni au kukutoa moshi kitovuni, siwezi kuja kusahau!!

Uncle bright

JF-Expert Member
Feb 9, 2023
1,040
4,080
Enzi hizo tulilizwa wengi kwa hii staili sababu hata mtu akipigwa inakuwa siri hakuna mitandao ya kuelimishana.

Mwaka 2005 nipo nakaribia kuvuka barabara ghafla mzee mwenye koti lake anaulizia hospitali nikamwelekeza ilipo maana haipo mbali ila yeye akasema ni mgeni, akaja mtu mwengine nae akamwelekeza ila akasema tumsindikize, nikaanza kujikuta nafata maelekezo nasindikiza na hapo hakuna maslahi yoyote(inasemekana huwa wanatumia madawa kukushika akili),

Nikiwa nasindikiza kama zuzu bila kujitambua ndio mzee akaanza stori kibao yeye ni bingwa wa tiba asili ila kutoa shukrani ya kumsindikiza atatusaidia, akaanza kutuambia kwamba mimi na huyo mwengine tumerogwa, huyo mwengine alitema vitu kama karatasi hivi mzee akasema ziliingizwa kichawi lakini kwangu mimi akaniambia nina uchawi mkali nimemezeshwa nywele inabidi twende sehemu akazitoe.

Tukaingia uchochoroni, nikatapishwa nywele akasema kuna mtu ananiroga kaamua kunisaidia kutoa uchawi ila kila kitu nilichokuwa nacho mfukoni niweke kwenye rambo, mfukoni niweke tu nywele nilizotapika niende kuzichoma nikifika nyumbani, nilitoa vitu mifukoni nikaviweka kwenye rambo iliwemo simu ya nokia na pesa takribani elf 80, niliambiwa tu nitunze 200 ya daladala niishike mkononi, hivyo vitu nivitoe nikishazichoma zile nywele.

Navyoondoka niliambiwa nisiangalie nyuma na niwe nasema nimepona, basi ndicho nilichofanya, kwa furaha niliyokuwa nayo kwa kudhani nimetolewa uchawi ni kweli nilipaza sana sauti nilitamka kama mwehu mara 10 hivi.

Nafika nyumbani nikakoka mkaa kuandaa moto, nikazichoma zile nywele, nikachukua ile rambo nyingine nitoe simu na hela, LA HAULA !! nikakuta kipande cha sabuni na mabox.

Nilipagawa sana, nilirudi sehemu niliyokutana nao nikaanza kuwatafuta, nikaanza kuuliza kila mtu "umemuona mzee flani ana koti la kijivu na kijana flani ana afro kafuga nywele?", niliamua kuondoka tu maana kuna watu ni kama wakaanza kuambiana nimepigwa nikaona soo kuanza kuchorwa.

Hii gia waliwahi kutaka kunifanyia upya nilibaki nawacheka tu, yani wanapenda sana kumtumia mzee ama mtu anaonekana wa bush kisha hapo hapo anakuja mwengine kujidai anaelekeza njia, Jibu nililowapa liliwatosha kupotea mtaa huo ndani ya sekunde chache

Wengine walikuwa wanafanya uone kitovu kinatoa moshi kusingizia wanafukuza jini.
 
Nyie ndio mliokuja na gari za mizigo ya viazi na Michele mjini.
kupigwa hakuepukiki tatizo wabongo wakipigwa hawataki wengine wajue, ni kimya kimya lakini wakisikia mwengine anatoa ushuhuda wake wanamcheka, Huu ni UJINGA.

Ukiumwa usione aibu kutumia kinga ili ugonjwa usisambaae.
Ukitapeliwa usione aibu kuelimisha wengine ili wasilizwe kirahisi
 
Huo wizi ulitanda miaka ya 2000 mwanzoni mpaka Kati ya 2006. Ila hawatumii uchawi wao wanacheza na psychology yako. Kosa kubwa ni tamaa maana hapo walikuambia uwasindikize watakulipa hela, na huyo aliekuja wa pili ndio anakuchota wewe.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
hakukuwa na hela mkuu, kati kati ya safari ndio mzeeakaanza mambo ya tiba
 
Walimkamata jamaa yangu mmoja miaka ya 2007 hv..alikuwa mzee anataka aelekezwe hospitali moj maeneo ya kariakoo akatokea mwingine akamwambia waongozane wamsindikize huyo mzee.....walimzungusha wee mpaka jangwani huko wakamfanyia hayo mazingaombwe ila kwenye hela jamaa hakuwa hata na mia mfukoni so wakamwacha
 
Wala hakuna uchawi ni ujinga wako tu na saikolojia,yule mtu wa pili anayekuja kama ana haraka zake halafu anajifanya kusimama ghafla na kumuelekeza njia huku anakulaumu ni kwann unaahindwa kumpeleka mzee ndo uchawi wenyrwe!!
Mimi niliwaacha kwenye Mataa maeneo ya cbe pale,alikuja mzee anasemq ametoka tanga anauliza shule ya kisutu nimpeleke,wakat natafuta msaada akatokea mjamaaa anajifanya anaharakaaa wakati tunaanza safari alivojichanganya akawa anaongea sana na yule mzeew kuhusu uchawi kuliko mm,nilivoona stori zimewakolea wao wawili nikapiga UTURN nikamwambia bro basi utamfikisha maana inaonesha mnaelewana,nikasepa zangu
 
ulitisha
 
Back
Top Bottom