Hivi kwanini Mungu ana wivu?

Hivi kwanini Mungu ana wivu?

Nafikiri tumeanza kuelewana, mimi kwenye maswala ya kujifunza huwa ni mweupe sana.

Hivyo huwezi kuhitimisha na kukataa kitu ambacho huwezi kuthibitisha kutokuwepo kwake.

Tofauti na hapo sema hivi kulingana na utafiti wa sayansi bado haujathibitisha uwepo wa Mungu.
hatujaelewana ila umekariri,

tambua kuna science ambapo kiini chake ni research pia kuna dini,itikadi ambapo kiini chake ni imani.
 
Umetaja fikra , faith na dreams mkuu wewe ni mjanja sana, ndio maana kila siku nakuambieni Mungu ni nadharia iliyo kichwani kwa muumini tu, ndio maana kamwe binadamu hawataweza kuwa na imani moja kuhusu Mungu ,kwa sababu kila mtu ana nadharia yake kutoka kwenye utamaduni wake na mapokea kama athari ya ukoloni.
Upo sawa, MUNGU anaanzia kwenye mawazo, nadharia au tuziite fikra za mwanadamu husika ila hii haimaanishi kuwa hayupo, as long as uwepo wake kwenye hizo fikra unaaffect maisha kama tuyajuavyo tayari yupo ndo maana anatamkwa, anajadiliwa, analinganishwa, anaabudiwa, anapiganiwa n.k n.k

Kuhusu aina gani ya imani iliyomzaa MUNGU kwenye fikra binafsi ninachojua ni kuwa hata wakoloni wasingekuja, MUNGU angekuwepo Africa.
 
Sayansi ikimvumbua MUNGU, hatakuwa MUNGU tena. Sayansi itajiuliza swali jingine litakalosababisha kuendelea kumtafuta MUNGU. Unadhani kwanini sayansi haiamini katika MUNGU?
Kwanza ngoja tudadavue swali lako ili nielewe Mungu yupi kwani unaye mzungumzia ,kuna Allah kuna yehova kuna Yesu ,kuna shangdi, Amaterasu, vishnu , mrungu ,ruwa Enkay,kabelele na nk ,kumbuka Mungu wote hao wana tabia na ahadi tofauti kwa hiyo kiufupi sio mmoja.
 
Irrelevant comparison, muweza yote,nguvu zote na unlimited love unamlinganishaje na mtu.
Jaribu ku meditate utajielewa mkuu, why tunamuita Simba wa Yuda. Kuna maneno na neno ni vitu viwili tofauti
 
Upo sawa, MUNGU anaanzia kwenye mawazo, nadharia au tuziite fikra za mwanadamu husika ila hii haimaanishi kuwa hayupo, as long as uwepo wake kwenye hizo fikra unaaffect maisha kama tuyajuavyo tayari yupo ndo maana anatamkwa, anajadiliwa, analinganishwa, anaabudiwa, anapiganiwa n.k n.k

Kuhusu aina gani ya imani iliyomzaa MUNGU kwenye fikra binafsi ninachojua ni kuwa hata wakoloni wasingekuja, MUNGU angekuwepo Africa.
Kwa hiyo kiuhalisia umeamini hizo ni illusion na hallucinations tu ! Kama mimi pia sina hizo fikra imani kwangu hayupo?
 
Jaribu ku meditate utajielewa mkuu, why tunamuita Simba wa Yuda. Kuna maneno na neno ni vitu viwili tofauti
Meditation haina uhusiano na mambo ya simba wa yuda , wala Meditation haikufanyi uone kuna kiumbe kina kupa nguvu , mkuu bado wewe ni lena ,ila sio kwa ubaya lakini.
 
Uko sawa, naposema mtu aliumbwa kwa mfano wa mungu namaanisha mtu(nishati).
Huu mwili wa nyama ni chombo tu sio mtu, hivyo alivyosema alimuumba mtu kwa sura na mfano wake ni hiyo nishati.(hata biblia imeeleza tunaona baada ya kumfanya mtu kwa mfano wake kisha aliwekwa katika mwili, Adam).

Asili ya mtu ni Mungu, na asili ya mwili ni ardhi(earth), hizi sura zetu za kimwili ni matokeo ya vizazi na vizazi toka mtu wa kwanza kuepo hadi sasa na zinatofautiana kulingana na mabadiliko ya genes zinazosababishwa na mazingira.
Mazingira yanapelekea kuundwa kwa asili fulani lakini haimaanishi yanabadili uhalisi, hivyo tuna miili ya mifano na sura tofauti kulingana na asili zetu ila kiuhalisi tuko mtu mmoja ambaye ametokana na chanzo kimoja (God).
Wanyama na mimea nayo ina nishati, vipi nayo ni mfano wa mungu?
 
Mkuu Tatizo umejibu swali ambalo sijauliza na umechanganya Mindset yangu na watu wengine uliofanya nao Conversation kwenye Mada hii..

Na umeshindwa kujua Why Nimekuuliza kuhusu swali dogo la Biden au Trump (Ni watu wanaofahamika Duniani)..

Umetaja Ibrahimu na ukasema umetokanaa na ibrahimu..nikajibu ibrahimu Hajatokana na watu wa kushi wala Tanzania..

So Narudi kwenye Swali lako (Mimi naongea Taratibu sana ila Wewe unapiga Kelele na kufoka kwanini wote tusiongee taratibu 😃😃)

Kuhusu Uumbaji Kuna Hadithi tofaufi za uumbaji Inategemea na Imani na Taifa ulilotoka..

Only Hadithi au Imani ya Ibrahimic Religion ndo inaanza kwa Adamu and Hawa ila ukienda kwa Imani zingine tofauti na Ibrahimic Faith kuna Aina nyingine ya Hadithi za uumbaji na wao pia wanaamini ziko Sahihi..

Sijui umenielewa?
Nimekuelewa vizuri mkuu, ila najaribu kukuelewesha ili unielewe vizuri kwamba unachozungumza wewe ni tofauti kidogo na kile ninachozungumza mimi. Ulimwengu una takriban miaka bilioni 14 na dunia ina takriban miaka bilioni 3.5. Source ya uhai katika sayari ya dunia (sifahamu kuhusu sehemu zingine ulimwenguni) ni living cell DNA ambayo kiasili ndiyo chanzo chetu sisi viumbe hai wote.Kwa hiyo ukijaribu kufuatilia muendelezo wa evolution mpaka kufikia apes na hatimaye mwanadamu, sio tu kwamba chanzo chetu ni kimoja bali we are all related. Sasa sembuse huyo Ibrahim sijui Biden sijui Trump? Sio binadamu? Kama tembo tu we are related as mammals sembuse binadamu? Kwa hiyo iwe Massawe sijui Shirima, Trump, Biden n.k Wote ni binadamu chanzo chetu ni kimoja na Creator ni mmoja.
 
You’re just an imposter.

Unaji contradict mwenyewe kama umesema ni muweza wa yote kwanini unaweka limit afanye tu unayotaka wewe au hujui maana ya dhana ya muweza wa yote?

Una Brain tumor wewe sio bure.
Si muweza wa yote tu, bali ana upendo mwingi na nguvu zote kwaio hatutegemei udhaifu wowote kutoka kwake.
 
Ok wewe tafiti zako zimeegemea wapi
mimi sijaona gap la kutafiti,ila kwakuwa kuna kitu kinaitwa imani hivyo nilianza kutafuta maana na kuangalia zipoje na nilivyoona gap nikapa jibu ila ni langu tu.
 
Meditation haina uhusiano na mambo ya simba wa yuda , wala Meditation haikufanyi uone kuna kiumbe kina kupa nguvu , mkuu bado wewe ni lena ,ila sio kwa ubaya lakini.
Kwani meditation mkuu unaielewaje???
Nilichomaanisha ni usome hayo maandishi kwamakini kwa tafakuli ya hasa.
 
Kwanza ngoja tudadavue swali lako ili nielewe Mungu yupi kwani unaye mzungumzia ,kuna Allah kuna yehova kuna Yesu ,kuna shangdi, Amaterasu, vishnu , mrungu ,ruwa Enkay,kabelele na nk ,kumbuka Mungu wote hao wana tabia na ahadi tofauti kwa hiyo kiufupi sio mmoja.
Hapa concept ni MUNGU sio mungu wa imani fulani. Ukifuta hizo imani zote, MUNGU anafutika? Au anaibuka kwa namna ingine? Huko kwenye aina za mungu sina comment mkuu.
 
Maswali mengine ni ya kijinga sana, yaani unataka sisi tukujibu kwanini Mungu ana wivu, si umuulize mwenyewe ili upate majibu yaliyosahihi juu ya huo wivu wake?
 
Wataalamu wa bibilia, nakumbuka kuna siku nilisoma hicho kitabu nikaona historia ya mnara wa babeli Mungu aliposhuka na kuwakuta binadamu wanatengeza ule mnara alishtuka na kuwatenganisha kwa lugha pamoja na maeneo ndiyo yakazaliwa mataifa mengine.

Tukio la pili kwenye sura ya mwanzo Mungu baada ya adamu kula ule mti ambao alikatazwa inaonekana ibilisi alikuwa anajua siri ya mti huo wa uzima japo hakuufahamu haswa ni upi ila baada ya Mungu kuona binadamu na jeshi lake watapanga kuutafuta ndiyo akauficha, nimesahau exactly ni wapi.

Case ya tatu, baada ya kuwatoa Wanaisraeli kupitia Mtume wake Musa aliwaambia kuwa yeye ni Mungu mkuu na anawivu hivyo wasiabudu mwengine isipoikuwa yeye.

Je, kwa kauli ya kusema kuna miungu mengine anafahamu kuwa kuna nguvu nyengine tofauti na yeye?

Je, hajiamini na nguvu zake?

Je, Mungu huyu ni tunayemuabudia wakristo na waislamu?

Je, ni binadamu wa mwanzo ambaye aliwahi kutambua siri za ulimwengu na akajitahidi kuzificha na hatimaye akajitolea taji la uungu?

Nawasilisha.
Kwa sababu sisi ni viumbe wake na ametuumba kwa mfano wake. Sisi sote ni wa kwake inapokuja kutokea hatumtii na kumfuata lazima kuna ambaye ni tofauti na yeye tunamfuata hapo ndipo wivu hutokea kwa sababu tumeumbwa ili tumfuate yeye Muumba.
 
Kwani meditation mkuu unaielewaje???
Nilichomaanisha ni usome hayo maandishi kwamakini kwa tafakuli ya hasa.
😁😁😁 sawa mkuu nmekuelewa ,hawa watu wa simba wa yuda nina kazi kubwa sana yakuwatoa tongotongo ndio maana 😁😁
 
Back
Top Bottom