Hivi mhaya halisia anatokea wapi mkoa wa Kagera?

Hivi mhaya halisia anatokea wapi mkoa wa Kagera?

Kifaru86

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2017
Posts
1,734
Reaction score
3,832
Wadau zangu kwa sasa nipo mkoa wa kagera nipo maeneo ya BUKOBA.

Katika huu mkoa siku zote najua wenyeji wa Mkuu mkoa ni WAHAYA

Lakini kinachonishangaza WAHAYA wenyewe kwa wenyewe wanabaguana maana nasikia kuna waziba, wanyaingiro, wanyambo, wahamba,waganda kyaka, wayoza

Nilipojaribu kuuzila nikaambiwa hawa...

Waziba wanatokea UGANDA

Wayoza wanatokea shinyanga kiasili ni wasukumaa

Wanyangiro hawa WAKO muleba ASILI yao nimeambiwa ni mchanganyiko wa mrundi na mnyarwanda pia kuna mhutu na mtusI Lakini pia naambiwa NI zao LA mjaluoo ndo maana rangi zao zinafanana

Wanyambo nasikia ni mchanganyiko wa muhutu na mtusi waliokimbia vita ya Rwanda mwaka 1959.

Mganda kyaka huyu nimeambiwa sio muhaya huyu anaitwa ni muhutu wa ugandaa.

Wahamba nasikia hawa ki ASILI NI wajaluo waliolowea muleba muda mrefu sana waka adapt UHAYA.

Jamani hadi sasa hebu tuambieni muhaya asilia anatokea wapi
 
Kimsingi hakuna kabila la Wahaya.Wahaya ni muunganiko wa makabila mengi km ulivyoyataja. Swala la asili ya kila kabila km ulivyoyataja hilo linahitaji taaluma na tafiti, siyo kwa wepesi unaodhania.

Kila kundi lilokuwa na mfalme/ Omukakama lilikuwa ni kabila kamili. Bukoba kulikuwa na abakama wengi na hivyo kuwa na makabila mengi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakubaliana na wewe.Nafikiri huo ndio muungano wa ajabu kabisa.makabila zaidi ya Saba kuungana na Kuwa kitu kimoja.
Wahaya Ni Kama Kusema Watanzania
Lakini Wana makabila mengi ndani yake.
Wahaya waliunganishwa na lugha,Chakula,jiografia
 
kihaya kina lahaja nyingi ikitegemea jirani zao.Hata rafudhi Ni tofauti japo wanaelewana.Hata salamu zinatofautiana,Kuna
Osingire waitu
Wasbota waitu
Mushanage
Tatasbota
Taspota
Hawa ni watani zangu wa jadi[emoji120] [emoji122] . Lakini ni wajuaji sana, mzuri ni aliyekufa [emoji23] [emoji23]

Cairo's
 
Waguma....

So Mkulu wetu ni wa wapi sasa?

Inamaana Wahaya si Kabila Bora Wanyambo wao hawataki kusikia mtu anawaita wao ni Wahaya..
 
Kimsingi hakuna kabila la Wahaya.Wahaya ni muunganiko wa makabila mengi km ulivyoyataja. Swala la asili ya kila kabila km ulivyoyataja hilo linahitaji taaluma na tafiti, siyo kwa wepesi unaodhania.

Kila kundi lilokuwa na mfalme/ Omukakama lilikuwa ni kabila kamili. Bukoba kulikuwa na abakama wengi na hivyo kuwa na makabila mengi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Yodoki, sasa wewe unasema "Enganda" ambazo siyo kabila! au? sina uhakika
 
Mpaka sasa swali halijajibiwa au labda aulize JE NI KABILA GANI AMBALO NDIO MZAWA HALISI WA KAGERA???

Same thing inaenda na Kigoma mpaka sasa mimi kama mimi sijajua wenye asili halisi ya Kigoma ni akina nani.

Sent from my Siemens kidole juu using JamiiForum mobile app.
 
Back
Top Bottom