Mrisho Mpoto si msanii wa kwanza duniani kutembea na kusafiri peku

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
617
1,800
mpoto.jpg

Mrisho Mpoto

Watanzania wengi wanamjua Msanii Mrisho Mpoto ambaye anafahamika si tu kwa kazi zake, bali pia kwakuwa hutembea peku peku wakati mwingi.

Mpoto amejipatia umaarufu kwa utaratibu wake huo katika ukanda wa Afrika Mashariki, lakini je, ni kwanini aliamua kutovipa viatu umuhimu katika Maisha yake kama wasanii wengine wanaotumia fedha nyingi kujing’arisha kwa ‘dundo kali’?

Katika baadhi ya mahojiano yake, Mpoto anaamini kwamba ili binadamu awe na akili na kuepuka kifo cha mapema, miguu lazima iwe na mawasiliano na ardhi. Anaamini kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya ardhi na mwili – kwamba ukuaji wa mtu unategemea asili tuliyonayo, hewa tunayotumia, maji na udongo. Kwa hivyo kuna nguvu kubwa chini ya ardhi.

Wanapeku wengine
Hata hivyo, Mpoto si wa kwanza wala wa pili, tatu au kumi kutembea peku kwa kuamua, tena akiwa na umaarufu. Watu wengi maarufu duniani pia wamekuwa waki-practice utaratibu huu unaojulikana kwa jina la Earthing ili kurejesha usawa wa miili yao na kuchochea uponyaji wa mwili wa asili.

Benjamin Clementine ni Mwingereza Mweusi. Jamaa ni mshairi, mwimbaji, mtunzi, mchezaji wa vyombo vya muziki. Aliwahi kuhojiwa kwanini havai viatu akasema kuwa aliwahi kuweka dhamira ya kuwa hata akipata umaarufu hiyo itakuwa ndiyo style yake.

Anaeleza kuwa wakati fulani alikuwa akicheza piano na viatu vilikuwa vikimsonga sana kwani hakuweza kugusa pedali vizuri, ndipo aliamua kuvivua na kucheza bila viatu, na hapo ndipo safari ya kuvaa viatu ilipoishia.

benjamin_clementine_.jpg

Benjamin Clementine
Mutabaruka ambaye yeye ni mwanamuziki, mwigizaji, mwalimu, na mwendeshaji wa vipindi vya mazungumzo wa nchini Jamaica, pia ni miongoni mwa watu maarufu zaidi duniani wanaotembea peku wakati wote.

Katika mahojiano kadhaa na vyombo vya habari, Mutabaruka ameelaza kuwa kutovaa viatu haikuwa uamuzi alioufanya ghafla tu. Anaeleza kuwa wakati fulani alikuwa anaishi katika vijiji ambapo watu wenye imani ya Rastafari walikuwa wakiishi baada ya kuondoka mjini ili kuishi maisha ya asili.

Huko watu walitembea peku ili ku-connect na nature, hivyo baada ya yeye kurudi jijini Kingston aliendelea kutembea bila viatu na amefanya hivyo kwa zaidi ya miongo mitatu sasa.

Muta.jpg

Allan "Mutabaruka" Hope
Mpekuaji maarufu mwingine ni huyu jamaa anayeitwaa Wanlov Kubolor, ambaye ni mwanamuziki, mwongoza filamu, mwanautamaduni kutoka Ghana.

Wanlov anasema kuwa kutovaa viatu kunamfanya mwili wake kuwa na mawasiliano na ardhi, jambo ambalo ambalo linamnawirisha, kumhamasisha, kumburudisha, na kumfurahisha. Anasema akiwa peku ni rahisi kwake kukumbuka jinsi maeneo aliyopitia yalivyohisi chini ya miguu yake.

Wanlov_the_Kubolor_.jpg

Wanlov Kubolor
Ingawa bado wapo watu maarufu wengi wanaotembea peku, tumalizie na mwanamama huyu nguli wa muziki kutoka nchini Cape Verde. Cesária Évora, au Malkia wa muziki wa Morna kama alivyotambulika duaniani kote, ni mshindi wa tuzo ya Grammy. Ingawa sasa ni marehemu, lakini alipeperusha bendera ya nchi yake kote duniani huku akitembea peku kila alipoenda.

Sababu yake ya kutembea peku ni kwamba alipokuwa mdogo siku zote alikuwa bila viatu. Alitembea mitaani bila viatu. Kwahiyo baada ya kuwa mtu mzima ameaona kuwa yupo huru zaidi kutembea bila kuvaa viatu, ingawa mara kadhaa huvaa kidogo ili miguu yake isigande sehemu baridi.

Evora.jpg

Cesária Évora, nguli wa muziki wa Morna kutoka Cape Verde

Jamaa mwingine anayekata mitaa akiwa peku ni Bw. Michael Franti. Huyu yeye ni mwimbaji, mshairi, msanii wa kughani (spoken word artist), na mwandishi wa nyimbo kutoka Marekani. Franti yeye alianza kutembea peku baada ya kusafiri duniani na kuona watoto ambao hawakuwa na viatu akaamua kumulika tatizo kwa kutembea peku pia.

Kwahiyo, kilichoanzia kama siku kadhaa za kuacha kuvaa viatu ili kuongeza uelewa kuhusu tatizo, kimegeuka kuwa miaka 20 mfululizo ya bila kuvaa viatu. Franti mara chache huvaa viatu anapoingia ndani ya ndege au mgahawa. Wale wanaohudhuria maonesho yake huhimizwa kuja na pea ya ziada ya viatu ili kusaidia watoto na watu wazima ulimwenguni ambao hawana viatu.

michael-franti-.jpg

Michael Franti & Spearhead ni kikundi cha muziki wa aina ya alternative-rock ambacho huchanganya hip-hop, reggae, folk, na jazz katika nyimbo zinazoakisi harakati za kupinga vita na masuala ya ukiukaji wa haki za kijamii. Franti anaonekana katikati ya bendi akiwa peku.
Hata hivyo, ingawa wengine wanaweza kuona kutembea peku ni jambo la kushusha hadhi ya mtu, lakini baadhi ya tafiti zinaonesha kuwa mawasiliano ya umeme yanayofanywa kati ya mwili wa binadamu na uso wa ardhi (earthing au grounding) husababisha athari nzuri kwa afya.
 
Sayansi za Mrisho Mpoto sio za nchi hii, aliwahi kusema vijana wengi wanakuwa na ushoga kwasababu ya kukalia pot walipokuwa watoto. Alisema wao zamani waliachwa washushe popote tu bila pingamizi.
 
msanii wa kwanza tangu lini. Maana viatu vimeanza majuzi tu. Zamani vilikuwa anasa kama kumiliki private jet na wasanii walikuwepo wengi tu.
 
Miaka ya 80,90 huko morogoro alikuwepo yule mzungu farther winge...alikuwa muda wote tunamuona anatembea peku
Awe mjini ama vijijini yeye ni peku tu
Hawa wakina mpoto kuwaona wakiwa peku hata hatushtuki

Ova
 
Mwenye ile shuleee
Miaka ya 80,90 huko morogoro alikuwepo yule mzungu farther winge...alikuwa muda wote tunamuona anatembea peku
Awe mjini ama vijijini yeye ni peku tu
Hawa wakina mpoto kuwaona wakiwa peku hata hatushtuki

Ova
 
Back
Top Bottom