Hivi kuna uhusiano wa kwenda Ulaya na kufeli maisha?

Sababu ya pekee ya kwanini bado nipo viunga vya Bongoland ni kwasababu nataka kuwa fisadi. Yaani shortcut za huku na ujanja ujanja mwingi hasa ukizipata "passwords " Sina kingine wajameni, kinyume na hapo ningeshatimka siku nyingi sana.

We nchi gani hii hata ukipambana kupaweka kwako vizuri kiasi gani na ukawa organised utatoka nje ya geti lako utakuwa disappointed na majirani zako, nchi gani hakuna uniformity ya kitu chochote mambo shangalabaghala kila kona. Nchi gani hata ukusanyaji wa taka tu ni tatizo hahah nacheka kwa huzuni sana.

Bongo kugumu sana alooh tunakaza mno ma.tako, sio kwamba huko kwingine ni kurahisi la hasha! Mimi nazungumzia mambo mengine kabisa, mambo ambayo kibongo bongo hata ukiwa na pesa utapambana nayo tu. Acha tuzitafute passwords tupige mpunga basi, nchi hii hovyo sana.

Hata biashara za huku kwetu ni ndogondogo sana, uwezo wa watu wengi kufanya manunuzi ni mdogo sana wajasiriamali watatajirikia wapi?

Nafuu kwa Diaspora mara 100! Tuendelee kupambana kila mtu kwa sehemu alipo.
 
Fanya ile makitu roho napenda...unaweza kwenda ulaya ukawa tajiri mara moja.....na usitamani kurudi....de viceversa is true!!.....tatizo la wabongo wengi wanaangalia na kujifunza kwa failures!!
 
Nadhani sio kweli.

Hata hapa bongo kuna waliofanikiwa na waliofeli vilevile.

Kuna jamaa namfahamu alienda kusoma Uingereza mwanzoni mwa miaka ya tisini akalowea huko huko. Anafanya kazi kwenye taasisi moja kubwa ya kifedha duniani ana pesa hatari. Kipindi cha Kikwete aliwahi kufanya kazi BOT akaona miyeyusho akarudi zake Ulaya.

Kuna wabongo ni ma-engineer wa kutegemewa wanafanya kazi kwenye mashirika makubwa ya dunia.

Wewe unakutana na vichaa wachache, walioenda Ulaya kula unga na kufukuzia nyuchi za kizungu unachukulia wote wako hivyo. Unafeli.
 
mmmh same same here, ndugu yangu 7 years huko alirudi na begi pia lina track suit moja na viatu vitatu kila kimoja hakina mwenzie 🤔
🤣😂🤣. Dah, nimecheka sana na hii comment kama vile ni mazuri. Haya maisha haya!! Sasa mlimwuuliza wenziwe wa viatu alipeleka wapi?
 
Sio wote wengine ndugu zetu waliokimbilia huko ndio wanatuokoa.
Bongo hii maisha ya kifala sana tena ukute unadegree ya sociology kama yangu bora ukimbilie tu huko ikabebe box
Mkuu usiilaumu degree yako, usicheze mbali na waliofanikiwa ..ukipata connection utatoboa na hakuna wa kukuliza hata hiyo degree yako.. !

Wapo madogo wamesoma vyou vya snaa hapo bagamoyo tena certificate na hata kumaliza wengine hawakufanikiwa lakini wanakula mashavu balozi mbali mbali...!

Usikomar sana na njia moja pekee mkuu..! Usicheze mbali na waliofanikiwa , upate connection
 
The diaspora is not monolithic.

If you associate with people who failed economically, that is a reflection of your poor judjement, small network and its poor reach.

We are out here making big moves.

Na siku hizi hata likizo tunaishia Turks and Caicos, au tukijq Bongo ni kifqmilia zaidi, kwa sababu ya umbeya wa wabongo.

Kama kuna lawama, laumu watu wako specifically, usipakazie diaspora.
Majadala ufungwe ! 😀😀😀
 
Kongole kwa Joannah kuanzisha uzi huu. Ni ukweli usiofichika kwamba baadhi ya diaspora wana hali ngumu huko walipo, na hasa wale ambao wanaishi bila kuwa na documents stahili. Lakini hata wengine ambao ni wanafunzi na wanaruhusiwa kufanya kazi masaa 20 kwa wiki wanaweza kujiwekea savings lakini hawafanyi hivyo. Sana sana wanaishia kununua nguo na sneakers ambazo kwa kweli sio bei ndogo. N sawakirudi bongo na hivyo vinguo vyao na slang yao basi wanaona wame-win only kuja kushangaa waliowaachaa bongo wao wako mbele kimaisha kuliko wao. ila kuna baadhi ya diaspora pia wamefanikiwa sana na wanasaidia sana familia zao bongo, na wao pia wame-invest vizuri kwa ajili wakirudi waweze kujikimu na kuishi maisha mazuri. Badala ya baadhi yetu humu kumshutumu Joannah, tutumie hoja hii hasa kwa wale ambao wako ughaibuni kuona hii kama "Wake Up Call" kwamba tusijisahau sana kwa kuwa kuna siku tutarudi kwetu bongo, na hivyo ni muhimu kujipanga!!!. Au sivyo ndiyo yale ya kurudi nyumbani na begi la nguo, hereni na macheni feki huku mwili una matatoo kibao na huna hata hela zaidi ya dola 2000 mfukoni. Unakuja kutamba na Kingereza ambacho bado ni kibovu anyways, na kujiona uko vizuri, kumbe unachekwa mtaani.

Kama wewe uko nje, kumbuka siku moja utarudi home, hivyo jipange. Hujachelewa. Hata kama umri umeenda, piga miaka yako kama 3 hivi kazi bila kuchoka au kufanya anasa ambazo hazina maana huko. Ukijitahidi, si haba hata ukirudi na dola 150,000 itasaidia kupata kibanda chako cha retirement na chenji kuanzisha mradi wa kukuweza kujikimu bila kuwa omba omba. Itazuia aibu ya kurudi na begi tu na pea tatu za viatu ambaa hata hizo viatu havina mwenzake.
 
Sasa Joannah kipi kimebadilika kutoka miaka hio ya 90 huko Europe na sasa watu hawa win tena wakienda?

Mimi naona uko peke yako unayeona ulaya ni pa kawaida, itisha hapo mkutano wa wanaotaka kwenda ulaya uone watakavyojaa maelfu!

Kisha usitudanganye watu wako better huko Tanzania, wakati familia nyingi hazipati milo mitatu and majority lives under 2 dollars per day...

Mwisho km wewe uko Dar usitufokee, jenga kwenu Chitoholi ,lol, ..sio wote wanokuja Dar,wanarudi vijijini wakiwa successful,the same as ulaya...kila mtu apambane na hali yake popote alipo!..lol
Point !
 
Wachangiaji wwengi hawana experience wala exposure/kusafiri wala kuishi nje /hukobulaya na marekani...

So wanaongea stori za kusadikika ,za kuambiwa na zakuongeza chumvi..

Ni wachache tu humu wenye kuujuwa ukweli!

Wabongo wengi wana tabia ya kufurahia kufeli kwa mtu, yani ukifeli kwao ni sherehe... wanapata faraja kuona mambo ni magumu kwa wote na sio wao tu, hawafurahisi na habari njema za mtu.

Unafki ndio balaa , pamoja na ule ujinga wa masikini jeuri- kujifanya huna shida na kitu fulani wakati " kimoyo moyo" unakaitamani ile mbaya
Hao mdio aina ya wabongo walio wengi ..

Wengi wanaponda sana idea za kusafiri na kuishi nje , lakini wanapopata taarifa za watu walio nje kufanikiwa huwa wanapata wivu na kujenga chuki sana !

Asilimia kubwa ya wanaoenda nje kwa njia halaili na kwania ya kujikwamua kimaisha hufanikiwa tena kwa asilimia kubwa kabisa ...
Kwa maana huwezi kulinganisha maisha ya bongo na U.S au canada ... na ukiona mtu anakwambia "komaa tu hapa hapa fursa zipo nyingi ujue ana akili mgando na hana exposure "

Na kama siku ikatokea akapata chance ya kusafiri, basi atafunguwa akali yake na kujuwa kumbe kuna maisha nje ya mipaka ya tz .!
 
Kwanza kabisa inategemea umeenda Ulaya au America(USA) Kwa sababu Gani,kwa maana ya kwamba visa yako ni ya aina gani...mfano hapa USA naamini na Nchi nyingine pia kuna visa za kazi,shule, utalii etc...So kwa mtu alieko ulaya kwa ajili ya shule au utalii haruhusiwi kufanya kazi, na hata waajiri wanaoga kuajiri haina hii ya watu,ila ukiwa mjanja unaweza kupata kazi ukafanya kimagendo.

So naamini wengi wa hivyo wanakuja kama wanafunzi ,utalii/wamealikwa na ndg na marafiki, so wanakua hawana access ya kazi ya moja kwa moja ya kumfanya aweze kupata pesa ya kutumia na ku save.

Pili, inategemeana na aina ya mtu na mipango yake pia.Kuna wengine hawana mipango mizuri na matumizi mazuri ya pesa...wakifika huku wanasahau walipotokea wanazolewa na tamaduni na maisha ya kampani zao huku
 
Back
Top Bottom