Hivi kwanini sisi Watanzania tunapenda kutembea taratibu kama konokono?

Wakuu,

Nimetembelea nchi kadhaa za Ulaya na Asia, kule watu wanatembea haraka haraka sana kuwahi kwenye mishe zao, lakini huku kwetu watu wanatembea taratibu kama konokono.

Tatizo ni nini?
Ccm imewabemenda kila MTU anakiriba tumbo...utatembea haraka unataka iwaje
 
Vipi kuhusu marafiki kujikusanya na kwenda sokoni, unawakuta hadi watano hivi wanatembea taratibu huku wanapiga stori. Ukitaka kuwahi mishe zako tembea peke yako kwa kasi.
 
Sio wote kaka, thread yako umeconclude wote, mi mbona nakamua fasta fasta tu
 
Wakuu,

Nimetembelea nchi kadhaa za Ulaya na Asia, kule watu wanatembea haraka haraka sana kuwahi kwenye mishe zao, lakini huku kwetu watu wanatembea taratibu kama konokono.

Tatizo ni nini?
Sio wote. Mwendo wangu ni wa kijeshi sina muda wa kupoteza kutembea kwa madaha.
 
siyo kutembea hata salamu mfana habari yako mtu anasema habariiiiiiiiiii yakoooooooo,how ayuuuuuu kwaheriiiiiii.
Hilo ndiyo tatizo.
Sasa watu wa hivyo, waliozoea 'polepole' hata yale 'mambo yetu' ukimfanyia haraka haraka ana kudharau. Utasikia anakuuliza...' una haraka gani?'......
 
Pilika za uchumi ndo zinachangia mtu kwenda kasi au slow. Hata wewe mwenyewe ukiwa kariakoo kama dili zako zimebuma utarudi ukiwa mpole sana huna haraka na mwazo chungu mzima. Ila sasa ikitokea dili zako zimelipa na unatakiwa urepoti maeneo mawili matatu tofauti mjini utaona kama mda hautoshi utatembea kasi kama radi kwa vile unajua ukichelewa kufika maeneo hupati hela mda ukiiisha. Kwaiyo ukiona wabongo wengi wapo slow siyo kwamba ni utamaduni wao ni vile dili zimebuma na wana mawazo, ukiona mtu yuko kasi ujue anawahi muda asije kuchelewa maeneo yake ya hela akakosa hela kwa sikuiyo. Ni swala la uchumi tu na mzunguko wa pesa, uchumi wetu bongo ni mdogo na watu wengi wameachwa dili zao zimebuma hivyo hawana cha kuwahi, ila wenzetu uko mbele uchumi ni mkubwa na watu wengi mno dili zao zimetiki hivyo ukiona wapo kasi ni kwamba wanawahi mpunga wasije wakachelewa maeneo yao wanakopatia hela. Ni ivyo tu wala siyo swala la rangi au joto au baridi.
Hii ni kweli, na mtu akitaka kuthibitisha apite ferry ajionee watu wakishuka kwenye pantoni wanavokuwa na kasi kubwa kuwahi mishe zao
 
Sa utembee haraka haraka wkt hata unakoenda hujui km utapata kazi! Usifikiri unaopishana nao wote wanaenda job. Wengine wanazurula tu no work
 
Hahahaha!! aise umeongea ukweli mtupu mara ya kwanza kutoka nje ya Tz, asubuhi nilivyoamka nikatoka nje nikaona kila mtu anatembea haraka ikabidi nisimame kushangaa watu wanavyotembea haraka haraka mpaka nikamuuliza mwenyeji wangu kulikoni na kuniambia kuwa ndo walivyozoea.
Mhhh 🏃😂
 
Wakuu,

Nimetembelea nchi kadhaa za Ulaya na Asia, kule watu wanatembea haraka haraka sana kuwahi kwenye mishe zao, lakini huku kwetu watu wanatembea taratibu kama konokono.

Tatizo ni nini?
Kwetu miundombinu mibovu unaweza kujikwaa ukaangukia kwenye maji ya chooni.
 
Hahaaa umelenga ndipo,ni uvivu hakuna kingine na ni ukweli mchungu.
 
Katika mada hii mada imenigusa sana umewaza kitu cha uhakika kabisa watanzania ni wavivu wanapotembea wanaudhi pindi wewe upo fasta unakuta mtu yupo mbele yako kakuziba njia anatembea kama kinyonga
Wakuu,

Nimetembelea nchi kadhaa za Ulaya na Asia, kule watu wanatembea haraka haraka sana kuwahi kwenye mishe zao, lakini huku kwetu watu wanatembea taratibu kama konokono.

Tatizo ni nini?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom