Hivi kuna uhusiano wa kwenda Ulaya na kufeli maisha?

Hiki ndicho Wabongo wasichooelewa. Na hawataelewa hadi siku watakapotoka Tanzania. Na kwa sababu hawatotoka, watakufa tu bila kuelewa. Watu wana hela kwenye nchi zilizoendelea lakini wanapanga mwanzo hadi mwisho.Cash ni muhimu sana ktk nchi zilizoendelea kuliko assets.

Ila marekani hali ni tofauti. Watu hawapendi kupanga maana mifumo ya kumiliki nyumba ni rahisi.
 
Wapangaji ni wengi hata US kuliko wenye nyumba zao. Hii ni kweli kwa kila nchi. Ila ninachosema ni kuwa ile hamu ya kuwa house ower siyo deep km ilivyo kwa Watanzania. Nchi zilizoendelea watu walio wengi hawana nyumba kwa kuchagua, siyo kwa kukosa means.
Ila marekani hali ni tofauti. Watu hawapendi kupanga maana mifumo ya kumiliki nyumba ni rahisi.
 
Hiki ndicho Wabongo wasichoelewa. Na hawataelewa hadi siku watakapotoka Tanzania. Na kwa sababu hawatotoka, watakufa tu bila kuelewa. Watu wana hela kwenye nchi zilizoendelea lakini wanapanga mwanzo hadi mwisho.Cash ni muhimu sana ktk nchi zilizoendelea kuliko assets.
Mifumo ya huko Ulaya kutojenga Ni sawa,msitufanye hatujui kwamba Ulaya kujenga sio issue,Sasa kufananisha Mambo ya Ulaya na bongo huko Sasa Ni kujizima data.eti kisa Ulaya hawapimi maendeleo kwa kujenga nyumba unaleta kipimo hicho huku bongo,my friends pangeni Sana nyumba mkiwa huko Ulaya Ila jengeni nyumbani mkirudi huku mnakuwa wasumbufu Sana tafadhali mjenge pa kufikia unless mmeamua hamtorudi Tena kuishi huku...mkiambiwa mnakimbilia kutuambia hatuna exposure wakati Kuna wenzenu wako huku wanahangaika kujibanza kwenye nyumba za watu na waliokuwa wana majibu Kama haya yako... wake up
 
Nyie jengeni ili siku mkifa, mnawaachia watoto nyumba. Sisi tutawaachia $$. Cash is king. Wakitaka kununua nyumba, watanunua wenyewe. Kila munu ave na kwao... Mtu amenunua maviwanja kama hatokufa siku moja. Akipata milioni 2, huyo anakwenda Mabwepande kununua kakiwanja... Hana hela benki, amejaza maviwanja tu mikoa mbalimbali! Halafu anajiona mjanja!
Mifumo ya huko Ulaya kutojenga Ni sawa,msitufanye hatujui kwamba Ulaya kujenga sio issue,Sasa kufananisha Mambo ya Ulaya na bongo huko Sasa Ni kujizima data.eti kisa Ulaya hawapimi maendeleo kwa kujenga nyumba unaleta kipimo hicho huku bongo,my friends pangeni Sana nyumba mkiwa huko Ulaya Ila jengeni nyumbani mkirudi huku mnakuwa wasumbufu Sana tafadhali mjenge pa kufikia unless mmeamua hamtorudi Tena kuishi huku...mkiambiwa mnakimbilia kutuambia hatuna exposure wakati Kuna wenzenu wako huku wanahangaika kujibanza kwenye nyumba za watu na waliokuwa wana majibu Kama haya yako... wake up
 
Nyie jengeni ili siku mkifa, mnawaachia watoto nyumba. Sisi tutawaachia $$. Cash is king. Wakitaka kununua nyumba, watanunua wenyewe. Kila munu ave na kwao... Mtu amenunua maviwanja kama hatokufa siku moja. Akipata milioni 2, huyo anakwenda Mabwepande kununua kakiwanja... Hana hela benki, amejaza maviwanja tu mikoa mbalimbali! Halafu anajiona mjanja!
Endelea kujizima data...kupanga Ni kuchagua
 
Wasalaam wanajamvi.

Jamani kuna jambo linanifikirisha kwa muda sasa, hivi kuna uhusiano wowote kwa vijana wa makamo wanaorudi toka ughaibuni na kufeli maisha? Nimekutana na case Kama tatu hivi ambazo zimenivuruga kichwa. Nitazielezea kiufupi.

1. Katika hekaheka za humu duniani nilikaribishwa kwenye house party moja maeneo ya Salasala, ilisheheni mbwembwe za kila aina, nilikuwa na wadada warembo na wakaka wamotoo, kila mtu alijifanyia ni mmarekani, Siku hiyo nilijiona nimeokota dodo chini ya mchongoma kwani Kuna jamaa very presentable aliyetambulishwa Kama ndio fresh karudi zake kutoka ughaibuni alitokea kunitunuku. Hapo ndio ulikuwa mwanzo wa penzi tamu nikiwa na matarajio kibao.

Picha linaanzia huyu Bwana hana hata nyumba, kapewa nyumba na wazazi wake maeneo ya Tangi bovu ndio anaishi hapo, huyu Bwana sifa ya umalaya hakubarikiwa, yeye ni mlevi hujapata ona, akiamka asubuhi anaoga, anawasha zake muziki anaanza kunywa whiskey jamani ni asubuhi ya saa tatu, hiyo Ni mpera mpera mpaka atavyolala Sasa sita. Alikuwa anapenda kupika mwenyewe, anapika anakula kidogooo vyote najilia mie yeye anatwanga mipombe yake.. Baada ya miezi kadhaa nikaanza muuliza ana mpango gani wa maisha? Kazi au biashara hana jibu sahihi.. Nina search zoom namuonyesha nafasi za kazi jibu lake sawa nita apply, miezi inayoyoma yule bwana hastuki wala nini. Imagine mtu ana 41 anapewa pocket money na mama..

Nikaanza lalamika kwa ndugu zake wa karibu, mtoto wa baba yake mdogo akaniita faragha "Kama kweli una ndoto na maisha yako hapo unapoteza muda wako buree huyo hajarudi na kitu chochote zaidi ya begi lake na picha za kwenye barafu, huko Germany hajasoma chochote na wala huku nyumbani hajainvest kitu chochote kufupi Ni kwamba"Kaenda KUZURURA miaka Saba halafu karudi hoi.. Nikachoka na penzi likafa.. Ila penzi lake lilikuwa tamu sana hana kero, muelewa, romantic kwa kweli abarikiwe Sana na atolewe tozo kwenye kila muamala ataofanya.

2. Huyu ni kaka wa best friend wangu, siku anaondoka hadi airport tumemsindikiza akielekea UK akiahidi ahadi kedekede lazima apambane atoke kimaisha kwamba nafasi aliyoipata hawezi chezea. Jamani kaenda huko miaka sita baadae hata nauli ya kurudi ilibidi atumiwe, karudi hana hata mia yupo tu amekuwa mwamba wa kupiga virungu.

3. Huyu wa tatu nahisi ndio kamaliza Ulaya yoteee kikubwa anachomiliki Ni saa aina Seiko anadai Ni original alinunua Milan, simu yake ya smartphone, kiingereza kilichonyooka na album yake ya Google photos ikiwa imesheheni picha pambe kabisa zenye mandhali ya kuvutia sana. Nae kwa virungu na uchawa hajambo.

Sasa Hawa Ni mfano tu wa wengi wanaokwenda huko ughaibuni na kurudi tee. Hebu tuwaulize nyie mnaojiita Diaspora huko huwa mnafanya nini? Wenzenu huku nyumbani Mambo yetu ni bambam tumeoana, tuna watoto, tunaishi vizuri. Sasa huko jamani mbona Kama mnapoteza muda Ila mkitupia picha mnatuvimbia kwelikweli ilihali si uhalisia.

My Take Kama huko Mambo meusi rudini nyumbani tujenge nchi. Nyie vijana wenye ndoto za kwenda kusaka tonge huko ughaibuni nawashauri mpambane tu hapa nyumbani mtatoboa unless mkachukue elimu mrudi.
Wakachukue elimu warudi, that is the word!
 
Mimi Niko bongo hapahapa ila Mwanaume ambae anatafuta maisha kiasi Cha kuizunguka dunia hawezi kuitwa amefeli hata kama bado hajapata/hajafanikiwa huyo anaitwa mpambanaji, ndo maana askari anaefia vitani bado anazikwa kwa heshima hata kama hakushinda vita ila ujasiri wake wa kusimama katkat ya njia za risasi unatosha kupewa heshima.

Bali mwanamke asie na mapenzi ya dhati ambae anaingia kwenye mahusiano na mtu asiempenda ila anautoa mwili wake kingono kwa mategemeo na nia ya kupata hafadhali ya kimaisha kupitia mgongo wa mwanaume mtafutaji mwanamke huyo ndo amefeli maisha, maana utatumika sana na wanaume wanaoigiza maisha Hadi utachakaa
nionyeshe kitufe cha kugonga likes mara mbili.
 
Umenena Vyema Sana mkuu....nimependa hapo kwenye"Wake Up Call"nadhani watakuelewa
Yaan wabongo sio hustler kama walivyo wanigeria kwa hiyo ni kama tatizo la kirithi la nchi sisi tumeridhika sana na maisha ndo changamoto kubwa tuliyonayo

Nchi kama marekani, Canada au any western Europe kutoboa ni ngumu kinyama inabid uwe exception a.k.a utumid kipaji ndo utatoboa kirahis, kule competition ni kubwa sana mim mda si walaumu

Wengi wakirudi wanakua na kama Wana mental unstable walichotegemea kule ni tofauti alafu huku tunatarajia makubwa kutoka kwao hio ndo changamoto

Wengi wanaoenda huko ulaya ni watoto wa-kishua wanajua nyumbani Kuna ela, tofauti na wanaoenda south Africa ni watoto wa mbwa kule wanaenda kutafuta Ela ndo maana ni rahisi kwao kutoboa
 
Hii mada tulishawahi kuiongelea hapa. Wengi Wabongo wenye bahati wanaoenda ughaibuni ni maboya. Wakifika kule wanaiga life style ya wenyeji,anasahau huku nyumbani anatakiwa afanye kitu.

Mfumo wa maisha ya ulaya ni rahisi sana kutoboa ili mradi tu ujitambue. Miaka 7 kukaa Ulaya kama unajitambua unarudi na hela ambayo kwa hapa bongo angeihangaikia maisha yake yote,asipate hata robo yake. Uwe tu na nidhamu ya pesa.Kule kuna kazi nyingi ambazo wenyeji hawataki kuzifanya wanaziona za kirock,kama udereva wa magari makubwa,kupanga mabox kwenye mashopaz,kurudishia bidhaa kwenye mashelvu. Na mshahara wake ni mnono,kiasi unaweza ukamzidi hata boss wa TRA kibongobongo. Kikubwa panga matumizi yako vizuri. Achana na starehe,starehe waachie wenyeji. Sasa unakutana na mbongo kama huyo wa kwanza anaiga life Style ya wenyeji,nae anakuwa hataki hizo kazi. Pili ni machinoo. Pombe kuanzia asubuhi,maisha ya kizungu sana. Huwezi kutoboa.

Kenya uwekezaji mkubwa mkubwa ule unaouona ni vijana wanaoishi ulaya. Ona vijana wa Nigeria pia,wametapakaa ulaya. Ona uwekezaji wao kwenye nchi zao.

Pia unawaona wasomali wanaamua liwalo na liwe wanasafirishwa kama mizigo ili mradi afike South Africa. Akifika South Africa kule ni njia tu ya kuunga ulaya. Na wakifika ulaya haichukui round anakuwa mfadhiri wa ndugu na jamaa zake huko kwao. Unafikiri pesa anaitoa wapi,kama sio kufanya kazi?. Wapo wanaoishia hapo south. Ujue yule uliemsafirisha leo kwa loli,na yule utakaeenda kumkuta South Africa miaka miwili ni tofauti sana. Miaka hiyo miwili atakuwa amepiga sana hatua kimaendeleo. Wanajituma sana wakifika huko tofauti na wabongo wanaoenda huko wengi wanapenda starehe. Mwisho wa siku wanaangukia kwennye sembe. Mpaka sasa vijana wa kibongo waishio south,wengi ni wezi na wauzaji na kutumia sembe ksbb ya kupenda starehe bila kufanya kazi.

Ipo mifano ya watu ninaowafahamu wanaopiga kazi ulaya. Wengine wameingia kule kwa gear ya kusoma,lakini wanapiga na kazi pia. Mmoja anajenga apartment 9 za ukweli mkoa fulani hapa nchini.

Kwa hiyo wengi hawafanikiwi ksbb hawajitambui,wanaendekeza starehe.
Hizo kazi za amazon usifikirie utani unaweza kufa mapema.. halafu ulaya kodi utawaambia nini.. wengi wanaokuja huku kwa kujilipua wanatumia pesa ya serikali tuu ya ulaya wanazaa watoto hata 7 ili pesa za watoto watumie waoulaya kama huna elimu umejiingiza kwenye matatizo makubwa sana huwezi toboa
 
Hizo kazi za amazon usifikirie utani unaweza kufa mapema.. halafu ulaya kodi utawaambia nini.. wengi wanaokuja huku kwa kujilipua wanatumia pesa ya serikali tuu ya ulaya wanazaa watoto hata 7 ili pesa za watoto watumie waoulaya kama huna elimu umejiingiza kwenye matatizo makubwa sana huwezi toboa
Western world ili uishi vizuri inatakiwa kipaji chako mixa uwe mwanamichezo yaan uwe na kitu Cha utofauti tofauti apo hata kama una degree kumi na sio exception utaishia mediocre na maisha ya stress na depression umo umo kule pagumu sana sio sehemu ya kukimbilia bila kuwa na target
 
Western world ili uishi vizuri inatakiwa kipaji chako mixa uwe mwanamichezo yaan uwe na kitu Cha utofauti tofauti apo hata kama una degree kumi na sio exception utaishia mediocre na maisha ya stress na depression umo umo kule pagumu sana sio sehemu ya kukimbilia bila kuwa na target
Kwasababu tuchukue mtu analipwa mshahara wa 2000€ kazi ngumu, hapo kodi kama huja familia wanachukua chao kama 30% wewe kodi ya nyumba kama mji mkubwa si chini ya 700€ unabaki na nini hapo.
 
Back
Top Bottom