Hivi mhaya halisia anatokea wapi mkoa wa Kagera?

Hivi mhaya halisia anatokea wapi mkoa wa Kagera?

Wenyeji wa Kigoma ni Waha. Neno waha maana yake watu wa hapa hapa.
Nijuavyo Waha asili yao ni Burundi hata wao wanajisema hivyo....ushawahi sikia kabila la WAGOMA???

Sent from my Siemens kidole juu using JamiiForum mobile app.
 
  • Thanks
Reactions: 365
Watu wa kyamutwala na bugabo ndo wahaya asilia.

Ila tanzania mbona kila kabila inasemekana asili yake ni kutokea nje ya nchi ina maana Tanzania zamani haikuwa na watu?
Lol, hata mimi sielewi hapo.... ila Wazaramo sidhani kama wana asili ya nje.... hawa watu wako pure.... may be ndio wenye Tz yao....

Sent from my Siemens kidole juu using JamiiForum mobile app.
 
Ukabila hakuna Tanzania... Sisi sote ni wamoja...

Cc: mahondaw
Kama kabila hakuna basi sote tungekua tunaongea lugha moja kusingekua na lugha za asili.... uzao wako ni muhimu kikubwa tusibaguane tu.

Sent from my Siemens kidole juu using JamiiForum mobile app.
 
unataka kutambika?
Mbona wachaga wote wanaitwa
wachaga,wakati lugha si wote
wanasikilizana.napo tuanzishe uzi?
"Ya ngoswe mwachie ngoswe".
 
Kimsingi hakuna kabila la Wahaya.Wahaya ni muunganiko wa makabila mengi km ulivyoyataja. Swala la asili ya kila kabila km ulivyoyataja hilo linahitaji taaluma na tafiti, siyo kwa wepesi unaodhania.

Kila kundi lilokuwa na mfalme/ Omukakama lilikuwa ni kabila kamili. Bukoba kulikuwa na abakama wengi na hivyo kuwa na makabila mengi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata mimi mkama wetu aliitwa "Takyamukuma"Pale Bunazi nakumbuka 70 walikuwa wazee wanaenda kuomba mvua!!

Samsung SH 8 Mobile Traveller
 
Mpaka sasa swali halijajibiwa au labda aulize JE NI KABILA GANI AMBALO NDIO MZAWA HALISI WA KAGERA???

Same thing inaenda na Kigoma mpaka sasa mimi kama mimi sijajua wenye asili halisi ya Kigoma ni akina nani.

Sent from my Siemens kidole juu using JamiiForum mobile app.
Sisi tunaoitwa "ABABUMBILO'Ndo halisia ila ukweli Kagera kupata halisia nivigumu kama ilivyo ngumu kumpata "Mtanzania halisi maana hata mgogo ni mkimbizi!!

Samsung SH 8 Mobile Traveller
 
Sisi tunaoitwa "ABABUMBILO'Ndo halisia ila ukweli Kagera kupata halisia nivigumu kama ilivyo ngumu kumpata "Mtanzania halisi maana hata mgogo ni mkimbizi!!

Samsung SH 8 Mobile Traveller
Ababumbilo.... ebwana eeeeh!!!
But nadhan Mtanzania halisi ni Mzaramo au unasemaje kwenye hilo... maana yeye sijasikia wapi alipotokea.

Sent from my Siemens kidole juu using JamiiForum mobile app.
 
Watu wa kyamutwala na bugabo ndo wahaya asilia.

Ila tanzania mbona kila kabila inasemekana asili yake ni kutokea nje ya nchi ina maana Tanzania zamani haikuwa na watu?
Lilikua pori,babu zetu walihamia tu kutoka mapori ya jirani
 
Lol, hata mimi sielewi hapo.... ila Wazaramo sidhani kama wana asili ya nje.... hawa watu wako pure.... may be ndio wenye Tz yao....

Sent from my Siemens kidole juu using JamiiForum mobile app.
Wazaramo ni mchanganyiko wa makabila ya watu wa kutoka nchi mbalimbali walioachwa bagamoyo kipindi cha biashara ya utumwa.
 
Wazaramo ni mchanganyiko wa makabila ya watu wa kutoka nchi mbalimbali walioachwa bagamoyo kipindi cha biashara ya utumwa.
So the real Tanzanians ni nani???

Sent from my Siemens kidole juu using JamiiForum mobile app.
 
Kama bado upo huko waulizie wahaya kuna kabila linaitwa wakoba wapo pembezoni mwa mji wa bukoba maruku katoma na viunga vyake ingawa wamepotea lakini naamimi bado watakuwemo hao ndio wahaya halisi

Sent from my C2305 using JamiiForums mobile app
 
Makabila ya Africa yako fluid kuliko tunavyodhania.

Kuna Chifu mmoja wa kabila Zambia alihojiwa akasema kabila lao halikuwapo kabla ya kuja Waingereza.Waingereza walipokuja, wakalitunga tu hilo kabila kwa sababu ya kurahisisha administration. Wawaambia watu kuanzia leo nyinyi mtakuwa kabila fulani.

Kwa hiyo habari za makabila usizichukulie kama kuna mtu aliye wa kabila fulani "pure".

Hakuna kitu kama hicho.

Sent from my Kimulimuli
 
Back
Top Bottom