SoC03 Akirudi mkoloni atukute na Kitambulisho cha Taifa

Stories of Change - 2023 Competition

Gill Rugo

Member
Aug 28, 2022
26
116
Mfalme Leopold Philippe, nina uhakika yupo kuzimu, meza moja na Henry Morton Stanley. Wanapokaa, unaliona pembe la kushoto la shetani kiangavu zaidi. Najua watakua wanacheka. Ndio, kuna moto unawasubiri; lakini, kazi yao duniani inameremeta mpaka leo. Wanacheka kwa sababu kuna kijana atachomwa moto kwa kosa la kuiba kuku, kuna mwanafunzi anasubiri kuchapwa fimbo kwa sababu ameshindwa kufikisha wastani wa 50 kwenye shule isiyo na walimu. Ni jadi yao kuagiza shisha kila ripoti ya mkaguzi inapotoka- wanatuona kama tulivyo, jinsi walivyotaka tuwe- waoga wa kuwawajibisha watu wenye madaraka wanapokosea.

Adolf Hitler, ana meza ya peke yake kwenye safu ya watenda dhambi mashuhuri. Ungeiona sura yake juzi- ya mtu anayejuta, kana kwamba kagundua damu zote ni nyeusi usiku- pale ombi lake la kuongezwa kiti kwa ajili ya malkia Elizabeth pembeni yake lilipokataliwa. Yeye haoni tofauti ya alichokifanya kwa wayahudi na alichofanya malkia kwenye MAUMAU. Haelewi kwanini bado tunaiabudu mifumo iliyotuweka kwenye utumwa, haimuingii akilini kwanini maraisi wa Afrika walikubali kujazwa kwenye basi kwenda kutoa heshima kwa malikia ambaye; sio tu kwamba alikataa kulipa fidia za ukoloni, lakini pia aligoma kuomba msamaha kwa unyama aliofanya duniani.

David Livingstone yupo pia, mahali. Alikuja Afrika na zaidi ya kueneza injili, na ndio maana mkataba wake na mbingu unahusisha mapumziko ya miezi miwili hapa, kila majira ya joto. Mwaka 1866, kutoka Zanzibar aliisihi Buckingham: “Tumeshinda beti, njooni na kila kitu.” Ushahidi pekee wa barua kutumwa ni unyanyasaji ulioikumba Afrika kwa miaka iliyofuata. Alihubiri kuhusu upendo, ‘akatufundisha’ ukarimu, akaiweka hofu ya Mungu mioyoni mwetu-halafu, kama kazi ilivyotaka- akatusihi tuvumilie mateso na kumuachia Mungu mambo yaliyo ndani ya uwezo wetu.

Amefanikiwa.

Hakuna hata neno moja lililofutwa wala kuongezwa kwenye mafundisho aliyoacha. Yeye anaujua ukweli; wanaoenda mbinguni-kama unamuamini Yehova- ni wale tu wanaoweza kutofautisha dini na Mungu. Anashindwa kuelewa itachukua miaka mingapi zaidi kulielewa hilo! Anajua fikra ni yeye aliyetuaminisha kwamba Mungu atatupiga radi tukijiuliza ukweli; lakini pia, mbona watumwa wa Marekani walipewa Biblia isiyo na hadithi ya Musa akiwakomboa waisraeli kutoka utumwani na walijiuliza na kujifunza mpaka wakaipata?

Katika watu wanaosherekewa sana huku ni Karl peters. Alipofika Tanganyika, hakuupenda upinde wa staili za nywele zilizopamba vichwa vyeusi. Akaamuru nywele zote zikwatwe na zitunzwe ‘vizuri’. Ndicho alichofanya Mwl. Edward kwa wanafunzi wa kozi ya mionzi pale Bugando wiki iliyopita. Aliwanyima wanafunzi mtihani mpaka wanyoe nywele ‘vizuri’. Tofauti kati ya Edward na Karl ni; Karl alizichukia nywele za kiafrika na Edward anaendeleza kazi ya Karl akizani ni mila zetu. Alifanikiwa sana Karl na magavana wenzake, ndo maana mpaka leo tunalipa ng’ombe nyingi zaidi kwa ajili ya mwanamke mweupe, tunaamini tumeumbiwa shida, tunaamini bila viboko mtoto mweusi hatoelewa.

Mfalme leopold na wenzake wanalijua hilo; wameshinda, tumeshindwa.

Ni miaka takribani 30 sasa toka nchi ya mwisho Afrika kupata uhuru kutoka kwa mabeperi. Nchi zingine zilipata uhuru miaka 20 kabla ya hapo. Zilikua na miaka zaidi ya 50 ya kutafta utambulisho wao, miaka zaidi ya 50 ya kuweka mifumo dhahiri kwa ajili ya kuleta uhuru wa mawazo, miaka zaidi ya 50 kuunganisha maji ya ziwa Kivu na kijiji kilichopo pembezoni . Lakini wapi! Bara zima lipo hapa.

Tumeshindwa.

Tumeshindwa kumpa uhuru mjukuu wa babu aliyefariki kwa ajili ya tumaini la uhuru kwa waafrika wote. Tumemnyima elimu binti ambaye bibi yake alilipa kodi ya matiti kisa ujauzito. Tumemfunga jela kijana aliyedirika kutekeleza haki yake ya kikatiba ya kuandamana. Tumemuua mtoto wa miaka 14 kisa ana pua ndefu. Na sababu ni moja…

Hatukuchagua upande baada ya kupata uhuru- na sio tu kwenye utamaduni na njia yetu ya maisha bali pia kisiasa, na kwa sababu hiyo, hatukuwahi kupata uhuru.

Kilichotokea ni kwamba mkoloni aliondoka kimwili tu, kiakiri na kimfumo bado yupo. Mifumo yake ilishakaa kwenye akili zetu kiasi kwamba tukaendelea palepale alipoacha. Ikawa kana kwamba tumeondoa minyoro yenye miiba na kujivika minyororo ya dhahabu. Kana kwamba tumemuondoa mtesi mwenye rangi nyeupe na kumleta mtesi mwenye rangi yetu, anayejua maumivu yetu, anayeijua historia yetu, aliyepitia mateso yetu.

Mtu huweza kuuliza: je tulipigana kumuondoa mtu mweupe au tulipigana tuwe huru. Kwa juu, jibu ni rahisi sana: ili kumuondoa mtu mweupe. Na ndio maana mpaka leo Afrika imejaa mifumo ya kidikteta.

Tunaweza tukasahihisha makosa ya waliotutangulia. Imefika wakati sasa tuchague sisi tupo upande gani, sisi ni wakina nani. Kwasababu njia pekee ya kuleta utawala bora na uwajibikaji ni kujitawala, na hilo halitowezekana bila kujipa utambulisho. Ni mda sasa wa kuacha kuwa mseto wa magharibi na mashariki.

Najua kwamba ilikua ngumu kuchagua kipindi cha vita baridi lakini muda wa kujifanya sisi ni wachanga, tunaohitaji mifumo yote miwili umeshapita. Tuchague moja: aidha sisi ni wanademokrasia au ni wakomunist, aidha tunasimamia haki za binadamu au tunatesa wasiofanana na sisi, aidha mfano wetu wa kuiga ni Marekani au ni Uchina.

Hatuwezi kupata vyote. Hatuwezi kubaki na katiba ambayo nusu yake ni demokrasia na nusu nyingine ni udikteta. Inachosha sana kumuuliza gavana kwanini nchi yetu ya kidemokrasia hairuhusu maandamano ya amani halafu akuambie utulie kwa sababu Somalia wao hawaruhusiwi kuandamana kabisa. Inaumiza sana kwa serikali ya kidemokrasia kujifananisha na nchi za kidikiteta ili kufuta ukubwa wa maovu yake.

Inabidi tuelewe kitu kimoja; sio mchina wala mmarekani, wote wapo kwa ajili ya matakwa yao kwanza, kwahiyo hawana tofauti kwenye hilo. Lakini pia tukumbuke kwanini mababu zetu walipigana. Wao walipigana ili tuwe huru kuongea mawazo yetu, ili tupige kula, ili tupate matibabu mazuri, ili tumuwajibishe kiongozi mla rushwa. Na, ni mfumo mmoja tu ambao unaweza kutupa hayo...

Demokrasia.

Ndio, tuliingizwa kwenye minyororo na waliouleta mfumo huo lakini maisha ni nini kama sio uhuru. Ni muda sasa: wa, kukubali yaliyotokea yametokea, kuacha kutumia demokrasia Jumatatu na kurudia udikteta Alhamisi, kuacha kudanganyana kwamba suluhisho ni nchi za kidikteta kwa sababu hazikututawala.

Ndio pia, tunahaki ya kujiuliza kama wana agenda zingine nyuma, lakini demokrasia ni kitu tunachoweza kupeana sisi wenyewe bila kushurutisha. Ni hivyo tu- mababu zetu walikufa ili sisi tuwe huru na wenye usawa.

Natamani siku moja, kama atakuja mkoloni- na atarudi, awe mzungu, mwarabu au mchina- akute tumeshafuta urithi wote mbaya tulioachiwa, akute kitambulisho chetu kikisema;

JINA- TANZANIA.

KUZALIWA- 26/04/1964.

JINSIA- DEMOKRASIA.
 
True
 
Karibu kusoma
 
Like it
 
Jinsia- demokrasia
 
Nzuri
 
Nice.
 
Nzuri.
 
Nice
 
safi sana, hongera hili bandiko lako liende facebook na twitter.
 
Back
Top Bottom