Hivi Ndivyo Benki Hutumia Pesa Zako

Hivi Ndivyo Benki Hutumia Pesa Zako

bless on

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2026
Posts
882
Reaction score
2,129
Ukiweka Shilingi Milioni 10 benki leo, unaamini kuwa pesa hizo ziko ndani ya chumba cha siri cha benki zikikusubiri wewe ukazichukue siku yoyote, sivyo?

Ukweli ni kwamba: Pesa hizo hazipo hapo! Siku hiyo hiyo uliyoondoka, benki inachukua takriban Shilingi Milioni 8.5 hadi 9 na kuwakopesha watu wengine ili itengeneze faida ya riba.

Hiki ndicho kinachotokea pale kila mtu anapoamua kwenda kuchukua pesa zake kwa pamoja:

Pindi yanapoanza kuenea uvumi kuwa benki fulani inafilisika, wateja wote hukimbilia matawi ya benki au ATM kuchukua akiba zao.

Kwa sababu benki inahifadhi asilimia ndogo tu ya fedha taslimu (kwa mfano 10%), pesa za benki hiyo zitaisha ndani ya masaa machache tu! Mfano huu ulitokea kwenye kashfa ya Silicon Valley Bank (SVB) nchini Marekani na benki mbalimbali kwenye historia.

Namba unazoona kwenye App ya benki yako au kwenye SMS sio "fedha halisi" zilizopo kwenye chumba cha akiba. Ni ahadi ya kisheria kutoka kwa benki kuwa itakupa fedha hizo pindi unapozihitaji.

Ikiwa wateja wote watageuka na kuomba ahadi hiyo itekelezwe siku hiyo hiyo kwa Cash, mfumo wote unavunjika na bank itatangaza kufilisika na mtaishia kupewa pesa kidogo sana, mwenyewe milion 10 kwenye account ata ambulia labda milioni 2 hivi.

Kama mabenki yangehifadhi 100% ya pesa zote za wateja kwenye vyumba vyao vya siri:

Asingepatikana mtu yeyote wa kupewa mkopo wa kujenga nyumba, kununua gari, au kuanzisha biashara.

Mzunguko wa uchumi ungefanya kazi taratibu sana. Mfumo huu ndio unaiwezesha benki "kutengeneza fedha mpya" kupitia mikopo.

Ili kuzuia hofu serikali ziliunda mifumo miwili kuu:

Benki Kuu (mfano: BOT nchini Tanzania): yaani benki inayozikopesha benki zingine fedha taslimu za dharura pindi zinapozidiwa.

Bodi ya Bima ya Amana: Inayomhakikishia mwananchi kuwa hata benki ikifilisika leo, kuna kiwango cha chini cha fedha zake atakachorudishiwa na serikali.

Mfumo wa ubenki wa dunia haujengwi kwenye fedha taslimu pekee, bali unajengwa kwenye IMANI. Siku ambapo watu wote watapoteza imani na benki kwa wakati mmoja, mfumo wote wa kifedha wa dunia unasimama!
Watakao faidika ni wadaiwa wa mabenki.
 
Kuna sheria inayo govern kuanzishwa kwa bank yoyote.

Ili uanzishe bank lazima uwe na kiasi fulani cha pesa ukiweke BOT, incase bank imefilisika wateja wako walipwe pesa zao.

Mambo sio mepesi kama ulivyoandika hapo juu, kuweka pesa bank sio kama kucheza kamari.
 
Kuna sheria inayo govern kuanzishwa kwa bank yoyote.

Ili uanzishe bank lazima uwe na kiasi fulani cha pesa ukiweke BOT, incase bank imefilisika wateja wako walipwe pesa zao.

Mambo sio mepesi kama ulivyoandika hapo juu, kuweka pesa bank sio kama kucheza kamari.
Kwani nilichoelezea ni uongo?
 
Back
Top Bottom