My dear Zanzibar

Etugrul Bey

JF-Expert Member
Aug 6, 2020
3,520
6,503
Hapana shaka kabisa Zanzibar imejibebea sifa nyingi hapa ndani katika jamhuri ya Muungano na nje ya nchi pia.

Na imebeba historia kubwa ya mambo ambayo inawafanya wageni kutoka mataifa mbali mbali kwende kutembea huko na kujionea utajiri wa historia wa mambo ya Kale.

Bila kusahau ukarimu wa Wazanzibar ambao kwa miaka mingi sana wamekuwa wakiishi kwa upendo na mapenzi kwa jamii nyingine.

Inasemwa huko zamani kabla ya watanzania bara hawajaanza kwenda huko kwa wingi, ilikuwa si jambo la ajabu kuacha au kusahau mali yako Sehemu na ukaikuta salama salimini, kwani hakika wanzazibar ni watu wenye imani kubwa na hofu ya Mungu ambayo imewajenga kuwa na imani pamoja na huruma.

Lakini baada ya ujio wa sisi wabara nasikia mambo yakabadilika, ustaarabu kwa kiasi kikubwa ukatoweka, uaminifu ukaisha na janja janja nyingi ikaingia huko, na ikawa sio zanzibar ile tena tunayoijua.

Pamoja na yote hayo bado zanzibar ina miiko yake na tamaduni zake ambazo bado wakazi wa huko wanajivunia nazo,na hiyo ndio asili yao.

Nakumbuka hivi karibuni kulizuka maneno mengi kuhusiana na wamasai kutotakiwa kutembea na silaha za jadi, watu walisema mengi sana juu ya Zanzibar. Swali linakuja je wazanzibar waache kufuata sheria zao kisa tu jamii fulani inaendeleza tamaduni zake?

Jibu hapana kila sehemu kuna sheria na taratibu zake, kinachopaswa kufanywa ni jamii hiyo inapoingia mazingira mapya inatakiwa ifuate taratibu za huko na huo ndio uungwana, kisha baadae wakirudi wanapotoka basi waendeleze tamaduni zao.

Nakumbuka hata wazungu wakienda sehemu yoyote kutalii kwanza hujifunza tamaduni na desturi za eneo husika ili wasije kuwakwaza wenyeji wa huko. Na ndio wazungu wanaoenda zanzibar huwezi kuwakuta wanatembea na vikaptula vifupi kwakuwa wanajua huo usio utamaduni wa wazanzibar.

Wakazi wengi wa Zanzibar ni waislamu ambao miongoni mwa ibada zao kubwa ni kufunga mwezi wa Ramadhani, hii ni ibada kubwa si kwa wazanzibar tu bali kwa waislamu duniani kote.

Zanzibar imejiwekea utaratibu wa kutokula hovyo hadharani katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani na lengo ni jamii ipate kuheshimu ibada hii adhimu na muhimu sana katika dini ya kiislamu.

Lakini bahati mbaya sana kuna watu ambao kwa mitazamo yao hasi wanaona jamii nyingine isiyo ya kiislamu inatengwa na kubaguliwa huko zanzibar, kitu ambacho si kweli.

Watu hawa huanzisha choko choko ili mradi tu taswira ya zanzibar ipate kuchafuka huko duniani,,, Watanzania huu sio utamaduni wetu hata kidogo, tunajulikana kama kisiwa cha amani basi ebu tusianze kuharibu taswira yetu kama Taifa.

Siku zote mitafuruku yote iwe ya kisiasa au ya kidini huanza kidogo kidogo kama hivi na mwisho wa siku linakuwa bomu ambalo halitamchagua mzanzibar wala mtanganyika,sisi sote tutakuwa katika balaa kubwa.

Ombi langu kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar muainishe maeneo maalumu ambayo wale ambao sio waislamu wapate kwenda kula milo yao huko na wawe huru kwa hilo, na hata kama ipo kwa sasa basi iongezwe ili ikidhi mahitaji halisi, kwani inahuzunisha sana kila Ramadhani inapoingia kunawepo na kashfa kama hizi.

Natumaini kwa uwezo wa Allah subhanahu wataala atawawezesha kuliendea jambo hili kwa hekima na busara kubwa.

Asante

Ni hayo tu!
 
Mkuu usipate tabu ,hapo utajua watanzani ni mbumbumbu sana kwanza video ya miaka sita nyuma.

Cha pili CCM wanashangalia hapa ,just imagine ile report ya CAG ya jana leo nyuzi hazitembei, wamehamia kwenye wazenji.

Nchi ina ujinga sana ,yaani kuna jamaa leo katweet kama mara 20 kote katukana waislamu badala ya wazanzibar ,mpaka mda huu CCM wanashangalia hawa watu wapo busy .

Kesho baada ya matokeo ya leo ya simba vs Al ahly patakuwa na mjadala mwingine kabisa 😁😁hao ndio watanzania.

Ile ishu ya joshua Mollel ilikaaa siku mbili kimya ,palikuwa na watu wanataka kwenda kupambana sijui wameishia wapi?
 
Mkuu usipate tabu ,hapo utajua watanzani ni mbumbumbu sana kwanza video ya miaka sita nyuma.

Cha pili CCM wanashangalia hapa ,just imagine ile report ya CAG ya jana leo nyuzi hazitembei, wamehamia kwenye wazenji...
Kweli kabisa chief

Badala ya kuongelea mambo ya msingi ambayo yanaweza kumuinua mtanzania lkn badala yake tunapoteza muda mwingi katika mambo ya kipuuzi kabisa.

Taarifa ya Cag ingetuamsha na kuongelea ni vipi rasimali za taifa zitumike kwa maslahi ya wengi lkn hatulioni hilo,,, hlf baadae tunaanza kulalamika,, sijui tumerogwa na nani
 
Nyerere kwanini ulituletea muungano nusu nusu!!?

Kama Kuna nchi iitwayonTanzania kwanini Kuna marais wawili!!?

Zanzibar ilipaswa kugawanywa kwenye mikoa kadhaa na sio iwe nchi tena!!

Zanzibar ilipaswa iwe na majimbo manne TU !iwe na mikoa minne tu!

Ujinga kama huu usingekuwepo nchini na watu wangezoea kuwa Kyle hakuna nchi Bali ni mkoa was Tanzania!!

Nyerere ulitukosea sana!!
 
All in all udini hautakiwi Tanzania, Hii nchi si ya kiislam na wala hakuna kipande cha nchi kitakachojinasibu ni cha kiislam, otherwise katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ibainishe hilo
 
All in all udini hautakiwi Tanzania, Hii nchi si ya kiislam na wala hakuna kipande cha nchi kitakachojinasibu ni cha kiislam, otherwise katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ibainishe hilo
Sijui kama zanzibar wamejiainisha kuwa ni nchi ya kiislamu.

Na wala hawahitaji kufanya hivyo hata kidogo,,, kikubwa utaratibu wao uheshimiwe
 
Mashoga kila nyumba na kuwafukua mitaro wake zenu huku mmejificha kwenye imani unadhani ni vizuri? Mnajifanya kwenda sokoni Wanaume kumbe wake zenu bila pampers hawawezi kutembea
Unaweza kudhibitisha chief au kwakuwa upo nyuma ya keyboard basi unaropoka tu.

Usiwavunjie watu heshima na utu wao kwa tuhuma za vijiweni
 
😂😂
 
Ombi langu kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar muainishe maeneo maalumu ambayo wale ambao sio waislamu wapate kwenda kula milo yao huko na wawe huru kwa hilo, na hata kama ipo kwa sasa basi iongezwe ili ikidhi mahitaji halisi, kwani inahuzunisha sana kila Ramadhani inapoingia kunawepo na kashfa kama hizi.
Point ya msingi hii
 
Unaweza kudhibitisha chief au kwakuwa upo nyuma ya keyboard basi unaropoka tu.

Usiwavunjie watu heshima na utu wao kwa tuhuma za vijiweni
Tutaendelea kuwavunjia heshima kwasababu nawao wameamua tusiheshimiane,kumchapa mtu hadharani ni Utu?wangeanza na huyu choko kumchapa fimbo au imani inaruhusu
Screenshot_20240329-160738.png
 
Sielewa ila nimelike tu ili mleta mada aendelee kumwaga magazeti
 
Unaweza kudhibitisha chief au kwakuwa upo nyuma ya keyboard basi unaropoka tu.

Usiwavunjie watu heshima na utu wao kwa tuhuma za vijiweni
Yule ustaadhi aliyempa mimba mwanafuwa form two Zanzibar ni kweli au ulongo?
 
Back
Top Bottom