Kuna muda nahisi na kuona kuwa imani ndiyo kizuizi kwa waafrika au sijui mnaonaje wenzangu

Mhafidhina07

JF-Expert Member
Aug 1, 2014
2,556
2,994
kwanza salaam!

MBALI NA KATIBA

KAMA IMANI NI MAENDELEO KWANINI TUSIFUNGE NA KUOMBA TUYAPATE?

Natambua kuwa ipo nadharia ya dunia ni duara,unavyopanda mchicha hutaotesha mbuyu abadani kwa nadharia hii inanikumbusha karne moja iliyopita wengi wa mababu zetu walikuwa ni weupe walidanganywa na kugaiwa dude kubwa la imani waangaike nalo huku wazungu na waarabu wakichota wanachokitaka, hili dude nchi zote unazoenda ambazo zimejinasibu na kulishikilia unakuta watu wake wanaishi kwa matumaini pamoja na uchawi kuwa ipo siku ,ipo siku ila bado hatujaweza kuteguwa kitendawili na bado hata wenye mamlaka kwa kuwa wanaamini kuwa wao ndiyo wenye haki kuwa pale wanaendelea kuishi kwa nguvu ya viongozi wa kiimani/kurubuni.

Nchi nyingi za ulaya ziliishi katika hali hii ila baadae waligundua kuwa wachache ndiyo wanafaidika kwa mfumo huo hivyo wakafanya mapinduzi ya kisayansi, siasa, uchumi na kijamii kwa lengo la kuleta tija ya mabadiliko kwa jamii zao lakini huku kwetu mambo ndiyo yale yale ndiyo maana uchawi mwingi unazuia watu wasiendelee hizo ni roho za mababu wasiopenda maendeleo.

Hebu angalia viapo vya akina yakubu kuwa anamuamini mungu wa baba yake na babu yake iweje sisi tuamini katika wao?

AFRIKA TUAMKE
 
Una mapepo wewe njoo Kawe ukanyage mafuta.
Wewe ndio una mapepo! Kawe Kuna nini? Kwani amekwambia ana shida ya nyama ya ng'ombe?? Kwa maana pale Kawe Tanganyika Parkers wewe je hujui kulikuwa na kiwanda Cha nini? Basi kama hujui uliza Kwa wazawa wa DSM, ndio maana mnafanywa kafara!!
 
Njoo ukanyage mafuta pia.
 
kwanza salaam!

MBALI NA KATIBA

KAMA IMANI NI MAENDELEO KWANINI TUSIFUNGE NA KUOMBA TUYAPATE?

Natambua kuwa ipo nadharia ya dunia ni duara,unavyopanda mchicha hutaotesha mbuyu abadani kwa nadharia hii inanikumbusha karne moja iliyopita wengi wa mababu zetu walikuwa ni weupe walidanganywa na kugaiwa dude kubwa la imani waangaike nalo huku wazungu na waarabu wakichota wanachokitaka, hili dude nchi zote unazoenda ambazo zimejinasibu na kulishikilia unakuta watu wake wanaishi kwa matumaini pamoja na uchawi kuwa ipo siku ,ipo siku ila bado hatujaweza kuteguwa kitendawili na bado hata wenye mamlaka kwa kuwa wanaamini kuwa wao ndiyo wenye haki kuwa pale wanaendelea kuishi kwa nguvu ya viongozi wa kiimani/kurubuni.

Nchi nyingi za ulaya ziliishi katika hali hii ila baadae waligundua kuwa wachache ndiyo wanafaidika kwa mfumo huo hivyo wakafanya mapinduzi ya kisayansi, siasa, uchumi na kijamii kwa lengo la kuleta tija ya mabadiliko kwa jamii zao lakini huku kwetu mambo ndiyo yale yale ndiyo maana uchawi mwingi unazuia watu wasiendelee hizo ni roho za mababu wasiopenda maendeleo.

Hebu angalia viapo vya akina yakubu kuwa anamuamini mungu wa baba yake na babu yake iweje sisi tuamini katika wao?

AFRIKA TUAMKE
Imani ni shambulio la akili.
 
Back
Top Bottom