Hivi mhaya halisia anatokea wapi mkoa wa Kagera?

Hivi mhaya halisia anatokea wapi mkoa wa Kagera?

Ujinga wa kusema huyu kabila hili au lile bila hata kumpima DNA na kumjua baba yake halisi ni nani tunautoa wapi?

Unaweza kusema huyu Mhaya halisi kwa sababu ni wa ukoo wa Bakoba wa Bukoba wakati hata DNA test ya kumjua baba yake halisi hujafanya?

Na unaweza kulifanyia DNA test kabila zima? Vipi kama huyo anayesemwa baba wa kabila mama yake alifanya rough nje na hivyo si wa kabila hilo?

Kabila zima litakuwa ni hilo kabila tena?

Hayo maswali yako nakumbuka niliwahi kumwuliza mdada mmoja hivi wa Kizungu kwenye darasa la Person & Society pindi nikiwa college.

Kwamba, mtu unawezaje kusema au kujiita wewe ni mzungu halisi au mwafrika halisi ilhali hujui kwa uhakika down the line akina nani ni ancestors wako.

Manake unaweza kweli ukawa mweusi tii lakini down the line mmoja wa ancestors wako akawa ni mhindi au mwarabu ila wewe hujui tu. Hapo wewe uhalisi wa uafrika wako uko wapi?

So haya mambo ya uhalisi wa ukabila ni mambo ya kufikirika zaidi.

Wengi wetu naamini tumechanganyika mno ila tu hatujui.

Kila kabila hapa Africa ni mchanganyiko tofauti tofauti wa makabila, usije kujidanganya ukisema utapata kabila moja linalosimama peke yake, kwa kukusaidia japo kw Ufupi , mfano, watu wa bukoba na missenyi na bukoba vijijini wote ni kitu kimoja huwezi kupata tofauti kwa hawa , ukienda Muleba utakuta kuna tofauti kidogo sana katika lafudhi, ukienda karagwe pia Utakuta kuna tofauti kidogo katika lafudhi, japo wote wanasikilizana. Sasa hapa kuna tofauti za kimazingira katika watu hawa, naanzia mpakani mwa Tz na Ug, Mutukula ukitoka mpakani hadi sehemu inaitwa Igayaza, hapa wote ni wahaya lakini wanatumia lugha ya Kiganda kuliko hata kihaya, ukitoka igayaza hadi bunazi na kyaka utakuta wanazungunza kihaya pia na kiganda ni lugha ya kawaida kwao yaani huwezi kumteta kwa Kiganda, baada ya hapo utaenda hadi bukoba mjini ambako ni kihaya japo kiganda ni lugha ya kawaida. Unapotokea Mpaka wa Uganda (AKIKOMERA) Huu ni mpaka wa Uganda na Tz kwa upande wa Minziro ndani ya wilaya Missenyi, pia Minziro yote ni wahaya japo Kiganda kinatumika kuliko kihaya au kiswahili, baada ya hapo utakutana na vijiji vya Kakindo, Mabuye na Kassambya ambavyo hutumia kihaya japo kiganda huwateti chochote, hivyo Missenyi, Bukoba mjini na vijinini ni wahaya ambao mila , desturi na taratibu za Kiganda si ngeni japo kuna sehemu kama Igayaza, na Minziro kiganda kinatumika sana kuliko lugha yoyote japo ni wahaya na ni TZ. KARAGWE. hii pia ina wahaya lakini bado imechanganyika na watu wa Rwanda kwa upande wa sehemu za Kyanyamisa kuelekea Ngara, pia Sehemu za Mulongo zina Wanyankore ambao ni Waganda yaanu anakotokea Mseveni Kaguta, japo wahaya bado wako ila lafudhi ya watu wa Karagwe wa Eneo hili ni tafauti sana na ile ya Wahaya wa Bukoba na Missenyi ila bado wanasikilizana sana. Kiufupi mkoa wa Kagera umeathiriwa sana na nchi za jirani, mfano Waangaza wa wilaya ya Ngara Mkoani kagera wanasikilizana sana na Warundi na Wanyarwandwa kuliko watu wengine wa mkoa wa kagera. Mfn Mhaya na Mhangaza hawasikilizani kabisa kana kwamba Mhaya anasikilizana kwa urahisi na Muganda huku Mhangaza anamsikiliza sana Mrundi sana.

Sent using Jamii Forums mobile app

Wadau zangu kwa sasa nipo mkoa wa kagera nipo maeneo ya BUKOBA.

Katika huu mkoa siku zote najua wenyeji wa Mkuu mkoa ni WAHAYA

Lakini kinachonishangaza WAHAYA wenyewe kwa wenyewe wanabaguana maana nasikia kuna waziba, wanyaingiro, wanyambo, wahamba,waganda kyaka, wayoza

Nilipojaribu kuuzila nikaambiwa hawa...

Waziba wanatokea UGANDA

Wayoza wanatokea shinyanga kiasili ni wasukumaa

Wanyangiro hawa WAKO muleba ASILI yao nimeambiwa ni mchanganyiko wa mrundi na mnyarwanda pia kuna mhutu na mtusI Lakini pia naambiwa NI zao LA mjaluoo ndo maana rangi zao zinafanana

Wanyambo nasikia ni mchanganyiko wa muhutu na mtusi waliokimbia vita ya Rwanda mwaka 1959.

Mganda kyaka huyu nimeambiwa sio muhaya huyu anaitwa ni muhutu wa ugandaa.

Wahamba nasikia hawa ki ASILI NI wajaluo waliolowea muleba muda mrefu sana waka adapt UHAYA.

Jamani hadi sasa hebu tuambieni muhaya asilia anatokea wapi
Katika miaka ya arobaini, Tanganyika ilikuwa imegawanywa katika majimbo (provinces) 8, ambayo ni: Lake, Northern, Tanga, Eastern, Southern, Central, Western na Southern Highlands. Lake Province ilikuwa na wilaya (districts) 11, ambazo ni Mwanza, Bukoba, Biharamulo, Ngara, Shinyanga, Geita, Musoma, Kwimba, Maswa, Mara (ambayo sasa ni Tarime) na Ukerewe. Idadi hii ilikuja ikaongezeka mwaka 1956 wakati Karagwe ilipopewa hadhi ya wilaya. Kabla ya 1956, wilaya ya Bukoba ilijumuisha wilaya za sasa za Bukoba, Muleba, Missenyi, Karagwe na Kyerwa.

Wenyeji wake waliitwa na wakoloni Wahaya, ingawa baada ya kupata wilaya yao, baadhi ya wenyeji wa Karagwe walikataa kuitwa Wahaya. Akifafanua chanzo cha jina hilo, Mjerumani Stuhlmann aliandika mwaka 1899 kuwa lilikuwa ni jina la maeneo ya Mukama Kisebuka na Mukama Bwahama wa Kiamutwara, hasa yale yaliyo kwenye mwambao wa ziwa.

Wajerumani walipoona mila zetu na lugha zetu zinafanana wakaamua kutuita Wahaya. Hivyo jina Wahaya linajumuisha Bahyoza, Bahendangabo, Baziba, Bahamba, Banyaihangiro, Banyambo, Bakara na Babumbiro. Wakoloni waliwaunganisha Wahaya katika Buhaya Council iliyokuwa na makao makuu yake pale Rwamishenye.

Kiongozi wa secretariat yake aliyekuwa na umaarufu mkubwa alikuwa ni Omwami Francisco Xavier Rwamugira aliyejulikana kama Omukama wa mwenda. Kwa kuwa alikuwa Mziba, alisababisha watu wengine kuwachukia Waziba, kutokana na hisia kuwa Rwamugira alikuwa anapendelea watu wa Kiziba.

Kila moja ya makabila haya ilikuwa inatawaliwa na Mukama (king), na kila Bukama (kingdom) iligawanywa katika gombolola zilizokuwa zinaongozwa na abami (palatines). Kila gombolola ilikuwa na vijiji kadhaa vilivyoongozwa na abakungu. Kabla ya wakoloni kuja, Mukama alikuwa absolute ruler, kwa maana kwamba, neno lake lilikuwa ni sheria na ardhi yote ilikuwa ni mali yake.Kadhalika hata watu, mifugo na misitu vyote vilikuwa ni mali zake.

Kiziba ilikuwa na gombolola 8 ambazo ni: Kanyigo, Bwanja, Buyango, Gera, Bugandika, Kitobo, Ishozi na Kibumbiro. Wakati wa utoto wangu mwami wa Kanyigo alikuwa Omulangila Lukambaiga mtoto wa Omulangila Lushanzilana, mtoto wa Mukama Mutatembwa. Lukambaiga ndiye baba yake Omutemba Bernado wa Bugombe.

Mzungu wa kwanza kukanyaga Bukoba alikuwa ni Mjerumani Emin Pasha aliyewasili tarehe 31 Oktoba, 1890, ingawa miaka 30 kabla ya hapo Waingereza wawili, T.H. Speke na T.A Grant waliwahi kufika Karagwe na kukutana na Omukama Rumanyika l (Rugundu). Gavana wa kwanza wa kijerumani ni Julius von Soden (1891-1893) na wa mwisho ni Heinrich Schnee (1912-1916).

Gavana wa kwanza wa kiingereza ni Sir Horace Byatt (1916-1924) na wa mwisho ni Sir Richard Turnbull (1958-1961).

Sisi Bahaya (wakiwemo Banyambo) tunajulikana kama Western Interlacustrine Bantu. Tulihama kutoka Uganda Magharibi katika karne za 15 na 16, hasa kutoka Bunyoro na Ankole. Koo nyingi kama ule wa kwangu (abaziba/ababiito) asili yetu ni Bunyoro na chache kama abamiilo/abagabo asili yao ni Ankole.

Kihanja, Ihangiro na Bukara Bakama wao ni Bahinda wakati wale wa Kiamutwara na Bugabo ni Bankango waliowaasi Bahinda na kujitangazia uhuru yapata mwaka 1820 wakati Mukama Kalemera ll alipofariki. Uasi huu uliongozwa na Kitekere na baadaye kuimarishwa na mtoto wake Omukama Kaitaba (1860-1888). Bakama wa Kiziba ukoo wao ni Baziba/Babiito. Baada ya kifo cha Mukama Burungu ll (1800-1835) walipendelea kuitwa Abayobya. Sababu ni kwamba wanatokana na Omulangila Luyobya, mtoto wa Mukama Ruhangarazi l. Kutokana na ukatili uliopitiliza wa Burungu ll, baba yake mdogo, Omulangila Luyobya, alishindwa kumvumilia, na hivyo akaanzisha vita ya kumng’oa. Katika vita hii alisaidiwa sana na mtoto wake aliyeitwa Rutahilwa. Luyobya kwake kulikuwa ni Bukwali, Kanyigo.

Burungu ll alijikuta katika hali ngumu ya kushambuliwa kutoka ndani na nje, kwani Bahyoza walikuwa pia wanamshambulia. Baada ya Burungu kuuawa na maadui mwaka 1835, Rutahilwa, mtoto wa Ruyobya alitawala na akapewa jina Kibi ll. Baada ya Kibi ll, alitawala mtoto wake Rugangarazi ll (1858-1865), halafu Mutatembwa (1865-1903), halafu Mutahangarwa (1903-1916), halafu Mboneko ll (1916-1926), halafu Mutakubwa (1926-1937), halafu Lutinwa (1937-1974).

Mutakubwa aliondolewa na wakoloni mwaka 1937 na hakuwa na mtoto. Hivyo ndugu yake Mboneko aitwaye Nestor Lutinwa alichaguliwa kumrithi, na akatawala mpaka Nyerere alipofutilia mbali utawala wa Bakama.

Katika Kanyigo nzima mtu pekee aliyezaliwa wakati wa utawala wa Mutahangarwa amebaki mmoja tu, naye ni mzee Ta Baltholomayo wa Bugombe. Huyu kuzaliwa kwake ni datable kwani nilipomhoji aliniambia kuwa wakati Mutahangarwa anafariki alikuwa na umri wa kuanza shule wa watoto wa siku hizi.

Sababu ya kuondolewa kwa Mutakubwa ni ufuska uliokithiri, ukiwemo ule wa kulazimisha. Mama yake Muchureza alijaribu kumkanya lakini hakusikia. Hivyo alikwenda kumuomba DC wa kikoloni amsaidie kumkanya. Badala ya kumkanya DC alimfukuza, kwani kwa mzungu kubaka ni dhambi isiyosameheka. Lakini DC hakuelewa kuwa Mukama hawezi kuwa na hatia ya kumbaka mwanamke au kufanya uasherati, kwani kwa mila zetu wanawake wote ni mali ya Mukama. Hivyo watu wakawa wanamuimba Muchureza kuwa ni kilimi nyakwelega ayagambiile omujungu ati Omukama nasiyana. Maana yake, wimbo ulikuwa unamsuta Muchureza kwa kujichongea (okwelega) bila sababu ya msingi.

Mutakubwa, baada ya kufukuzwa, alimalizia maisha yake pale Kigarama, kwa Edward Kasano, kwani baba yake Edward alikuwa tumbo moja na Mutakubwa, wote wakiwa ni watoto wa Muchureza. Alifariki mwaka 1948 na kuzikwa pale Kigarama. Jambo la ajabu nililoshuhudia ni kwamba wazee pale kijijini waliendelea kumpa heshima kama Mukama wakimwamkia Habuka Izoba, Habuka Lugaba, Habuka Nyakusinga, nk.

Baadaye nilikuja kuelewa kuwa mtu akishasimikwa kama Mukama anakuwa na namna ya uungu (semi-divine). Hivyo ukimnyima heshima yake unaweza ukapatwa na mabaya.

Enock L. Kamuzora

If you know your enemy than yourself you shall never suffer a defeat

Watu wa kyamutwala na bugabo ndo wahaya asilia.

Ila tanzania mbona kila kabila inasemekana asili yake ni kutokea nje ya nchi ina maana Tanzania zamani haikuwa na watu?

Watu walikuwapo wakiwemo WAGOGO.

Ukifika Bukoba Mjini ndio utastaajabu.....!!

Hapa wapo Waswahili kama wale wanaopatikana jijini Dar, ukiwauliza asili watakuambia wametoka Kigoma, Tabora, Mwanza, Tanga n.k.

Ni wachache sana walio tokea Bukoba Vijijini...!

Sent using Jamii Forums mobile app
nilishangaa sana nilipofika kwa mara ya kwanza mkoa wa kagera na kutembelea wilaya zake za muleba na bukoba.

niliona baadhi ya wenyeji wa mkoa huo wenye ngozi nyeusi kama wajaluo lakini wameshika dini na wana imani kali kushinda hata sisi waswahili wa pwani ambako dini yetu ndio iliko anzia ikitokea mashariki ya kati.

Tukitaka kuulizana nani ni nani, Sijui asili yake wapi?nchi hii itabaki tupu

Ova

Hawa wako kama wachaga. Ukifika moshi kuna mkibosho, machame, mmarangu, kishumdu, old Moshi sasa hapo mchaga halisi niyupi. Kwahiyo hata wahaya nihivyo. Kuna kitu kinaitwa dialect kina leta mutual intelligebility katika hizi kabila. Navitu kama milima kama Kilimanjaro Na mto kagera vinasababisha haya yote. Tofauti nasehemu ambazo nitambalare kama Dodoma. Singida etc

Makabila mengi ya mipakakani yana michanganyiko,iko zaidi Kagera kwa sababu kumepakana na nchi tatu.Hapo kuna pia makabila ya wafugaji(walikuwa ni watu wa kuhamahama sana).Back in the days niliwahi kuuliza kama ulivyouliza,kuna eneo linaitwa 'Buhaya' ndio asili ya Wahaya original ndivyo nilivyojibiwa.

Sent using Jamii Forums mobile app

Kiamtwala na maeneo ya Bukala ndio sehemu ya mwanzo kabisa ya makazi ya Wahaya na ndio maana Mukama Lugomola alikuwa mkuu wa wakama enzi za wakama

Sent using Jamii Forums mobile app

Watu wa kyamutwala na bugabo ndo wahaya asilia.

Ila tanzania mbona kila kabila inasemekana asili yake ni kutokea nje ya nchi ina maana Tanzania zamani haikuwa na watu?
Ilikuwa pori tupu [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Aiseee....good research

Sent using Jamii Forums mobile app
Matango tupu..!

Kwanza mjaluo hawahi kuwa mbantu.

Pili tafuta kitabu kinaitwa interclustrine society back to 1000 years kitakusaidia, hao wanyaihangiro, wanyambo, wayoza ni sawa na kuchanganya makande na ubwabwa. Maana hapo kuna kabila na koo (wao huita oluganda) kumjua mhaya utajua ni mchanganyiko wa watusi(wafugaji/abalangira) na wahutu(wakulima na wafanyakazi hasa wachungaji wa ng'ombe za mhutu/watwana/bagabire)..!

Waingereza walilitunga kabila lao wao wakiwa wapi hao watungwaji? Zambia au waliwachukua watu wa nchi mbali mbali na kuwaunganisha na kutengeneza kabila moja??

Hapa naona umenipa mwanga kidogo wa kung'amua kitu.

Sent from my Siemens kidole juu using JamiiForum mobile app.
Hata kwa wahaya iko hivyo kila Mukama ktk utawala wake alikuwa na kabila lake ilikuwa makabila 8 lakini wajerumani walipo wakuta wale wa wavuvi wa ziwani= (wahaya) wakaunganisha abakama 8na kuteu kiongozi wao wote na kumuita mkama 9. Wanajua historia wanajua hilo.

Sent using Jamii Forums mobile app

Ukichunguza sana haitakosa.

Ukimsoma Dr. Thomas Molony aliyeandika kitabu cha "Nyerere:The Early Years" anayezungumzia miaka ya mwanzo ya Kambarage Nyerere, utaona kwamba kumbe hata Burito Nyerere, baba yake Kambarage Nyerere, hakuwa Chifu wa kurithi utawala kutoka kwa baba yake, alikuja kuwa Chifu baada ya watu kumkataa Chifu aliyekuwepo kabla kwa sababu ya migogoro.

Kwa hiyo kuna mambo machache ya kuzingatia hapa.

1. Wakoloni katika jitihada za kurahisisaha utawala wao, walitumia dhana ya "kabila" kutatua matatizo ya utawala kwa kuwagawanya watu katika makabila tofauti, mengine ambayo hayakuwa well defined na mengine ya kutunga tu ambayo hayakuwepo kabisa. Hapo utakutana na habari za "divide and rule".

2. Hata kabla ya utawala wa wakoloni, uhamaji hamaji wa makabila ya Kibantu hususan Africa katika miaka 2000 iliyopita, na zaidi katika miaka 300 iliyopita, umesababisha habari nzima ya "kabila pure" kuwa ni kitu kisichoyumkinika. Hii habari iko hata kwa makabila yasiyo ya kibantu. Peter Firstbrook katika kitabu chake cha historia ya familia ya Obama "The Obamas: The Untold Story of An African Family" kaonyesha jinsi uhamaji hamaji wa watu kutoka kaskazini ulivyokwenda mpaka kuja kuzaliwa Barack Obama. Leo hii kuna Wasukuma wamehama makazi kutoka Mwanza wamefika mpaka Ufipa na wengine wako Zambia wamejichanganya huko. Habari nzima ya "kabila pure" ni hadithi zaidi ya ukweli

bantumigration.jpg
Mchoraji wa hii ramani ana ukweli fulani kwa mfano Wanyakiusa pamoja na kwamba wako mbali na wahaya lakini utakuta baadhi ya mila maneno yanaingiliana moja kwa moja mpaka Namibia, Angola Zambia kwangu inanipa maana kwamba wote asili ni moja.

Sent using Jamii Forums mobile app

Bakoba mbona bado Wapo mpaka leo, jina la Bukoba linatokana na CRAN ya Abakoba lakini hilo alimaanishi ni kabila wanabaki ni Wahaya - tukija lafudhi ya kuzungumza Kihaya utakuta Wahendangabo(Bugabo), Wayoza(Kiamtwara) na Akabara(Maruku) lafudhi yao ni moja na maneno yote yanafanana i.e uwezi kuwatofautisha.
Lakini sisi tunajuana akiongea tu unajua huyu wa Bugabo, huyu wa Maruku.

Sent using Jamii Forums mobile app

Back
Top Bottom