Hivi kwanini kitambulisho cha Mpiga Kura kinapatikana kwa siku moja lakini kitambulisho cha taifa kinapatikana baada ya miaka miwili?

BB_DANGOTE

Member
Sep 25, 2023
32
23
Ndugu wana JF hili ni swali nililojiuliza sana kwa muda mrefu.

Kwa tathimini kwamba zaidi ya asilimia 60 taarifa za wananchi zanapatikana mtandaoni kwa kuwa siku za saivi asilimia kubwa ya watu wamesoma na kama wamesoma na kuhitimu unamaanisha taarifa zao zote zinapatikana kwenye mfumo wa serikali ikiwemo mwaka na tarehe ya kuzaliwa pamoja na jina lako na la wazazi wako na mengine mengine mengi.

Kwangu mimi naona huu ni uzembe na kukosa uwajibikaji kwa sector husika, kwani wanajamii mnaonaje kuhusu hili suala?

Karibuni.
 
Au kunakikwazo kinacho sababisha mambo haya yawe ivo labla wenye uelewa watusaidie jambo hili
 
Ukiona nchi ambayo huduma za maji umeme hazifiki vijijini ila kipindi cha uchaguzi masanduku ya kura yanafika jua upo kwenye nchi ya viongozi wahuni na matapeli.
 
mmm ndo mana msanii mmoja nilimsikia alisema "viongoz wa marekan wakija bongo na wa bongo wakienda marekani utasikia marekani itaomba msaada bongo"
 
  • Thanks
Reactions: _ID
ila tunaweza kusema urasimu kumbe kuna ugumu unakuwepo wakati wa utengenezaji wa ivo vitambulisho
 
Back
Top Bottom