Hivi mhaya halisia anatokea wapi mkoa wa Kagera?

Hii nchi haina mwenyewe...ni yetu wote tunaoishi humu
Ni yetu sote yes ila kutafuta root sio jambo baya kikubwa tusibaguane na kukejeliana....
Muumba wetu alisema "Nimewaumba tofauti tofauti ili mpate kujuana...." hapo utaona kua kumbe kujuana asili zetu sio dhambi bali ni kutaka kufahamiana zaidi.

Sent from my Siemens kidole juu using JamiiForum mobile app.
 
Makabila ya Africa yako fluid kuliko tunavyodhania.

Kuna Chifu mmoja wa kabila Zambia alihojiwa akasema kabila lao halikuwapo kabla ya kuja Waingereza.Waingereza walipokuja, wakalitunga tu hilo kabila kwa sababu ya kurahisisha administration. Wawaambia watu kuanzia leo nyinyi mtakuwa kabila fulani.

Kwa hiyo habari za makabila usizichukulie kama kuna mtu aliye wa kabila fulani "pure".

Hakuna kitu kama hicho.

Sent from my Kimulimuli
Waingereza walilitunga kabila lao wao wakiwa wapi hao watungwaji? Zambia au waliwachukua watu wa nchi mbali mbali na kuwaunganisha na kutengeneza kabila moja??

Hapa naona umenipa mwanga kidogo wa kung'amua kitu.

Sent from my Siemens kidole juu using JamiiForum mobile app.
 
Ni yetu sote yes ila kutafuta root sio jambo baya kikubwa tusibaguane na kukejeliana....
Muumba wetu alisema "Nimewaumba tofauti tofauti ili mpate kujuana...." hapo utaona kua kumbe kujuana asili zetu sio dhambi bali ni kutaka kufahamiana zaidi.

Sent from my Siemens kidole juu using JamiiForum mobile app.
Ni kweli,naunga mkono hoja,ila ninachokataa ni mtu kusema eti mimi ni mtanzania halisi kuliko wewe! Mimi nilishawahi kumuuliza babu kuhusu babu yake ikaonekana wamehama nchi zaidi ya moja...na katika kuhama huko unakuta,mababu walizaliwa watano,ila aliyefika Tanzania mmoja,mwingine yuko sudani,mwingine yuko kenya,mwingine yuko Drc etc.hapo unazungumzia miaka 200 nyuma.
 
Hujaelewa kitu hapa tunataka kujua kabla ya watu kuletwa utumwa na kuchanganyika je TANGANYIKA ilikua na watu wa aina gani???
coz kila anayeguswa anaonesha ni mhamiaji kama babu zako hapo ulivyoelezea sasa je ndio kusema Tanganyika kulikua pori tu hakuna watu au ilikuaje..... ndio tunataka kuwajua hasaaa watu hao ni akina nani??

Sent from my Siemens kidole juu using JamiiForum mobile app.
 
Waingereza walilitunga kabila lao wao wakiwa wapi hao watungwaji? Zambia au waliwachukua watu wa nchi mbali mbali na kuwaunganisha na kutengeneza kabila moja??

Hapa naona umenipa mwanga kidogo wa kung'amua kitu.

Sent from my Siemens kidole juu using JamiiForum mobile app.
Waingereza walienda Zambia. Wakawakuta Waafrika. Waafrika walikuwa wa kabila tofauti tofauti wana migogoro yao ya ardhi na mambo ya wakulima vs wafugaji kama tunavyojua. Katika kurahisisha utawala wao Waingereza, wakawachukua watu fulani kati ya hao waliokuwa wanagombana, wakawaambia nyinyi mtakuwa kabila jipya na Chifu wenu atakuwa huyu hapa.

Wakatunga kabila jipya kabisa ambalo halikuwepo kabla.

Na mpaka leo lipo.

Nilikuwa naangalia hapa kwenye maktaba yangu nipate kitabu nilichosoma habari hii na ukurasa, lakini naona miaka mingi imepita na nimekusanya vitabu vingi vya Africa na mpaka sasa nimeangalia index za vinne sijakiona hiki.

Shukrani sana bro Al Watan sasa naomba kujua kwa Tanganyika na wao walikumbwa na dhoruba kama ya Wazambia??

Sent from my Siemens kidole juu using JamiiForum mobile app.
 
Shukrani sana bro Al Watan sasa naomba kujua kwa Tanganyika na wao walikumbwa na dhoruba kama ya Wazambia??

Sent from my Siemens kidole juu using JamiiForum mobile app.
Ukichunguza sana haitakosa.

Ukimsoma Dr. Thomas Molony aliyeandika kitabu cha "Nyerere:The Early Years" anayezungumzia miaka ya mwanzo ya Kambarage Nyerere, utaona kwamba kumbe hata Burito Nyerere, baba yake Kambarage Nyerere, hakuwa Chifu wa kurithi utawala kutoka kwa baba yake, alikuja kuwa Chifu baada ya watu kumkataa Chifu aliyekuwepo kabla kwa sababu ya migogoro.

Kwa hiyo kuna mambo machache ya kuzingatia hapa.

1. Wakoloni katika jitihada za kurahisisaha utawala wao, walitumia dhana ya "kabila" kutatua matatizo ya utawala kwa kuwagawanya watu katika makabila tofauti, mengine ambayo hayakuwa well defined na mengine ya kutunga tu ambayo hayakuwepo kabisa. Hapo utakutana na habari za "divide and rule".

2. Hata kabla ya utawala wa wakoloni, uhamaji hamaji wa makabila ya Kibantu hususan Africa katika miaka 2000 iliyopita, na zaidi katika miaka 300 iliyopita, umesababisha habari nzima ya "kabila pure" kuwa ni kitu kisichoyumkinika. Hii habari iko hata kwa makabila yasiyo ya kibantu. Peter Firstbrook katika kitabu chake cha historia ya familia ya Obama "The Obamas: The Untold Story of An African Family" kaonyesha jinsi uhamaji hamaji wa watu kutoka kaskazini ulivyokwenda mpaka kuja kuzaliwa Barack Obama. Leo hii kuna Wasukuma wamehama makazi kutoka Mwanza wamefika mpaka Ufipa na wengine wako Zambia wamejichanganya huko. Habari nzima ya "kabila pure" ni hadithi zaidi ya ukweli

bantumigration.jpg
 
[emoji122] [emoji122] [emoji122] Shukrani sana kwa muda wako hakika umejitahidi sana kudadavua ungekua mwalimu wangu wa History ningepata A, Lol.... umekata kiu yangu sasa yaani hapa ndio umemaliza kila kitu.

Peace and Love.

Sent from my Siemens kidole juu using JamiiForum mobile app.
 
[emoji122] [emoji122] [emoji122] Shukrani sana kwa muda wako hakika umejitahidi sana kudadavua ungekua mwalimu wangu wa History ningepata A, Lol.... umekata kiu yangu sasa yaani hapa ndio umemaliza kila kitu.

Peace and Love.

Sent from my Siemens kidole juu using JamiiForum mobile app.
Shukurani na wewe kwa usikivu.

Umenirudisha kurejea mitabu yangu hapa.
 
Nijuavyo Waha asili yao ni Burundi hata wao wanajisema hivyo....ushawahi sikia kabila la WAGOMA???

Sent from my Siemens kidole juu using JamiiForum mobile app.
Wengi wana dhana hiyo lakini ukweli ni kinyume chake. Hakuna kabila la wagoma. Ukitaka kuyajua vizuri makabila ya eneo hili la Afrika mashariki kabla ya kuja wakoloni na agharabu kabla ya uhuru pitia kwenye link hii hapa: www.worldstatesmen.org/Tanzania_native.htlm Hapa utaweza kujua ukweli kuhusu makabila maarufu hapa Tanzania na chimbuko lake. Waha hawana asili ya Burundi ila kinyume chake ni kweli kwa kuwa hata mfalme wa kwanza wa Burundi asili yake ni Heru ambayo ni south Buha kingdom- Utawakuta kina Ndarichako humo.
 
Shukurani na wewe kwa usikivu.

Umenirudisha kurejea mitabu yangu hapa.
Hehehehehe nimefurahi kuona mtu katumia muda wake kwa ajili tu ya kunipa elimu.....
Nimefurahi sana hujui tu.

Sent from my Siemens kidole juu using JamiiForum mobile app.
 
Wengi wana dhana hiyo lakini ukweli ni kinyume chake. Hakuna kabila la wagoma. Ukitaka kuyajua vizuri makabila ya eneo hili la mashariki kabla ya kuja wakoloni na agharabu kabla ya uhuru pitia kwenye link hii hapa: www.worldstatesmen.org/Tanzania_native.htlm Hapa utaweza kujua ukweli kuhusu makabila maarufu hapa Tanzania na chimbuko lake. Waha hawana asili ya Burundi ila kinyume chake ni kweli kwa kuwa hata mfalme wa kwanza wa Burundi asili yake ni Heru ambayo ni south Buha kingdom- Utawakuta kina Ndarichako humo.
Ebwana eeeeh kuuumbe.... nitaipitia hiyo link....
shukrani sana kaka GwaB kwa muda wako wa kunielimisha.....[emoji120]

Sent from my Siemens kidole juu using JamiiForum mobile app.
 
Ebwana eeeeh kuuumbe.... nitaipitia hiyo link....
shukrani sana kaka GwaB kwa muda wako wa kunielimisha.....[emoji120]

Sent from my Siemens kidole juu using JamiiForum mobile app.
Karibu sana mkuu,Upatapo muda chungulia na hii PDF ina mengi unaweza kujifunza kuhusu makabila ya kibantu.
 
Attachments

Karibu sana mkuu,Upatapo muda chungulia na hii PDF ina mengi unaweza kujifunza kuhusu makabila ya kibantu.
Shukran sana.... nimeisave mahali salama.... nitaipitia kurasa moja baada ya nyingine.

Back
Top Bottom