Gavana wa BoT- Emmanuel Tutuba: Kiwango cha akiba yetu ya fedha za kigeni kinatosha uagizaji wa huduma na bidhaa kutoka nje kwa zaidi ya miezi 4.8

Gavana wa BoT- Emmanuel Tutuba: Kiwango cha akiba yetu ya fedha za kigeni kinatosha uagizaji wa huduma na bidhaa kutoka nje kwa zaidi ya miezi 4.8

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,943
Reaction score
2,982
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imebainisha kuwa kiwango cha akiba ya fedha za kigeni nchini kimeendelea kuimarika na kufikia uwezo wa kuagiza bidhaa na huduma kutoka nje kwa kipindi cha miezi 4.8, kiwango ambacho kiko juu ya matakwa ya kisheria ya nchi.

Hayo yameelezwa leo Juni 12, 2026, na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Emmanuel Tutuba, wakati akihutubia katika kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 tangu kuanzishwa kwa benki hiyo, yaliyofanyika kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

"kwa zaidi ya miaka 25 Benki Kuu imeendelea kujenga na kulinda akiba ya fedha za kigeni ikihakikisha uwepo wa uwezo mkubwa wa kuagiza bidhaa kutoka nje ya nchi kupitia huduma zilizopo kwa zaidi ya miezi minne. Kwa sasa, kiwango cha akiba yetu ya fedha za kigeni kinatosha uagizaji wa huduma na bidhaa kutoka nje kwa zaidi ya miezi 4.8, ikiwa ni juu ya kiwango kilichowekwa kisheria cha miezi minne."-Emmanuel Tutuba -Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania.

 
Back
Top Bottom