Hivi mhaya halisia anatokea wapi mkoa wa Kagera?

Hivi mhaya halisia anatokea wapi mkoa wa Kagera?

Mchoraji wa hii ramani ana ukweli fulani kwa mfano Wanyakiusa pamoja na kwamba wako mbali na wahaya lakini utakuta baadhi ya mila maneno yanaingiliana moja kwa moja mpaka Namibia, Angola Zambia kwangu inanipa maana kwamba wote asili ni moja.

Sent using Jamii Forums mobile app
Upo right kabisa.... kumbe hawa wazungu ndio walikuja kutuchanganya changanya huku jamaniiii

Hivi na wao wana makabila kama sisi huku???

Sent from my Siemens kidole juu using JamiiForum mobile app.
 
Shukrani sana bro Al Watan sasa naomba kujua kwa Tanganyika na wao walikumbwa na dhoruba kama ya Wazambia??

Sent from my Siemens kidole juu using JamiiForum mobile app.
Makabila mengi yalipewa majina na watu wengine mfano wahehe hakukuwa na kabila linaitwa wahehe bali ilikuwa mtu akiongea nao wanasema He he He yaani kwenye maongezi he he zilikuwa nyingi watu wakawaita wahehe. Swali kabla ya kuitwa wa hehe walikuwa kabila gani?
 
Makabila mengi yalipewa majina na watu wengine mfano wahehe hakukuwa na kabila linaitwa wahehe bali ilikuwa mtu akiongea nao wanasema He he He yaani kwenye maongezi he he zilikuwa nyingi watu wakawaita wahehe. Swali kabla ya kuitwa wa hehe walikuwa kabila gani?
Hehehehehe hiyo kali sasa, wewe Yehodaya sio unanipiga fix mchana kweupe wewe sikuamini amini ujue[emoji23] [emoji23] [emoji23]

Itakua kabla ya hehehe walikua wanacheka hahaha so kabila lao lilikua wahaha kabla hawajaamua kubadili swaggs za vicheko.

Lol.

Sent from my Siemens kidole juu using JamiiForum mobile app.
 
Hawa wako kama wachaga. Ukifika moshi kuna mkibosho, machame, mmarangu, kishumdu, old Moshi sasa hapo mchaga halisi niyupi. Kwahiyo hata wahaya nihivyo. Kuna kitu kinaitwa dialect kina leta mutual intelligebility katika hizi kabila. Navitu kama milima kama Kilimanjaro Na mto kagera vinasababisha haya yote. Tofauti nasehemu ambazo nitambalare kama Dodoma. Singida etc
Inasemekana mchaga halisi ni mu uru kwa sababu wao ndio wapo ktk ya mji wa moshi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tulikatazwa na Mwalimu kujadili makabila..
 
Kimsingi hakuna kabila la Wahaya.Wahaya ni muunganiko wa makabila mengi km ulivyoyataja. Swala la asili ya kila kabila km ulivyoyataja hilo linahitaji taaluma na tafiti, siyo kwa wepesi unaodhania.

Kila kundi lilokuwa na mfalme/ Omukakama lilikuwa ni kabila kamili. Bukoba kulikuwa na abakama wengi na hivyo kuwa na makabila mengi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Never,
 
Siku wakiparaganyika kabila la wahaya litapotea.
tutakuwa na makabila yafustayo
Wahamba
wanyaiyangiro.
wayoza
wanyambo
waziba
wagandakyaka
Hakuna kabila ya waganda kyaka kama hujui uliza missenyi wanaitwa babumbilo.
 
Wahaya wako muleba missenyi na bukoba na karagwe sema tofauti inakuja kwenye rafudhi wote wanaongea kihaya ila rafudhi tofauti kama ulivyotaja apo juu kama unavyoona Tanzania mikoa yote inazungumza kiswahili ila kwa rafudhi tofauti
Wahaya hawapatikani Karagwe labda wahamiaji wa Karagwe, Karagwe ni ya Wanyambo
 
Wadau zangu kwa sasa nipo mkoa wa kagera nipo maeneo ya BUKOBA.

Katika huu mkoa siku zote najua wenyeji wa Mkuu mkoa ni WAHAYA

Lakini kinachonishangaza WAHAYA wenyewe kwa wenyewe wanabaguana maana nasikia kuna waziba, wanyaingiro, wanyambo, wahamba,waganda kyaka, wayoza

Nilipojaribu kuuzila nikaambiwa hawa...

Waziba wanatokea UGANDA

Wayoza wanatokea shinyanga kiasili ni wasukumaa

Wanyangiro hawa WAKO muleba ASILI yao nimeambiwa ni mchanganyiko wa mrundi na mnyarwanda pia kuna mhutu na mtusI Lakini pia naambiwa NI zao LA mjaluoo ndo maana rangi zao zinafanana

Wanyambo nasikia ni mchanganyiko wa muhutu na mtusi waliokimbia vita ya Rwanda mwaka 1959.

Mganda kyaka huyu nimeambiwa sio muhaya huyu anaitwa ni muhutu wa ugandaa.

Wahamba nasikia hawa ki ASILI NI wajaluo waliolowea muleba muda mrefu sana waka adapt UHAYA.

Jamani hadi sasa hebu tuambieni muhaya asilia anatokea wapi
Kagera wapi wahaya og wapo Uganda

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Simulizi kama hizi ni vizuri ikaandikwa kwenye kitabu ili historia hii isipotee.
Katika miaka ya arobaini, Tanganyika ilikuwa imegawanywa katika majimbo (provinces) 8, ambayo ni: Lake, Northern, Tanga, Eastern, Southern, Central, Western na Southern Highlands. Lake Province ilikuwa na wilaya (districts) 11, ambazo ni Mwanza, Bukoba, Biharamulo, Ngara, Shinyanga, Geita, Musoma, Kwimba, Maswa, Mara (ambayo sasa ni Tarime) na Ukerewe. Idadi hii ilikuja ikaongezeka mwaka 1956 wakati Karagwe ilipopewa hadhi ya wilaya. Kabla ya 1956, wilaya ya Bukoba ilijumuisha wilaya za sasa za Bukoba, Muleba, Missenyi, Karagwe na Kyerwa.

Wenyeji wake waliitwa na wakoloni Wahaya, ingawa baada ya kupata wilaya yao, baadhi ya wenyeji wa Karagwe walikataa kuitwa Wahaya. Akifafanua chanzo cha jina hilo, Mjerumani Stuhlmann aliandika mwaka 1899 kuwa lilikuwa ni jina la maeneo ya Mukama Kisebuka na Mukama Bwahama wa Kiamutwara, hasa yale yaliyo kwenye mwambao wa ziwa.

Wajerumani walipoona mila zetu na lugha zetu zinafanana wakaamua kutuita Wahaya. Hivyo jina Wahaya linajumuisha Bahyoza, Bahendangabo, Baziba, Bahamba, Banyaihangiro, Banyambo, Bakara na Babumbiro. Wakoloni waliwaunganisha Wahaya katika Buhaya Council iliyokuwa na makao makuu yake pale Rwamishenye.

Kiongozi wa secretariat yake aliyekuwa na umaarufu mkubwa alikuwa ni Omwami Francisco Xavier Rwamugira aliyejulikana kama Omukama wa mwenda. Kwa kuwa alikuwa Mziba, alisababisha watu wengine kuwachukia Waziba, kutokana na hisia kuwa Rwamugira alikuwa anapendelea watu wa Kiziba.

Kila moja ya makabila haya ilikuwa inatawaliwa na Mukama (king), na kila Bukama (kingdom) iligawanywa katika gombolola zilizokuwa zinaongozwa na abami (palatines). Kila gombolola ilikuwa na vijiji kadhaa vilivyoongozwa na abakungu. Kabla ya wakoloni kuja, Mukama alikuwa absolute ruler, kwa maana kwamba, neno lake lilikuwa ni sheria na ardhi yote ilikuwa ni mali yake.Kadhalika hata watu, mifugo na misitu vyote vilikuwa ni mali zake.

Kiziba ilikuwa na gombolola 8 ambazo ni: Kanyigo, Bwanja, Buyango, Gera, Bugandika, Kitobo, Ishozi na Kibumbiro. Wakati wa utoto wangu mwami wa Kanyigo alikuwa Omulangila Lukambaiga mtoto wa Omulangila Lushanzilana, mtoto wa Mukama Mutatembwa. Lukambaiga ndiye baba yake Omutemba Bernado wa Bugombe.

Mzungu wa kwanza kukanyaga Bukoba alikuwa ni Mjerumani Emin Pasha aliyewasili tarehe 31 Oktoba, 1890, ingawa miaka 30 kabla ya hapo Waingereza wawili, T.H. Speke na T.A Grant waliwahi kufika Karagwe na kukutana na Omukama Rumanyika l (Rugundu). Gavana wa kwanza wa kijerumani ni Julius von Soden (1891-1893) na wa mwisho ni Heinrich Schnee (1912-1916).

Gavana wa kwanza wa kiingereza ni Sir Horace Byatt (1916-1924) na wa mwisho ni Sir Richard Turnbull (1958-1961).

Sisi Bahaya (wakiwemo Banyambo) tunajulikana kama Western Interlacustrine Bantu. Tulihama kutoka Uganda Magharibi katika karne za 15 na 16, hasa kutoka Bunyoro na Ankole. Koo nyingi kama ule wa kwangu (abaziba/ababiito) asili yetu ni Bunyoro na chache kama abamiilo/abagabo asili yao ni Ankole.

Kihanja, Ihangiro na Bukara Bakama wao ni Bahinda wakati wale wa Kiamutwara na Bugabo ni Bankango waliowaasi Bahinda na kujitangazia uhuru yapata mwaka 1820 wakati Mukama Kalemera ll alipofariki. Uasi huu uliongozwa na Kitekere na baadaye kuimarishwa na mtoto wake Omukama Kaitaba (1860-1888). Bakama wa Kiziba ukoo wao ni Baziba/Babiito. Baada ya kifo cha Mukama Burungu ll (1800-1835) walipendelea kuitwa Abayobya. Sababu ni kwamba wanatokana na Omulangila Luyobya, mtoto wa Mukama Ruhangarazi l. Kutokana na ukatili uliopitiliza wa Burungu ll, baba yake mdogo, Omulangila Luyobya, alishindwa kumvumilia, na hivyo akaanzisha vita ya kumng’oa. Katika vita hii alisaidiwa sana na mtoto wake aliyeitwa Rutahilwa. Luyobya kwake kulikuwa ni Bukwali, Kanyigo.

Burungu ll alijikuta katika hali ngumu ya kushambuliwa kutoka ndani na nje, kwani Bahyoza walikuwa pia wanamshambulia. Baada ya Burungu kuuawa na maadui mwaka 1835, Rutahilwa, mtoto wa Ruyobya alitawala na akapewa jina Kibi ll. Baada ya Kibi ll, alitawala mtoto wake Rugangarazi ll (1858-1865), halafu Mutatembwa (1865-1903), halafu Mutahangarwa (1903-1916), halafu Mboneko ll (1916-1926), halafu Mutakubwa (1926-1937), halafu Lutinwa (1937-1974).

Mutakubwa aliondolewa na wakoloni mwaka 1937 na hakuwa na mtoto. Hivyo ndugu yake Mboneko aitwaye Nestor Lutinwa alichaguliwa kumrithi, na akatawala mpaka Nyerere alipofutilia mbali utawala wa Bakama.

Katika Kanyigo nzima mtu pekee aliyezaliwa wakati wa utawala wa Mutahangarwa amebaki mmoja tu, naye ni mzee Ta Baltholomayo wa Bugombe. Huyu kuzaliwa kwake ni datable kwani nilipomhoji aliniambia kuwa wakati Mutahangarwa anafariki alikuwa na umri wa kuanza shule wa watoto wa siku hizi.

Sababu ya kuondolewa kwa Mutakubwa ni ufuska uliokithiri, ukiwemo ule wa kulazimisha. Mama yake Muchureza alijaribu kumkanya lakini hakusikia. Hivyo alikwenda kumuomba DC wa kikoloni amsaidie kumkanya. Badala ya kumkanya DC alimfukuza, kwani kwa mzungu kubaka ni dhambi isiyosameheka. Lakini DC hakuelewa kuwa Mukama hawezi kuwa na hatia ya kumbaka mwanamke au kufanya uasherati, kwani kwa mila zetu wanawake wote ni mali ya Mukama. Hivyo watu wakawa wanamuimba Muchureza kuwa ni kilimi nyakwelega ayagambiile omujungu ati Omukama nasiyana. Maana yake, wimbo ulikuwa unamsuta Muchureza kwa kujichongea (okwelega) bila sababu ya msingi.

Mutakubwa, baada ya kufukuzwa, alimalizia maisha yake pale Kigarama, kwa Edward Kasano, kwani baba yake Edward alikuwa tumbo moja na Mutakubwa, wote wakiwa ni watoto wa Muchureza. Alifariki mwaka 1948 na kuzikwa pale Kigarama. Jambo la ajabu nililoshuhudia ni kwamba wazee pale kijijini waliendelea kumpa heshima kama Mukama wakimwamkia Habuka Izoba, Habuka Lugaba, Habuka Nyakusinga, nk.

Baadaye nilikuja kuelewa kuwa mtu akishasimikwa kama Mukama anakuwa na namna ya uungu (semi-divine). Hivyo ukimnyima heshima yake unaweza ukapatwa na mabaya.

Enock L. Kamuzora

If you know your enemy than yourself you shall never suffer a defeat

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wadau zangu kwa sasa nipo mkoa wa kagera nipo maeneo ya BUKOBA.

Katika huu mkoa siku zote najua wenyeji wa Mkuu mkoa ni WAHAYA

Lakini kinachonishangaza WAHAYA wenyewe kwa wenyewe wanabaguana maana nasikia kuna waziba, wanyaingiro, wanyambo, wahamba,waganda kyaka, wayoza

Nilipojaribu kuuzila nikaambiwa hawa...

Waziba wanatokea UGANDA

Wayoza wanatokea shinyanga kiasili ni wasukumaa

Wanyangiro hawa WAKO muleba ASILI yao nimeambiwa ni mchanganyiko wa mrundi na mnyarwanda pia kuna mhutu na mtusI Lakini pia naambiwa NI zao LA mjaluoo ndo maana rangi zao zinafanana

Wanyambo nasikia ni mchanganyiko wa muhutu na mtusi waliokimbia vita ya Rwanda mwaka 1959.

Mganda kyaka huyu nimeambiwa sio muhaya huyu anaitwa ni muhutu wa ugandaa.

Wahamba nasikia hawa ki ASILI NI wajaluo waliolowea muleba muda mrefu sana waka adapt UHAYA.

Jamani hadi sasa hebu tuambieni muhaya asilia anatokea wapi
Mkuu kwa tabia ya Wahaya ni ngumu sana kujua kabila halisi la mtu wa Bukoba bali mama ndiyo anaweza jua kabila la mwanae kutokana na mme aliyempa mimba.

Nadhani umenipata.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Conclusion, itambulike wahaya ni kabila lengine na wanyambo n kabila lengine pia habari za kuwa mnatuuliza et we dada unatokea mkoa gani nakwambia kagera unasema et ooh mbona hamna wahaya weupe inakuaje uko hvo,sasa ni hvi sisi n wanyambo,na wahaya wanajijua wenyewe
 
Back
Top Bottom