Jinsi nilivyotapeliwa na wakushi ambao hutumia uchawi/mazingombwe ya kumtemesha mtu nywele na kucha

NetMaster

JF-Expert Member
Sep 12, 2022
1,454
4,845
wanakupumbaza akili kwa madawa ya kienyeji ama technique wazijuazo wao na kukufanyia mazingaombwe ya kukutemesha kucha au nywele, huwa wanakua wawili mmoja anajifanya anauliza sehemu mwengine anajifanya mpita njia.

Mkasa wangu niliwahi kumsimulia mtu moja tu wa karibu sana, wengine huwa nadanganya kwamba "ilibaki kidogo nitapeliwe", "niliwatoroka", "nilijiongeza", n.k, hivi ni vichaka ambavyo watanzania wengi tunavikimbilia kukwepa aibu ya kuchekwa na kuonekana washamba ila kiuhalisia sio ushamba, haya mambo hata maprofesa wanaliwa timing wanaingia kingi ila wanapiga kimya, hata hao wanaocheka na kuwaona wenzao ni washamba nao wameshawahi kutapeliwa ila wanaficha ukweli. Huku JamiiForums kuna usiri kwa hio naweka mkasa mzima.

Kilichonikuta mimi ni hiki;

Ilikua mida ya mchana majira ya saa saba katika jiji mojawapo hapa nchini, niliondoka ofisini niende centre kwenye maduka kununua vifaa kwajili yakukamilisha kazi ya mteja, nilipofika centre nilishuka kwenye bajaji nikaanza kutambea kuelekea madukani, mbele hatua kadhaa nilikutana na mzee mmoja wa makamo mwenye umri Kama miaka 48 au zaidi na alikua amevalia tisheti nyeusi na suruali ya jinsi ya blue iliyopauka kwa kuchakaa.

Alinifuata na kuniuliza "Kijana hoteli ya wapemba unaifahamu? Mimi ni mgeni katika hili jiji naomba unielekeze”. Kabla hajamaliza kuna mpita njia kijana alipita amesimama karibu yetu ni kama anataka kuvuka barabara, yule mzee akasema ngoja nimuulize huyu kijana.

Akamuuliza, "Samahani kijana hoteli ya wapemba unaifahamu?" Yule mpita njia akamwamuonesha kwa kidole akiangalia upande wa mashariki akasema “Hoteli ya wapemba iko tu pale”, akamwambia yule mzee “Twende kidogo hapo mbele nimuelekeze huyu (mimi) akupeleke manake mimi nawahi stendi kumpokea mtu".

tukaanza kutembea kuelekea huko na hata sijui niliwezaje, maana nilienda centre kwa mambo mengine ila nikajikuta nafanya vingine. Tukiwa njiani ili yule mzee akaanza kusema, "Mimi nimetoka Morogoro natibu kwa kutumia kitabu, hata nyie nikiwaangalia tu viganja vyenu naweza kujua nyota zenu na matatizo yenu".

Yule mpita njia mwenzangu akamjibu"Hebu tuangalizie", akamwangalia kiganjani alitikisa kichwa kwa masikitiko akasema kwa uchungu "Wewe umehangaika sana hapa mjini lakini hujafanikiwa kwakua umelishwa kucha za maiti" jamaa alishtuka akawa kama amepanik hivi.

Ikafika zamu yangu nikampa kiganja akasema "Wewe una nyota nzuri lakini umelishwa nywele za mtoto mchanga, kuna mtu hapendi ufanikiwe zaidi ya hapa ulipo na pia nywele hizo zinakufanya usiwe na nguvu, huwezi kuja kuzalisha mwanamke". Niliingiwa na woga.

yule mpita njia akamwamba yule mzee “tusaidie kuondoa matatizo hayo mkuu" yule mzee akasema "mna kioo hapo?" tukajibu hapana akauliza mna karatasi nyeupe, yule mwenzangu akaitikia " ndio" akatoa karatasi mfukoni akampa akaishika kisha akasema " tafuneni hiyo karatasi” aliigawa vipande viwili, tukapokea na kuitafuna, akasema "haya kohoeni kwa nguvu", naam!

Sikuamini nachokiona, nikakohoa nywele kidogo na mwenzangu akakohoa kucha, baada ya hapo mzee yule alionesha kukasirika akaongea kwa ukali, "Nimesema mkohoe kwa nguvu mmekohoa taratibu, nywele zimebaki tumboni na kucha sasa mtakufa sijui niwasaidiaje”. Nilitetemeka kwa woga.

Yule mzee alikuwa kama anatafuta mbinu ya kutusaida huku kashika kichwa, mimi hapo najuta hata kukutana naye, yule mwengine anamuomba kila mara “Mzee tusaide”. Baada ya dakika 2 hivi akatuambia "Sasa sikilizeni fuatani maelekezo nitakayowapa la sivyo mtakufa hapahapa” aliongea kwa msisitizo akaanza kutoa maelekezo.

"Hizo nywele na kucha mlizotema inabidi muwahi kwenda kwenu mkazichome kwa manuizi ili mziyeyushe zilizobaki tumboni, mnavyozichoma wewe ulietema kucha nuia kucha zote zilimo tumboni ondoka na wewe wa nywele nuia nywele zote zilimo tumboni ondoka. “

Tulitafuta karatasi pembezoni, yule mpita njia alifungasha kucha zake na mimi nikafungasha nywele nilizotema. Baada ya hapo yule mzee akatuambia tuweke kwenye mifuko ya suruali lakini kama hairusiwi mifuko mingine iwe imebeba chochote, iwe ni ya suruali/jeans, shati au koti kwahiyo tuvitoe vyote tulivyovibeba tuvifungie ndani ya rambo.

Kulikuwa na kijiduka kwa karibu yule mpita njia alienda kununua vimifuko viwili ni vile vikaki, yule mpita njia aliweka saa, pesa kama elf 70 hivi na simu mbili, mimi nikaweka pesa 138,000 na simu. Tuliambiwa tuchukue pesa ya nauli tu, yule mpita njia alisema kwao siyo mbali atatembea, mimi nilichukua buku ambayo ilikuwa ndogo katika hela nilizoweka.

Zile kaki mzee akatupa zikiwa zimekazwa na akatuambia "Hii mifuko msithubutu kufungua mpaka mfike kwenu, mkifika kwenu muiweke pembeni, mchome kwanza hizo nywele na kucha huku mnanuia nilivyowaelekeza, baada ya hapo ndiyo mnaweza kuchukua vitu vyenu vya kwenye hio mifuko".

Yule mpita njia alisema anarudi kwao ambako ni karibu na ile hoteli aliyoulizia yule mzee kwahiyo wacha amsindikize kwanza mzee. Mimi nikamuaga yule mzee na kumshukuru, mzee alinikumbusha kwamba nichome kwanza zile nywele ndiyo nifungue mfuko.

Nilifika stendi ya mabasi nikapanda usafiri nikarudi kwangu, nilipofika kitu cha kwanza nilichukua kiberiti nikaenda kuchoma kile kikaratasi nilichofungashia zile nywele. Baada ya hapo sasa nikaenda kufungua kaki ili nitoe simu nicheki kama kuna missed call au message, daah!

Yaani ndani ya bahasha nilikuta vipande vya maboksi vyenye ukubwa wa zile noti na nikaona kuna kimbao fulani ukubwa kam wa simu, pamoja na uanaume huu nusu nipige ukunga aisee! Nilikagua ile bahasha kama dakika 5 hivi siamini nachokiona, nilipaniki na kuchanganyikiwa nisijue cha kufanya kwa yaliyonikuta.

Nilirudi centre ile sehemu niliyowakuta nikazunguka sana mpaka kule eneo la tukio, nilikuwa nauliza watu wenye shughuli zao maeneo hayo kama wamewaona nikijaribu kuwaeleza walivyovaa na walivyo ila hakuna aliewaona, wengine nikiwauliza hata kabla sijamaliza wanajibu kwa mkato, umeshapigwa!

Basi hayo ndiyo yaliyonikuta, nikisimulia wenzangu huwa nawadanganya kwamba nilijiongeza kiakili nilikataa kutoa pesa na simu nikaondoka nikaamua liwalo na liwe lakini ukweli bado naujua mimi mtendwa kwamba niliingizwa chaka.
 
Hv hizi pesa hawa jamaa huwa wananufaika nazo sana kama kujenga nyumba za kisasa kumilik usafir au huwa wanaishia kutumia kwa matumiz ya kula tu
Kuna binti flani ni muhudumu wa gesti kwenye stori za hapa na pale aliiambia gesti yao imezoeleka na matapeli huwa ni kama wanapenda kukutana hapo, wakinywa pombe huwa wanafunguka vingi, wengi walianzisha biashara lakini wanaambulia hasara na biashara, kama kuna biashara huwa ni kwajili ya kusafishia pesa ili waonekane wanapata fedha kihalali, hata kama dukani mauzo ya mwezi mzima ni elf 50 wao wanadanganya ni milioni 2 ilimradi wawe na ushahidi kwamba pesa zao ni halali.

kinachowasaidia ni kwamba wana ushirikiano sana, mwenzao akikamatwa huwa wanamtoa fasta maana wana connetions nyingi na mapolisi, huwa wanasaidiana sana hawa jamaa lakini ukiingia kwenye makundi yao huwezi kutoka kirahisi na huwa kuna mambo ya ushirikina kiasi kwenye kufanya kazi zao.
 
🤣🤣Hao wasng nishawahi kukutana nao mara 2 aisee moja ilikua 2015 hv na nyingne mwaka 2019 na zote walifanikiwa nikaongozana nao lakan kuna sehemu nilifka nikafanikiwa kuwatoroka mara zpte mbili lkn sjui waliwezaje mpaka nikakubali kuwasindikiza aisee wana dawa kaLi ila nna uhakika mm nimeaga kwetu qummk na waliniambia hvhv mamb ya nyota aisee
 
🤣🤣Hao wasng nishawahi kukutana nao mara 2 aisee moja ilikua 2015 hv na nyingne mwaka 2019 na zote walifanikiwa nikaongozana nao lakan kuna sehemu nilifka nikafanikiwa kuwatoroka mara zpte mbili lkn sjui waliwezaje mpaka nikakubali kuwasindikiza aisee wana dawa kaLi ila nna uhakika mm nimeaga kwetu qummk na waliniambia hvhv mamb ya nyota aisee
mimi nikisimuliaga huu mkasa kwa wengine wanaonijua huwa nadanganya kwamba niliongozana nao lakini niliwatoroka, watanzania wengi wana nazoea ya kumcheka mtu alietapeliwa kwahio ni ngumu kuwa muwazi.

huku jamiiforums hakuna anaenijua nipo huru
 
Pole sana ila nikupe mbinu wanaanza kukuteka tangu unapokuwa unawasikiliza kuwa makini mjini ni hatar sana.
ubaya wa hawa jamaa wana mbinu nyingi sana, leo utakwepa x lakini kesho unaangukia kwenye y.... watu wengi sana wanatapeliwa lakini huu utamaduni wetu wa kumuona mtu alietapeliwa ni mshamba unafanya waliotapeliwa kubaki nayo moyoni, haya mambo ilibidi mtu awe wazi kuelezea ili na wengine tuelimike
 
ubaya wa hawa jamaa wana mbinu nyingi sana, leo utakwepa x lakini kesho unaangukia kwenye y.... watu wengi sana wanatapeliwa lakini huu utamaduni wetu wa kumuona mtu alietapeliwa ni mshamba unafanya waliotapeliwa kubaki nayo moyoni, haya mambo ilibidi mtu awe wazi kuelezea ili na wengine tuelimike
Haina ujanja wale wanakulegeza kabisa Wana uwizi kibao wa kila aina ndo maana hata wale ombaomba hapa Town watu wanaogopa kuwasaidia hujui wale wezi watakuja kwa njia ipi? Ni kuomba mungu tu...Kuna jamaa aliibiwa na mzee anasema walikutana huko muhimbili mzee anaumwa yuko na jamaa anasaidia kutembea jamaa yeye alikuwa anaelekea kigamboni wale wakasema wanaelekea huko huko Tena darajani kwa mbele.

Jamaa akawabeba walikuwa na begi yule kijana kabeba Yale ya billbong kama ya laptop..basi jamaa alienda kufika darajani akawashusha kama dk 5 anaangalia vitu kweny gari kama PC yake hamna, na kweny alikuwa na pesa pia kweny kijibagi chake cha kazini hamna pia, mda huo jamaa alitoka kazini aliomba ruhusu kwenda muhimbili kufanya check up then achukue dawa arudi kwake kupumzika ila kaibiwa vitu kibao mpaka kadi ya bank mpaka anashangaa wamefungua saa ngapi..amerudi pale darajani fasta Tena na gari hakuna mtu hata mmoja wamesepa kweupe yaani saa 7.
 
Haina ujanja wale wanakulegeza kabisa Wana uwizi kibao wa kila aina ndo maana hata wale ombaomba hapa Town watu wanaogopa kuwasaidia hujui wale wezi watakuja kwa njia ipi? Ni kuomba mungu tu...Kuna jamaa aliibiwa na mzee anasema walikutana huko muhimbili mzee anaumwa yuko na jamaa anasaidia kutembea jamaa yeye alikuwa anaelekea kigamboni wale wakasema wanaelekea huko huko Tena darajani kwa mbele.

Jamaa akawabeba walikuwa na begi yule kijana kabeba Yale ya billbong kama ya laptop..basi jamaa alienda kufika darajani akawashusha kama dk 5 anaangalia vitu kweny gari kama PC yake hamna, na kweny alikuwa na pesa pia kweny kijibagi chake cha kazini hamna pia, mda huo jamaa alitoka kazini aliomba ruhusu kwenda muhimbili kufanya check up then achukue dawa arudi kwake kupumzika ila kaibiwa vitu kibao mpaka kadi ya bank mpaka anashangaa wamefungua saa ngapi..amerudi pale darajani fasta Tena na gari hakuna mtu hata mmoja wamesepa kweupe yaani saa 7.
Hao omba omba wengi wanatolewa mikoani huko wanaletwa na magenge ya mjini kila moja wao anapewa eneo lake la kuomba na pesa inaenda kwa wahuni, wao omba omba wengi wanapewa hela ya chakula tu.

omba omba wanaotaka bonus za ziada hufanya wizi ila bado watapeleka walichoiba kwa wakuu wa magenge yaliyowaleta, hayo magenge ndio huwa wanachora script za kuwaibia watu kama huyo aliewapakiza kwenye gari na kuibiwa laptop, wakipeleka hio laptop wanaambulia hela ya chakula walau kizuri na bonus ya elf 20 imeisha hio!!, laptop inaenda kuuzwa hata kwa laki 6
 
Pole sana mkuu....
Mimi pamoja na kuzurura kote mitaa ya kariakoo, karume , ilala...sijawahi kukutana na hawa watu...naskia story tu kwa watu
Huna nyota ya Bahati!! hao nimesha kutana nao sana!! taaangu nikiwa seco. na karo zangu hawakuniweza!.....namie nilikuwa nawafanyia usanii mmoja alitaka nidhurumu simu palee magomeni Morocco!

baada ya mazungumzo marefuuu alisema hebu tuone simu yako nimuite Padre nikampa simu imefungwa na rubber Band siyo za dunia hii!! ikabidi acheke wala sikuwa na wais wasi nenda kapigie hata huko nje!

akazuga kidogo akanambia padre hapokei simu!.....soda misosi yake nikanywa na kula bureee!! kifupi mie ndo nilifaidi! mwingine kaja ofisini ke wa kiarabu mzuriii! kabisaaa

anakasema ataka kwenda Tanga, kuchukua biashara so nimkopeshe Laki moja tu! nikasema sawa mbona hiyo kidogo tu! ila nisubiri hapo naenda Bank kukuchukulia! akasubiri weeee! mpaka leo! anasubiri!

halafu hawanaga kumbukumbu nzuri siku nyangine usiku nakula zangu chips! kwa kioski kaja huyo huyo! kwa mambo yale yale!..nikwambaia nilikwambia siku ile unisubiri nirlipo rudi sija kukuta kumbe hukupata??

dada wa watu kakata moto palepaleee akawa wa baridiiiii!!...........
 
mimi nikisimuliaga huu mkasa kwa wengine wanaonijua huwa nadanganya kwamba niliongozana nao lakini niliwatoroka, watanzania wengi wana nazoea ya kumcheka mtu alietapeliwa kwahio ni ngumu kuwa muwazi.

huku jamiiforums hakuna anaenijua nipo huru
Hata mm kuna watu hawaamini kama niliweza kuwatoroka tena mara 2 kbsa ya kwanza ilikua jion ya pili usiku kbsa saa moja kuelekea saa 2 usiku tena hyo ya saa 2 usku ndo niliongozana nao umbaLi mrefu sana kuna muda kama akili ilinijia nikawaambia subr niingie dukaNi nikala uchochoro nikawaacha wananisubiria kumbe nimepta uswahilini
 
Sijawai kutapeliwa....

Sample ya uo utapeli ulinikuta nikiwa kidato cha tano, nilienda town nkapewa Atm nyingi nkawatolee wana fedha,

Around twn katokea mtu nimwelekeze hospital ya macho, eti katongea Tanga ni n mgen, lakin lafidhi yake si ya Tanga, gafla katokea mtu anapajua eti niende nao, nkawaambia vizuri kwakua huyu anapajue mwambie akupeleke alafu mi huyo sijataka maelezo.....

Tapeli akiongea maneno 7 nshamjua
 
wanakupumbaza akili kwa madawa ya kienyeji ama technique wazijuazo wao na kukufanyia mazingaombwe ya kukutemesha kucha au nywele, huwa wanakua wawili mmoja anajifanya anauliza sehemu mwengine anajifanya mpita njia.

Mkasa wangu niliwahi kumsimulia mtu moja tu wa karibu sana, wengine huwa nadanganya kwamba "ilibaki kidogo nitapeliwe", "niliwatoroka", "nilijiongeza", n.k., hivi ni vichaka ambavyo watanzania wengi tunavikimbilia kukwepa aibu ya kuchekwa na kuonekana washamba ila kiuhalisia sio ushamba, haya mambo hata maprofesa wanaliwa timing wanaingia kingi ila wanapiga kimya, hata hao wanaocheka na kuwaona wenzao ni washamba nao wameshawahi kutapeliwa ila wanaficha ukweli.

huku jamiiforums kuna usiri kwa hio naweka mkasa mzima

Kilichonikuta mimi ni hiki :::

Ilikua mida ya mchana majira ya saa saba katika jiji mojawapo hapa nchini, niliondoka ofisini niende centre kwenye maduka kununua vifaa kwajili yakukamilisha kazi ya mteja, nilipofika centre nilishuka kwenye bajaji nikaanza kutambea kuelekea madukani, mbele hatua kadhaa nilikutana na mzee mmoja wa makamo mwenye umri Kama miaka 48 au zaidi na alikua amevalia tisheti nyeusi na suruali ya jinsi ya blue iliyopauka kwa kuchakaa.

alinifuata na kuniuliza "kijana hoteli ya wapemba unaifahamu? Mimi ni mgei katika hili jiji naomba unielekeze” kabla hajamaliza kuna mpita njia kijana alipita amesimama karibu yetu ni kama anataka kuvuka barabara, yule mzee akasema ngoja nimuulize huyu kijana, akamuuliza "samahani kijana hoteli ya wapemba unaifahamu? " yule mpita njia akamwamuonesha kwa kidole akiangalia upande wa mashariki akasema “hoteli ya wapemba iko tu pale”, akamwambia yule mzee “tuende kidogo hapo mbele nimuelekeze huyu (mimi) akupeleke manake mimi nawahi stendi kumpokea mtu"

tukaanza kutembea kuelekea huko na hata sijui niliwezaje maana nilienda centre kwa mambo mengine ila nikajikuta nafanya vingine, tukiwa njiani ili yule mzee akaanza kusema "Mimi nimetoka Morogoro natibu kwa kutumia kitabu, hata nyie nikiwaangalia tu viganja vyenu naweza kujua nyota zenu na matatizo yenu", yule mpita njia mwenzangu akamjibu" hebu tuangalizie", akamwangalia kiganjani alitikisa kichwa kwa masikitiko akasema kwa uchungu "wewe umehangaika sana hapa mjini lakini hujafanikiwa kwakua umelishwa kucha za maiti" jamaa alishtuka akawa kama amepanik hivi. ikafika zamu yangu nikampa kiganja akasema" wewe una nyota nzuri lakini umelishwa nywele za mtoto mchanga kuna mtu hapendi ufanikiwe zaidi ya hapa ulipo na pia nywele hizo zinakufanya usiwe na nguvu huwezi kuja kuzalisha mwanamke" niliingiwa na woga.

yule mpita njia akamwamba yule mzee “tusaidie kuondoa matatizo hayo mkuu" yule mzee akasema "mna kioo hapo?" tukajibu hapana akauliza mna karatasi nyeupe, yule mwenzangu akaitikia " ndio" akatoa karatasi mfukoni akampa akaishika kisha akasema " tafuneni hiyo karatasi” aliigawa vipande viwili, tukapokea na kuitafuna, akasema "haya kohoeni kwa nguvu" naam! sikuamini nachokiona nikakohoa nywele kidogo na mwenzangu akakohoa kucha, baada ya hapo mzee yule alionesha kukasirika akaongea kwa ukali" nimesema mkohoe kwa nguvu mmekohoa taratibu, nywele zimebaki tumboni na kucha Sasa mtakufa sijui niwasaidiaje” nilitetemeka kwa woga

Yule mzee alikuwa kama anatafuta mbinu ya kutusaida huku kashika kichwa, mimi hapo najuta hata kukutana nae yule mwengine anamuomba kila mara “mzee tusaide” , baada ya dakika 2 hivi akatuambia "sasa sikilizeni fuatani maelekezo nitakayowapa la sivyo mtakufa hapahapa” aliongea kwa msisitizo akaanza kutoa maelekezo " hizo nywele na kucha mlizotema inabidi muwahi kwenda kwenu mkazichome kwa manuizi ili mziyeyushe zilizobaki tumboni, mnavyozichoma wewe ulietema kucha nuia kucha zote zilimo tumboni ondoka na wewe wa nywele nuia nywele zote zilimo tumboni ondoka. “

tulitafuta karatasi pembezoni yule mpita njia alifungasha kucha zake na mimi nikafunhasha nywele nilizotema. Baada ya hapo yule mzee akatuambia tuweke kwenye mifuko ya suruali lakini kama hairusiwi mifuko mingine iwe imebeba chochote iwe ni ya suruali / jeans, shati au koti kwa hio tuvitoe vyote tulicyovibeba tuvifungie ndani ya rambo, kulikuwa na kijiduka kwa karibu yule mpita njia alienda kununua vimifuko viwili ni vile vikaki, yule mpita njia aliweka saa, pesa kama elf 70 hivi na simu mbili, mimi nikaweka pesa 138,000 na simu, tuliambiwa tuchukue pesa ya nauli tu, yule mpita njia alisema kwao sio mbali atatembea, mimi nilichukua buku ambayo ilikuwa ndogo katika hela nilizoweka. zile kaki mzee akatupa zikiwa zimekazwa na akatuambia "hii mifuko msithubutu kufungua mpaka mfike kwenu, mkifika kwenu muiweke pembeni, mchome kwanza hizo nywele na kucha huku mnanuia nilivyowaelekeza, baada ya hapo ndio mnaweza kuchukua vitu vyenu vya kwenye hio mifuko"

Yule mpita njia alisema anarudi kwao ambako ni karibu na ile hoteli aliyoulizia yule mzee kwahio wacha amsindikize kwanza mzee, mimi nikamuaga yule mzee na kumshukuru, mzee alinikumbusha kwamba nichome kwanza zile nywele ndio nifungue mfuko, nilifika stendi ya mabasi nikapanda usafiri nikarudi kwangu, nilipofika kitu cha kwanza nilichukua kiberiti nikaenda kuchoma kile kikaratasi nilichofungashia zile nywele, baada ya hapo sasa nikaenda kufungua kaki ili nitoe simu nicheki kama kuna missed call au message, daaah!!

Yani ndani ya bahasha nilikuta vipande vya maboksi vyenye ukubwa wa zile noti na nikaona kuna kimbao flani ukubwa kam wa simu, pamoja na uanaume huu nusu nipige ukunga aisee!! Nilikagua ile bahasha kama dakika 5 hivi siamini nachokiona, nilipaniki na kuchanganyikiwa nisijue cha kufanya kwa yaliyonikuta, nilirudi centre ile sehemu niliyowakuta nikazunguka sana mpaka kule eneo la tukio, nilikuwa nauliza watu wenye shughuli zao maeneo hayo kama wamewaona nikijaribu kuwaeleza walivyovaa na walivyo ila hakuna aliewaona, wengine nikiwauliza hata kabla sijamaliza wanajibu kwa mkato ,umeshapigwa!

Basi hayo ndiyo yaliyonikuta, nikisimulia wenzangu huwa nawadanganya kwamba nilijiongeza kiakili nilikataa kutoa pesa na simu nikaondoka nikaamua liwalo na liwe lakini ukweli bado naujua mimi mtendwa kwamba niliingizwa chaka.
Mtafute Monica wa UMUGHAKA akusaidie kuwapata wezi wako
 
Back
Top Bottom