Hivi kwanini sisi Watanzania tunapenda kutembea taratibu kama konokono?

Wakuu,

Nimetembelea nchi kadhaa za Ulaya na Asia, kule watu wanatembea haraka haraka sana kuwahi kwenye mishe zao, lakini huku kwetu watu wanatembea taratibu kama konokono.

Tatizo ni nini?

Mkuu inategemea ,huenda kawahi kutoka kwake na ana muda mrefu wa kufika anakoelekea
 
Wakuu,

Nimetembelea nchi kadhaa za Ulaya na Asia, kule watu wanatembea haraka haraka sana kuwahi kwenye mishe zao, lakini huku kwetu watu wanatembea taratibu kama konokono.

Tatizo ni nini?

Kumbuka pia, hali ya hewa uchangia. Ulaya ni baridi ukitembea taratibu ndo mwili unazidi pata baridi zaidi. Niliishi kidogo Ulaya nilifanya utafiti juu ya hili ulisemalo. Hivyo hii imewajenga muda wote kuwa katika mwendo wa haraka. Na pia wenzetu mambo mengi uwachanganya. Wazungu ni tofauti na waafrica sisi tunauwezo wa kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja. Lakini wenzetu daah! Anaweza jichanganya. Hivyo ujaribu kufanya kitu kimoja kwa haraka ili apate muda wa kufanya jingine. Na vilevile wametawaliwa na muda. hii uwasumbua sana, kulingana na majira na msimu katika maisha yao. Sasa wewe fikiria mara saa ziende mbele mara zirudi nyuma. Africa hiyo hatuna. Najivunia maisha yetu ya Africa yasiyo na pressure! Ndo maana wa Ulaya wamejaa msongo wa mawazo.
 
Ni kweli mkuu, watanzania tunatembea polepole tena kizembe mpaka tunaboa. Mi nilidhani ni mimi tu ndio naliona hilo. Enzi za watumishi wa umma wapo Dar, basi ukienda maendeo karibu na ofisi zao mida ya kutoka lunch, unakutana na watumishi wa umma wapo vikundi watatu au wanne wanatoka kula, yani wanatembea kizembe hao utadhani hawarudi ofisini. Unakuta wababa wana matumbo, wengine shati limechomoka nusu huku wanatembea kizembe wanachokonoa meno na toothpick, yaani ni shiida.
Sijui walivyohamia huko Dodoma labda wamejifunza kutembea harakaharaka siku hizi.
 
Wakuu,

Nimetembelea nchi kadhaa za Ulaya na Asia, kule watu wanatembea haraka haraka sana kuwahi kwenye mishe zao, lakini huku kwetu watu wanatembea taratibu kama konokono.

Tatizo ni nini?
Nilidhani ni Mimi peke yangu nimeona hili. Nadhani kwa mtu aliyekwenda nje,hasa nje ya Africa atakuwa ameliona hili.

Pamoja na uharaka wa kukimbizana na muda lakini bila shaka kuna factor zingine. Kuna mtu aliwahisema kuwa"HAKUNA MTU ANAYETEMBEA SLOW UKAKUTA AKILI YAKE IPO FASTER. KUNA UWIANO WA MWILI WAKO KIVITENDO NA UWEZO WAKO KIAKILI" .

Na akili inayozungumziwa sio shuleni tu. Maana mbongo akiambiwa fulani ana akili sana atakuambia mbona kaishia la SABA.Binafsi nilianza kuamini hii kitu.

NB: Haikumaanisha watu wote wanaotembea taratibu basi uwezo wao kiakili ni mdogo. Hivyo atakayeona inamgusa hii asikasirike wala kujibu kwa ghadhabu.

Waafrica wengi tupo slow saaana.
 
Kuna "some psychological facts" nilikuwa nasoma kwenye "quora" jamaa anasema kutembea harakaharaka ni dalili ya kujiamini na kutembea taratibu ni dalili ya woga na kutokujiamini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukianza tu darasa la kwanza au la pili unaanza kufundishwa methali zinazo discourage haraka haraka.

Haraka haraka haina baraka.

Mwenda pole hajikwai.

Simba mwenda pole ndo mla nyama.

Kawia ufike etc.

Nafikiri shida itakuwa inaanzia huku.

Hili nalo neno..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom