Hivi mhaya halisia anatokea wapi mkoa wa Kagera?

Hivi mhaya halisia anatokea wapi mkoa wa Kagera?

Katika miaka ya arobaini, Tanganyika ilikuwa imegawanywa katika majimbo (provinces) 8, ambayo ni: Lake, Northern, Tanga, Eastern, Southern, Central, Western na Southern Highlands. Lake Province ilikuwa na wilaya (districts) 11, ambazo ni Mwanza, Bukoba, Biharamulo, Ngara, Shinyanga, Geita, Musoma, Kwimba, Maswa, Mara (ambayo sasa ni Tarime) na Ukerewe. Idadi hii ilikuja ikaongezeka mwaka 1956 wakati Karagwe ilipopewa hadhi ya wilaya. Kabla ya 1956, wilaya ya Bukoba ilijumuisha wilaya za sasa za Bukoba, Muleba, Missenyi, Karagwe na Kyerwa.

Wenyeji wake waliitwa na wakoloni Wahaya, ingawa baada ya kupata wilaya yao, baadhi ya wenyeji wa Karagwe walikataa kuitwa Wahaya. Akifafanua chanzo cha jina hilo, Mjerumani Stuhlmann aliandika mwaka 1899 kuwa lilikuwa ni jina la maeneo ya Mukama Kisebuka na Mukama Bwahama wa Kiamutwara, hasa yale yaliyo kwenye mwambao wa ziwa.

Wajerumani walipoona mila zetu na lugha zetu zinafanana wakaamua kutuita Wahaya. Hivyo jina Wahaya linajumuisha Bahyoza, Bahendangabo, Baziba, Bahamba, Banyaihangiro, Banyambo, Bakara na Babumbiro. Wakoloni waliwaunganisha Wahaya katika Buhaya Council iliyokuwa na makao makuu yake pale Rwamishenye.

Kiongozi wa secretariat yake aliyekuwa na umaarufu mkubwa alikuwa ni Omwami Francisco Xavier Rwamugira aliyejulikana kama Omukama wa mwenda. Kwa kuwa alikuwa Mziba, alisababisha watu wengine kuwachukia Waziba, kutokana na hisia kuwa Rwamugira alikuwa anapendelea watu wa Kiziba.

Kila moja ya makabila haya ilikuwa inatawaliwa na Mukama (king), na kila Bukama (kingdom) iligawanywa katika gombolola zilizokuwa zinaongozwa na abami (palatines). Kila gombolola ilikuwa na vijiji kadhaa vilivyoongozwa na abakungu. Kabla ya wakoloni kuja, Mukama alikuwa absolute ruler, kwa maana kwamba, neno lake lilikuwa ni sheria na ardhi yote ilikuwa ni mali yake.Kadhalika hata watu, mifugo na misitu vyote vilikuwa ni mali zake.

Kiziba ilikuwa na gombolola 8 ambazo ni: Kanyigo, Bwanja, Buyango, Gera, Bugandika, Kitobo, Ishozi na Kibumbiro. Wakati wa utoto wangu mwami wa Kanyigo alikuwa Omulangila Lukambaiga mtoto wa Omulangila Lushanzilana, mtoto wa Mukama Mutatembwa. Lukambaiga ndiye baba yake Omutemba Bernado wa Bugombe.

Mzungu wa kwanza kukanyaga Bukoba alikuwa ni Mjerumani Emin Pasha aliyewasili tarehe 31 Oktoba, 1890, ingawa miaka 30 kabla ya hapo Waingereza wawili, T.H. Speke na T.A Grant waliwahi kufika Karagwe na kukutana na Omukama Rumanyika l (Rugundu). Gavana wa kwanza wa kijerumani ni Julius von Soden (1891-1893) na wa mwisho ni Heinrich Schnee (1912-1916).

Gavana wa kwanza wa kiingereza ni Sir Horace Byatt (1916-1924) na wa mwisho ni Sir Richard Turnbull (1958-1961).

Sisi Bahaya (wakiwemo Banyambo) tunajulikana kama Western Interlacustrine Bantu. Tulihama kutoka Uganda Magharibi katika karne za 15 na 16, hasa kutoka Bunyoro na Ankole. Koo nyingi kama ule wa kwangu (abaziba/ababiito) asili yetu ni Bunyoro na chache kama abamiilo/abagabo asili yao ni Ankole.

Kihanja, Ihangiro na Bukara Bakama wao ni Bahinda wakati wale wa Kiamutwara na Bugabo ni Bankango waliowaasi Bahinda na kujitangazia uhuru yapata mwaka 1820 wakati Mukama Kalemera ll alipofariki. Uasi huu uliongozwa na Kitekere na baadaye kuimarishwa na mtoto wake Omukama Kaitaba (1860-1888). Bakama wa Kiziba ukoo wao ni Baziba/Babiito. Baada ya kifo cha Mukama Burungu ll (1800-1835) walipendelea kuitwa Abayobya. Sababu ni kwamba wanatokana na Omulangila Luyobya, mtoto wa Mukama Ruhangarazi l. Kutokana na ukatili uliopitiliza wa Burungu ll, baba yake mdogo, Omulangila Luyobya, alishindwa kumvumilia, na hivyo akaanzisha vita ya kumng’oa. Katika vita hii alisaidiwa sana na mtoto wake aliyeitwa Rutahilwa. Luyobya kwake kulikuwa ni Bukwali, Kanyigo.

Burungu ll alijikuta katika hali ngumu ya kushambuliwa kutoka ndani na nje, kwani Bahyoza walikuwa pia wanamshambulia. Baada ya Burungu kuuawa na maadui mwaka 1835, Rutahilwa, mtoto wa Ruyobya alitawala na akapewa jina Kibi ll. Baada ya Kibi ll, alitawala mtoto wake Rugangarazi ll (1858-1865), halafu Mutatembwa (1865-1903), halafu Mutahangarwa (1903-1916), halafu Mboneko ll (1916-1926), halafu Mutakubwa (1926-1937), halafu Lutinwa (1937-1974).

Mutakubwa aliondolewa na wakoloni mwaka 1937 na hakuwa na mtoto. Hivyo ndugu yake Mboneko aitwaye Nestor Lutinwa alichaguliwa kumrithi, na akatawala mpaka Nyerere alipofutilia mbali utawala wa Bakama.

Katika Kanyigo nzima mtu pekee aliyezaliwa wakati wa utawala wa Mutahangarwa amebaki mmoja tu, naye ni mzee Ta Baltholomayo wa Bugombe. Huyu kuzaliwa kwake ni datable kwani nilipomhoji aliniambia kuwa wakati Mutahangarwa anafariki alikuwa na umri wa kuanza shule wa watoto wa siku hizi.

Sababu ya kuondolewa kwa Mutakubwa ni ufuska uliokithiri, ukiwemo ule wa kulazimisha. Mama yake Muchureza alijaribu kumkanya lakini hakusikia. Hivyo alikwenda kumuomba DC wa kikoloni amsaidie kumkanya. Badala ya kumkanya DC alimfukuza, kwani kwa mzungu kubaka ni dhambi isiyosameheka. Lakini DC hakuelewa kuwa Mukama hawezi kuwa na hatia ya kumbaka mwanamke au kufanya uasherati, kwani kwa mila zetu wanawake wote ni mali ya Mukama. Hivyo watu wakawa wanamuimba Muchureza kuwa ni kilimi nyakwelega ayagambiile omujungu ati Omukama nasiyana. Maana yake, wimbo ulikuwa unamsuta Muchureza kwa kujichongea (okwelega) bila sababu ya msingi.

Mutakubwa, baada ya kufukuzwa, alimalizia maisha yake pale Kigarama, kwa Edward Kasano, kwani baba yake Edward alikuwa tumbo moja na Mutakubwa, wote wakiwa ni watoto wa Muchureza. Alifariki mwaka 1948 na kuzikwa pale Kigarama. Jambo la ajabu nililoshuhudia ni kwamba wazee pale kijijini waliendelea kumpa heshima kama Mukama wakimwamkia Habuka Izoba, Habuka Lugaba, Habuka Nyakusinga, nk.

Baadaye nilikuja kuelewa kuwa mtu akishasimikwa kama Mukama anakuwa na namna ya uungu (semi-divine). Hivyo ukimnyima heshima yake unaweza ukapatwa na mabaya.

Enock L. Kamuzora

If you know your enemy than yourself you shall never suffer a defeat
historia ndefu sana ila chenga nyingi sana. references zoote za mzungu. adui anakujua kuliko unavyojijua kweli?,
fanya research utawajua kupitia wahusika na wana historia tofauti na za hao waliopotosha kweli yetu

Hakuna kabila inaitwa Wahaya. Wahaya ni jumuishi ya kabila zilizopo Kagera. Wahaya ni watu wenye asili ya visiwani na pembezoni mwa ziwa victoria wenye shughuli ya uvuvi tu japo nao wana makabila yao.
Jina WAHAYA ilitokana n la shughuli ya uvuvi. Neno Wahaya imetoholewa au kuzaliwa kutoka neno Okuhaaya.
OKUHAAYA no kitendo cha uvuaji samaki na kwa asili mfano ya kwetu Kiziba ambapo wanatoka walangira watwale nk hawakutumia kabisa Samaki kitu ambacho wao ni wahiima( wahiima asili yao ni wafugaji na uwindaji). waziba kwa asili na tamaduni walidharau sana vitokanavyo majini na hawakutumia kabisa Samaki. hii ni sababu kuu ya lujitanabaisha baina yao na watu wengine waitwao wahaya kwakua hawaku haaya. ufugaji na uvuvi ni matabaka mawili tofauti ifahamike hivyo.
Hivyo ukiondoa wanyambo Waziba nao sio wahaya. hivyo basi wahaya ni jamii ya wahyoza(Kyamutwara Empire) wakoba kwa ujumla wao(wenye Bukoba) abagabo (wenyeji wa Bugabo)jamii ipatikanayo Maruku na wanyaihyangiro(kutoka Muleba) hawa ndio wenye stahiki wa jina WAHAYA hivyo wasubi, waziba, wanyambo, wahangaza sio wahaya.

Mchoraji wa hii ramani ana ukweli fulani kwa mfano Wanyakiusa pamoja na kwamba wako mbali na wahaya lakini utakuta baadhi ya mila maneno yanaingiliana moja kwa moja mpaka Namibia, Angola Zambia kwangu inanipa maana kwamba wote asili ni moja.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nikujumbushe wanyakyusa wapo pande mbili. Mnyakyusa Mchele na Ndizi Mnyakyusa ndizi ni jamii kamili ya wanyambo, waziba. Historia inaanzia miaka ya 1460 baada ya watoto wa King Agaba wa Bunyoro Kitara kusambazwa ulinwenguni baada ya kuhofia kupinduliwa na watoto wake wakiume. kila mtoto alielejezwa na forerellers wapo pa kwenda na mazingira ya mfanano yenye kukubali Ndizi na mtama. hivyo walitokea Bunyoro kwends Mbeya na hii inatupa ukaribu wao kiasili.

Hayo maswali yako nakumbuka niliwahi kumwuliza mdada mmoja hivi wa Kizungu kwenye darasa la Person & Society pindi nikiwa college.

Kwamba, mtu unawezaje kusema au kujiita wewe ni mzungu halisi au mwafrika halisi ilhali hujui kwa uhakika down the line akina nani ni ancestors wako.

Manake unaweza kweli ukawa mweusi tii lakini down the line mmoja wa ancestors wako akawa ni mhindi au mwarabu ila wewe hujui tu. Hapo wewe uhalisi wa uafrika wako uko wapi?

So haya mambo ya uhalisi wa ukabila ni mambo ya kufikirika zaidi.

Wengi wetu naamini tumechanganyika mno ila tu hatujui.
hujataka kujijua. mambo yote yapo wazi hayajifichi

Ujinga wa kusema huyu kabila hili au lile bila hata kumpima DNA na kumjua baba yake halisi ni nani tunautoa wapi?

Unaweza kusema huyu Mhaya halisi kwa sababu ni wa ukoo wa Bakoba wa Bukoba wakati hata DNA test ya kumjua baba yake halisi hujafanya?

Na unaweza kulifanyia DNA test kabila zima? Vipi kama huyo anayesemwa baba wa kabila mama yake alifanya rough nje na hivyo si wa kabila hilo?

Kabila zima litakuwa ni hilo kabila tena?
Huhitaji DNA kujitambua. kuna inherited elements nyingi tu hazijifichi.

wazee wetu hawakukosea na mtoto ambae hakua wa ndani alijulikana tangu mimba wengine kuzaliwa kwake tu.

Japo wambebesha mama jukumu la kuwa DNA tester wako sio lazima. watoto wa mitaani walitupwa wakiwa wadogo na hushia kujua asili zao wengi tu.

Nachelea kusema hujataka kuitafuta. Nothing stays hidden forever

Back
Top Bottom