Hivi kwanini sisi Watanzania tunapenda kutembea taratibu kama konokono?

Sasa mkuu uanze kukimbiakimbia hapo Dar, hilo joto utaliambiaje? Si utaloa jasho kama umenyeshewa mvua? Mwishowe uanze kutunukishia kikwapa! Wenzetu wacha wakimbie maan kule ni baridi!
 
Mkuu nchi hii ilitawaliwa na waarabu coast ya pwani yote.waarabu mambo yao hawana haraka kabisa na kutafuta maisha wanajua ni ya kupita tu.
yan ww ndo kizibo kabisa, sasa kma walitawala pwani nyie wa bara imekuaje? Au TZ ni bara pekee?
 
Wakuu,

Nimetembelea nchi kadhaa za Ulaya na Asia, kule watu wanatembea haraka haraka sana kuwahi kwenye mishe zao, lakini huku kwetu watu wanatembea taratibu kama konokono.

Tatizo ni nini?
Siyo kutembea tu hata kuongea. Utakuta mtu anakupigia simu na anaongea kwa mapozi kama wote hamna cha kufanya.
 
Wakuu,

Nimetembelea nchi kadhaa za Ulaya na Asia, kule watu wanatembea haraka haraka sana kuwahi kwenye mishe zao, lakini huku kwetu watu wanatembea taratibu kama konokono.

Tatizo ni nini?

Huko USA na ULAYA maisha yao yanafungamana na hali ya Hewa kwa kiasi fulani. Kwa mfano huko msimu wa baridi Winter mambo huwa magumu sana ndio maana maisha yao muda ni mchache wa kufanya kazi. Hivyo wanapaswa kutumia ule muda waupatao kwa uangalifu sana.


Lakini huku maisha yetu hayana kufungamana na hali ya hewa mwaka mzima tunapig kazi . Hakuna cha masika wala kiangazi.
So ndio maana watu hawana haraka na mishe zao.

Lakini piq huku maisha yetu tumetawaliwa sana na Imani kuwa Riziki inatoka kwa Mungu ndio maana kukazuka misemo kama

1. Kama ipo ipo tu
2. Riziki mafungu saba
Na misemo mingine ambayo huko Ulaya haipo

Wao kule wana "Time is money"
 
No hurry in Africa , ukitembea speed unaokutana nao barabarani wanaoshangaa shangaa , ukiwaambia nipishe nipite, watakujibu eeeh siungeanza safari toka Jana Kama unaharaka Sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siyo kutembea tu hata kuongea. Utakuta mtu anakupigia simu na anaongea kwa mapozi kama wote hamna cha kufanya.
Na salamu nne kwa wakati mmoja! Mambo? Mzima? Kwema kabisa? Unaendeleaje? Yani kupotezeana tu muda.
 
hali ya hewa. Niligundua hili nilipokuwa Nairobi . Kule wanatembea haraka, nikaja Dar ni polepole. Nikafika Mombasa ni pole pole. Ndio nikajua jua Kali huaababiaha kupunguza speed mwendo
 
Wakuu,

Nimetembelea nchi kadhaa za Ulaya na Asia, kule watu wanatembea haraka haraka sana kuwahi kwenye mishe zao, lakini huku kwetu watu wanatembea taratibu kama konokono.

Tatizo ni nini?
nimejikuta nacheka kwanguvu yaani kuna muda hadi inakera haswa mjini kwenye mishe nyingi unawahi usafiri mtu amekublok mbele na mwendo wa kinyonga hahhahaha hua najiuliza huyu mtu vipi
 
Kuwahi wapi? Kusimama na kusalimiana na jirani dakika 15 hadi 20, kuchat dk 15, fb page dk 20, JF dk 20, lunch 2 hours, foleni 2 hours total 6 hours. So saa zetu za kazi ni 4 tu. Haraka za nini?
Wakuu,

Nimetembelea nchi kadhaa za Ulaya na Asia, kule watu wanatembea haraka haraka sana kuwahi kwenye mishe zao, lakini huku kwetu watu wanatembea taratibu kama konokono.

Tatizo ni nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Joto, jua kali, vumbi la DAR na mwendo kasi wapi na wapi. Ulaya lazima watembee haraka baridi inawatandika.
Hata Arusha, Mbeya, Njombe watu wanatembea haraka ila joto la DAR na pwani yote kwa ujumla si rafiki kwa binadamu kutembea mwendokasi
 
Kwann tutembee haraka kwani tunaharakia wapi? Kuna msemo unasema kama una haraka ungeondoka jana' halafu Hao wa huko ulipokuwa walifundishwa kuangalia kulia, kushoto, halafu kulia ndo wavuke barabara? Hawajui ishu ya simba kwenda pole ndie mla nyama? Na je polepole ndio mwendo? Haraka haraka haina Baraka? Tupo on the light truck' tuvumiliane tu.
 
Kanuni yangu ninayotumia ni hii"walk 25 percent faster"
Kusema ukweli utembeaji wa mtu unaweza kueleza mengi sana kuhusu huyo mtu kuanzia mtazamo wake na uwezo wake wa kufikiri.
Ukiona mtu anatembea taratibu basi ujuwe hata mind yake ipo taratibu sana Katika kupambanua Mambo.Na hii ndo mana nchi za Bara la giza hazipati maendeleo.
Kama ni kweli wale wenye matege halafu wanatembea kasi akili zao ni za namna gani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom