Hivi kuna uhusiano wa kwenda Ulaya na kufeli maisha?

Kwa comments hizi tutaendele kushuhudia watu kama kina Obama wanatokea kwa Wenzetu.
West Africa, mtoto anachangiwa pesa ili azamie, akatafute maish sisi tunasema bora kwetu wakati Africa tunaijua na kwetu tunajua n tunaona palivyo.
Kwa ufupi fighting spirit ya Wabongo wengi nje ni ndogo, mmatumbi anataka kuiishi Paris kama mzungu lazima life likupige K.O
Wabongo sio hustler kabisa, sisi sio wapiganaji ndo maana ni nadra kusikia diaspora ni maarufu au kafanya kitu flani

Mfano angalia kwenye wachezaji wengi kama wakina Saka, Tammy Abraham, giannis unaona kabisa hata diaspora wakibongo sio wapambanaji ni tatizo kubwa sana linaloisumbua jamii yetu
 
Kwasababu tuchukue mtu analipwa mshahara wa 2000€ kazi ngumu, hapo kodi kama huja familia wanachukua chao kama 30% wewe kodi ya nyumba kama mji mkubwa si chini ya 700€ unabaki na nini hapo.
Mim siwez walaumu wanafeli kwa Sababu western world kugumu sana, at least wanaoenda kama ma-experts kitu ambacho kwa watanzania ni kigumu sana kutokana na ubovu wa elimu yetu na mentality ya kibongo
 
Umesema huku mambo pambe mmeoana.
Sasa kama mmeoana kipi kilikupelekea kudanga na huyo kaka wa Kibongo /Kimarekani?
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Ni wehu ni wachache sanaa wanakumbuka kujiwekeza wengi wao ni wehu blaza wangu wa pili anaishi UK mwaka wa 12 sasa hana nyumba wala mke wala mtoto japo yeye ni artist anijiweza kidogo huwa anakuja na kuondoka lakini abachofanya bongo hakuna hata kibanda
 
Na nyie mnaoponda diasporas mnajua ni wangapi wamekwamishwa na kurudisha nyuma na ndugu zao waliopo hapa nyumbani? Watu wanatuma hela wajengewe wanatumiwa picha za uongo watu wanakula hela, wapo waliofungua miradi kibao ndugu wakaiua. Kwahio mkiona watu wamerudi hawana kitu msihukumu hamjui kilichowasibu.
 
Hizo kazi za amazon usifikirie utani unaweza kufa mapema.. halafu ulaya kodi utawaambia nini.. wengi wanaokuja huku kwa kujilipua wanatumia pesa ya serikali tuu ya ulaya wanazaa watoto hata 7 ili pesa za watoto watumie waoulaya kama huna elimu umejiingiza kwenye matatizo makubwa sana huwezi toboa
Sio kweli.
 
Wasalaam wanajamvi.

Jamani kuna jambo linanifikirisha kwa muda sasa, hivi kuna uhusiano wowote kwa vijana wa makamo wanaorudi toka ughaibuni na kufeli maisha? Nimekutana na case Kama tatu hivi ambazo zimenivuruga kichwa. Nitazielezea kiufupi.

1. Katika hekaheka za humu duniani nilikaribishwa kwenye house party moja maeneo ya Salasala, ilisheheni mbwembwe za kila aina, nilikuwa na wadada warembo na wakaka wamotoo, kila mtu alijifanyia ni mmarekani, Siku hiyo nilijiona nimeokota dodo chini ya mchongoma kwani Kuna jamaa very presentable aliyetambulishwa Kama ndio fresh karudi zake kutoka ughaibuni alitokea kunitunuku. Hapo ndio ulikuwa mwanzo wa penzi tamu nikiwa na matarajio kibao.

Picha linaanzia huyu Bwana hana hata nyumba, kapewa nyumba na wazazi wake maeneo ya Tangi bovu ndio anaishi hapo, huyu Bwana sifa ya umalaya hakubarikiwa, yeye ni mlevi hujapata ona, akiamka asubuhi anaoga, anawasha zake muziki anaanza kunywa whiskey jamani ni asubuhi ya saa tatu, hiyo Ni mpera mpera mpaka atavyolala Sasa sita. Alikuwa anapenda kupika mwenyewe, anapika anakula kidogooo vyote najilia mie yeye anatwanga mipombe yake.. Baada ya miezi kadhaa nikaanza muuliza ana mpango gani wa maisha? Kazi au biashara hana jibu sahihi.. Nina search zoom namuonyesha nafasi za kazi jibu lake sawa nita apply, miezi inayoyoma yule bwana hastuki wala nini. Imagine mtu ana 41 anapewa pocket money na mama..

Nikaanza lalamika kwa ndugu zake wa karibu, mtoto wa baba yake mdogo akaniita faragha "Kama kweli una ndoto na maisha yako hapo unapoteza muda wako buree huyo hajarudi na kitu chochote zaidi ya begi lake na picha za kwenye barafu, huko Germany hajasoma chochote na wala huku nyumbani hajainvest kitu chochote kufupi Ni kwamba"Kaenda KUZURURA miaka Saba halafu karudi hoi.. Nikachoka na penzi likafa.. Ila penzi lake lilikuwa tamu sana hana kero, muelewa, romantic kwa kweli abarikiwe Sana na atolewe tozo kwenye kila muamala ataofanya.

2. Huyu ni kaka wa best friend wangu, siku anaondoka hadi airport tumemsindikiza akielekea UK akiahidi ahadi kedekede lazima apambane atoke kimaisha kwamba nafasi aliyoipata hawezi chezea. Jamani kaenda huko miaka sita baadae hata nauli ya kurudi ilibidi atumiwe, karudi hana hata mia yupo tu amekuwa mwamba wa kupiga virungu.

3. Huyu wa tatu nahisi ndio kamaliza Ulaya yoteee kikubwa anachomiliki Ni saa aina Seiko anadai Ni original alinunua Milan, simu yake ya smartphone, kiingereza kilichonyooka na album yake ya Google photos ikiwa imesheheni picha pambe kabisa zenye mandhali ya kuvutia sana. Nae kwa virungu na uchawa hajambo.

Sasa Hawa Ni mfano tu wa wengi wanaokwenda huko ughaibuni na kurudi tee. Hebu tuwaulize nyie mnaojiita Diaspora huko huwa mnafanya nini? Wenzenu huku nyumbani Mambo yetu ni bambam tumeoana, tuna watoto, tunaishi vizuri. Sasa huko jamani mbona Kama mnapoteza muda Ila mkitupia picha mnatuvimbia kwelikweli ilihali si uhalisia.

My Take Kama huko Mambo meusi rudini nyumbani tujenge nchi. Nyie vijana wenye ndoto za kwenda kusaka tonge huko ughaibuni nawashauri mpambane tu hapa nyumbani mtatoboa unless mkachukue elimu mrudi.
Wacha nifunge mdomo wangu and mind my business!!..Kuna ukweli wa haya uliyojaribu kuelezea lakini yanafichwa sana!!..
 
Huyo mwamba wa tano ungeendelea naye tu,sioni tatizo, kama kwao pesa zipo na wanampa na nyumba tayari kashapewa tatizo liko wapi. Nimemfurahia yeye hana ubinafsi ameachia watu wengine wanaotoka familia maskini wapate kazi wajikombe ila yeye alishakombolewa zamani na wazazi wake.

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
 
Wacha nifunge mdomo wangu and mind my business!!..Kuna ukweli wa haya uliyojaribu kuelezea lakini yanafichwa sana!!..
Ongea tu , ukiishi ughaibuni lazima uwe na discipline ya maisha usilete maisha yako ya kibongo huku, hamna cha born town au mission town huku. Ughaibuni usipofanya kazi kwa bidii basi na maisha yako yatakua ya kizembe zembe hivyo hivyo. Vijana wengi walioenda ughaibuni kuanzia 2005s walienda kwa nia wakirudi bongo wawe wametusua wakakuta hali sio hali ndio hao nafikiri wanaongelewa wamekwama, lakini wale walioenda 1990s wengi wao walienda kuishi ma mbele na kurudi bongoland ni majaaliwa. kuna tofauti!!!
 
Ongea tu , ukiishi ughaibuni lazima uwe na discipline ya maisha usilete maisha yako ya kibongo huku, hamna cha born town au mission town huku. Ughaibuni usipofanya kazi kwa bidii basi na maisha yako yatakua ya kizembe zembe hivyo hivyo. Vijana wengi walioenda ughaibuni kuanzia 2005s walienda kwa nia wakirudi bongo wawe wametusua wakakuta hali sio hali ndio hao nafikiri wanaongelewa wamekwama, lakini wale walioenda 1990s wengi wao walienda kuishi ma mbele na kurudi bongoland ni majaaliwa. kuna tofauti!!!
Wewe Una nini Ndugu!!.. Unadhani wote humu hatujawahi kuishi ulaya,Marekani na Gulf?!!..Hebu tuliza matako yako huko!!!..
 
Dada acha kutaka mawazo yako ndio yaonekane legit.

Mimi Nina ndugu yangu Ni anko wangu yuko Canada. Dar ana viwanja si chini Ya 10. Na vitano viko kwenye very prime area. Ana hotel moja iko njia ya Morogoro road.

Kiwanja Cha mwisho aliniingizia hela mimi kwenye account yangu ili anunue eneo liko sinza. Sasa imagine mtu ananunua eneo sinza.

So acha kuwa naive and stop that generativity mentality.


Nina mengi ya kuandika kuhusu ndugu zangu wengine watatu walioko huko na kufuru walizofanya bongo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom